Ipo siku Wapinzani watatamka hadharani kuwa Watamuunga mkono Rais Samia Uchaguzi ujao

Chakula Bei Juu, Wewe Unakwenda Lumumba Kusaini Huyaoni
Kilimo Ni Biashara kwa Sasa,Acha wakulima wafaidike na jasho lao maana kwa muda mrefu Sana wameumia Sana katika kubeba mzigo wa kulilisha Taifa hili lakini mwisho wa siku waliokuwa watu wa kupangiwa Bei na mahali pa kwenda kuuza , mpaka wakati huu alipopatikana mfariji wao na mkombozi wao Rais Mama Samia Suluhu Hassan aliyekuja kuwashika mkono na kuwafuta machozi yao
 
oya Mwashambwa hii namba uliyoacha inapokea pesa?
 
Labda kwa ccm B lakini kwa chadema utasubiri sana.
 
Kafanya Jambo gani lililowagusa WANANCHI moja Kwa moja ukitoa Hili la kuruhusu mikutano.
 
Nakubaliana na wewe mkuu.

Alichokifanya jana Mbowe hakina tofauti na wale wapinzani wa awamu ya tano, upinzani kuunga mkono, nahisi ni APPROACH na SLOGAN ndio tofauti awamu ya sita tunaita MARIDHIANO na awamu ya tano KUUNGA MKONO JUHUDI.

Zamu ya Mwenyekiti
 
Kwa nini isiwe hivyo katika eneo la Urais pia??
Kwenye Eneo la Urais Hakuna mpinzani wa kushindana na Rais Samia maana amefanya makubwa yenye tija yaliyomgusa kila mwananchi bila kujari chama chake,ndio maana umeona katika mkutano wa chadema jina la Rais Samia likitawala kwa kusifiwa
 
Serikali kazi take ni kuwainua watu kiuchumi na siyo kuwadidimiza,serikali ya Rais Samia Ndio kazi kubwa inayoifanya kwa Sasa kuwainua watu kiuchumi kwa kuwawezesha na kuwawekea mazingira rafiki na wezeshi
Nakukumbusha tena! Propaganda zako zinafaa sana huko vijijini tena ukisisitiza amani, mshikamano na upendo. Humu watu wameshavuka kiwango cha kuhitaji malazi, chakula na mavazi! Usikimbie point, umesema SSH anawasemea wanyonge - nimeuliza hao wanyonge wametengenezwa na nani kama wapinzani unaowasema hapa hawakuwahi kuongoza??

Kazi kubwa ulionayo ni kuwaaminisha watu kuwa kila kitu kinachofanyika sasa ni bora kabisa ambacho wapinzani hawawezi kufanya. Unawezaje kufanya ulinganifu katika watu wawili ambao mmoja hakuwahi kufanya chochote?? Unailinganishaje CCM na wapinzani katika kutatua matatizo ya taifa hili wakati wapinzani hawakuwahi kuongoza nchi??
Ndio maana nasema propaganda zako zilengwe kwa watu sahihi - wasiojua!! Humu wengi wanajua!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…