Hayo ''mapumbavu'' yaliyoandamana yamefanya hivyo kwa sababu ya tamaa binafsi i.e. yanatetea matumbo yao. Sijui ni kwa nini Mbowe hashtuki. Alisema familia yake inamlilia sana asiendelee lakini ''familia'' ya CHADEMA inamashinikiza aendelee. Kitu ambacho hajui ni kuwa familia yake inampenda ndiyo maana inampa huyo ushauri wakati ''familia'' ya CHADEMA'' inamtumia tu. Kuna siku atakuja kugundua hili.
Ni kweli ninayaita mapumbavu kwa sababu siku Mbowe alipoitisha maandamano ambayo bila shaka yangeleta mabadilko makubwa sana kwa watawala na hata uchaguzi wa serikali za mitaa usingekuwa wa kiduwanzi kama ulivyokua, Haya mapumbavu hawakutoa pua zao nje kuandamana isipokua Mbowe peke yake na watoto wake walioona ni bora kufa na baba yao.
Watoto wa Mbowe kwa kweli walionyesha upendo mkubwa sana lakini Familia ya Chadema mapumbavu kabisa hayakutoka walimwacha mbowe peke yake na kujikuta anakamatwa kama Kibaka anayeiba kuku .Halafu eti wote wanampenda .
Mbowe aking'atuka kwa heshima atakua amejijengea heshma kubwa sana na naamini Siku moja huko Mbeleni Mtoto wake atapewa tena Uenyekiti wa Chama kwa heshma kubwa ya baba yake .
Alilazimishwa kugombea ni wazi kuwa anaweza akashinda kutokana na pesa nyingi zinazozunguka zilizotokana na uuzwaji wa Bandari. Wajumbe wa atapigwa pesa za kutosha na wanaweza wakamchagua kulinda maslahi na nafasi zao.
Lakini pia Mbowe alipogombea ni wazi hata haya mawe tunayoyapiga huku hatutayapiga na tutamuaga kwa heshma kubwa sana na kwa mbwembwe kubwa na kwa raha kubwa sana atakapokua anapita mikoani kumtambulisha mwenyekiti mpya . Hakika Mbowe asipogombea atajijengea heshima kubwa sana sana.
Kisu ndiye mtu sahihi kwa sasa ambapo Ufisadi ni mkubwa na watanzania kwa sasa hakuna mtu wanayemwamini kama Lisu na Mwabukusi.
Huku akikaa Lisu kule Mwabukusi. Wananchi wakiwa na matumaini ya kumpata kiongozi anayeweza kusimamia sheria na kulinda watu wake na kushawishi jumuiya za kimataifa kuwawekea vikwazo majizi yanayaoliibia Taifa hili na kwenda kuficha mapesa huko Dubai na Marekani nadhani patachangamka sana .
.