Ndugu zangu Watanzania,
Nimeona nisema haya mapema sana ili yakitokea ya kutokea CHADEMA wasije anza kusema wamehujumiwa na serikali au CCM. Kwa sababu mtu mvivu wa kutumia akili akipata tatizo huwa anakimbilia kutafuta majibu mepesi na marahisi,Kama ambavyo amewahi kusema baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere katika kitabu chake cha Tujisahihishe cha mwaka 1962.
Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa CHADEMA kushindwa kumuandalia Makamu Mwenyekiti wake jukwaa zuri ,la kueleweka na lenye usalama wa kutosha. Yaani makamu Mwenyekiti anapewa meza ya kupangiaa nyanya na vitunguu sokoni tena iliyochakaa,kuchoka,kupauka na mbaya sana ili itumike kama jukwaa? Yaani CHADEMA inashindwa kuchangishana pesa kununua mbao ili kutengeneza jukwaa zuri ,la kueleweka na lenye usalama?
Chama bora,makini ,imara na chenye weledi kama CCM huwa kina mpangilio mzuri sana wa mambo yake ambayo yanakuwa yanaakisi afya njema ya akili ya wanachama pamoja na viongozi wake.ukiona chama kinashindwa hata kuandaa tu jukwaa la kiongozi wake mkubwa kama Makamu ,basi ujuwe ndio akili za viongozi wake zilipogota na kufikia. Mpangilio wa vitu huanzia akilini,kichwani nakuja katika matendo. Haya ya kumpatia Lissu meza na kupangiwa matofali chini kwa hakika ni aibu ya karne,ni maajabu yanayo takiwa kuingia katika maajabu ya Nchi na Bara la Afrika.
CHADEMA haijawahi kuwa siriasi,ni chama kipo kipo tu,kinajiendea endea tu kama kipofu gizani.kinajisukuma sukuma tu kama mtu aliyezidiwa na Pombe kichwani.hakina mipango wala mikakati wala maono wala malengo hata ya urefu wa pua zao. Hakiwezi hata kupanga nini kitafanya kesho. ndio maana hakiwezi hata kuweka mipango na maandalizi juu ya jukwaa atakalotumia kiongozi wake kuzungumza na watu.
CHADEMA walivyo wavivu wa kufikiri na kutumia akili vyema ,ikitokea Lissu akaanguka na kuumia Vibaya Mwili wake,utaona kwa ufinyu wa akili wanaanza kuitupia lawama serikali yetu na chama chetu cha Mapinduzi CCM kuwa ndio imesababisha.watasema Lissu na CHADEMA wamehujumiwa.halafu haraka sana kama kawaida yao wataanza kutoa namba za kuomba michango ya kumtibu hospitali na gharama zingine.Maana hiyo ndio kazi ambayo CHADEMA inaweza kuifanya kwa ufanisi mzuri sana, kutokana na kupenda sana pesa za bila jasho.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.