Sasa ndugu yangu.
Kwanza Gaza ni gereza. Israel yote kaizungushia fence. Hakiingii chochote wala kutoka chochote isipokuwa kwa ruhusa ya Israel.
Eneo lenyewe ni dogo wala si kubwa! Limetolewa mifano mara nyingi humu. Ukubwa wake ni kama wilaya ya Kigamboni.
Hamas anaopambana nao wanatumia silaha duni za kienyeji za kujitengenezea wao.
Hamas haina ndege, haina jeshi la bahari, haina vifaru. Zaidi ya wanamgambo elfu ishirini kadhaa.
Israel imetumia 82% ya uwezo wake wa kijeshi ambapo mpaka sasa anapigana kwa takribani miezi 6 sasa.
Lakini hayo yoye yakitokea kuna mambo yafuatayo nayo yametokea:
Israel imeomba msaada wa kijeshi Marekani. Wanapatiwa silaha na zana za kivita mbali mbali na si mara moja wala mara mbili.
Wanapatiwa msaada wa gharama za kuendesha vita kwani vita yake na Hamas uchumi wake umeporomoka.
Tuwe wa kweli! Kwa kikundi hicho cha Hamas na eneo dogo kama hilo tena alilolizingira Israel ni wa kupambana nalo kwa miezi 6? Ambapo mpaka muda huu anahangaika nalo?
Kama hali ndiyo hii akipigana na nchi inayojiweza atakuwa katika hali gani? Yenye jeshi la anga, jeshi la maji, jeshi la ardhini n.k?
Tukubali, kwa sasa Israel haina uwezo wa kupigana na nchi yoyote ile.