Ipo sheria inayomnyima haki mtumishi wa umma kumiliki kampuni na biashara inayofanana na ile anayoitumikia?

Ipo sheria inayomnyima haki mtumishi wa umma kumiliki kampuni na biashara inayofanana na ile anayoitumikia?

winnerian

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
379
Reaction score
603
Kama ipo sheria inayomnyima haki mtumishi wa umma kumiliki kampuni na biashara inayofanana na ile anayoitumikia umma ifutwe mara moja. Katika ulimwengu wa sasa huwezi kumnyima binadamu kujiendeleza kiuchumi kwasababu tu ya mgongano wa kimaslahi.

Sheria zinazotakiwa kuwepo ni za kulinda mgongano wa maslahi usitokee katika eneo la kazi (conflict of interest) na sio kumfunga mtu pingu za maisha kwamba hawezi kufanya shughuli flani. Madaktari wana miliki hosipitali, maduka ya dawa, zahanati na hawafanywi chochote. Wabunge walitizame hili.

Watumishi Serikalini wapigwa marufuku kumiliki kampuni sawa na kazi wanazofanya

“Mtu huwezi kujichukulia hatua mwenyewe hivyo kwa yeyote mwenye kampuni binafsi ya ujenzi ajichunguze itamletea mgogoro mkubwa na sisi kama Serikali hatuwezi kumvumilia Mtumishi wetu ambaye anakiuka kwa makusudi sheria ya maadili ya utumishi wa umma,”

“kuwa na kampuni binafsi inasababisha mgongano wa kimaslahi hivyo ni ngumu sana kufanya kazi kwa ufanisi na kuzingata mkataba kwani wewe ndio kila kitu hilo halivumiliki na unakwamisha malengo ya serikali kuwafikishia wananchi maendeleo,”

Hizi ni baadhi ya statement za Mh. Kairuki ambazo zinadidimisha juhudi za Mtanzania kujikomboa na umaskini. Sheria zirekebishwe.
 
Navyojua kuna Mamlaka nilikuwa nikifanya kazi, hairuhusiwi kufungua biashara inayoendana na manachofanya pale.
Ila wengi wamefungua, aina hiyo ya biashara kwa majina ya watu wengine. Ngumu kudhibiti hilo.
 
sina hakika ni baadhi tu au kuna zile maalum tu, maana nimeshuhudia madaktari wa umma wakimiliki hospitali na dispensari zao binafsi, Walimu wakiwa na shule zao binafsi etc
 
sina hakika ni baadhi tu au kuna zile maalum tu, maana nimeshuhudia madaktari wa umma wakimiliki hospitali na dispensari zao binafsi, Walimu wakiwa na shule zao binafsi etc
Kweli waafrica sisi tumejifunga funga ba kila aina ya sheria kusudi tu tusisonge mbele
 
Hata ungekuws wewe lazima ungependelea kampuni yako!sheria iko poa sana au acha kazi wafanye wengine maana wewe kuwa na kampuni tayari una ajira ya kudumu, pambana!
 
Hivi ukiwa mtumishi na unabiashara au kampuni unategemea tenda au kazi ziende kwako au mtumishi
Kama ana kampuni awaachie wasio na ajira,huu ni ibinafsi wa kutaka vyote viwe vyako,wakati wengine wanatesema hata mlo mmoja hawana iwe wakati wa mavuno wa jua kwao ni njaa tuu!Sheria iko poa sana.
 
Daktari haruhusiwi kufungua kituo cha afya kwa eneo analofanyia. Mkaguzi wa CAG haruhusiwi kufungua private audit firm. Legal Officer wa Serikali haruhusiwi kufungua legal firm katika eneo analofanyia. Hawa ukikuta wamefanya hivyo ni kinyume na sheria.
 
Navyojua kuna Mamlaka nilikuwa nikifanya kazi, hairuhusiwi kufungua biashara inayoendana na manachofanya pale.
Ila wengi wamefungua, aina hiyo ya biashara kwa majina ya watu wengine. Ngumu kudhibiti hilo.
Huku kwetu imebatizwa jina "conflict of interests"
 
Hata ungekuws wewe lazima ungependelea kampuni yako!sheria iko poa sana au acha kazi wafanye wengine maana wewe kuwa na kampuni tayari una ajira ya kudumu, pambana!
Umetumia wivu kufanya tathmini ya madhara ambayo yanapatikana nasheria mbovu.

Nchini China wanasonga mbele kwa speed ya ajabu kwa kuwezesha kila mtu afanye biashara ilimradi anaingiza kitu.
 
Umetumia wivu kufanya tathmini ya madhara ambayo yanapatikana nasheria mbovu.

Nchini China wanasonga mbele kwa speed ya ajabu kwa kuwezesha kila mtu afanye biashara ilimradi anaingiza kitu.
Hapa sio china!wabongo wataweka vimeo hata wasiojua kufanya kazi,hii bongo noma na bahati mbaya wivu huwa sina napenda maendeleo ya mtu yoyote na nipo tayari kusaidia.
 
Back
Top Bottom