Unaota au unaongea tu ili kujifurahisha? Kwa kiwango cha uwoga wa Watanzania ninayoijua, CCM kuondoka madarakani itachukua karne nyingi mnoooo.
Yaani katika dunia ya leo pamoja na utandawazi, elimu na teknolojia ya mawasiliano uliyopo bado CCM waliweza kuvurga uchaguzi na kuingiza makada wao zaidi ya asilimia 90 kwenye bunge, na hakuna hata wananchi walioonyesha hasira na kutokuridhishwa na matokeo ya uchaguzi kwa namna yoyote ile? Alafu itegemee kwamba ipo siku CCM itakubali tu kiulaini eti tuandike katiba mpya, au tufanye tume ya uchaguzi iwe huru?
Mimi ndoto za mchana sipendi kabisa. Watanzania ni mazezeta ndo maana wanatawaliwa kindezi na watatawaliwa bado na CCM kwa miongo mingi sana.
Yaani kiongozi wa upinzani anakamatwa kindezi na kubambikiziwa kesi eti badala watu wakinukishe wanabaki kusubiri mataifa ya kigeni yawapiganie na wanafurahi kuona wawakilishi wa mabalozi wakijumuika nao mahakamani?
Badala ya kuitumia hiyo kama fursa, wakinukishe ili jumuiya ya kimataifa ione dhahiri kwamba watu wamechoka waingilie kati kwa kuwasaidia kuibana serikali. Kwa utulivu uliyopo bongo, hakuna serikali ya nje inayoweza kuibana CCM kwasababu itakuwa ni uchokozi wa wazi kabisa ila pangetifuka, uchumi uvurugwe hasa na pasikalike, mbona wangetafuta wapatanishi na kuunda tume huru?