Iran kutumia njia ya anga kupelekea silaha kwa magaidi ya Hezbollah, njia ya ardhini kupitia Syria imedhibitiwa na Israel baada ya kuangushwa Asad

Wejamaaa mbona unataka watu wanaokusoma ambao wanajua Iran imeinyuka Israel mala 2 .mwez April na October sasa uwongo wake upo wp mbona nyinyi mnapenda kuipamba Israel na sifa ambazo ana kias chakutaa ukweli ulio wazi mnalipwa kusema uwongo au ww ni mchungaji unadhani JF ni kijiwe chako cha kuwaongepewa watu. Kila siku mnadai Iran ilipigwa lkn ushaid akuna yemen tu juzi imepiga Telaviv na ushaidi upo chuma kinatua live mjini. Ww umeenda mbali ata kukana kupigwa Israel mala2 kichekesho zaid lkn pia mnadai Iran ilipigwa tuoneshen ushaid ufanane na jinsi tunaona Israel ikibutuliwa live. Una ushaid utatoa wapi wkt Iran mmeamua kuipiga ki propaganda mala utasikia hooo Iran aisubutu tena kuipiga Israel kwakua inajua ilichofanywa!!! Sasa Yemen juzi kapiga Telaviv kitu kizito na kila mtu anajua Yemen ni Iran ni sawa tu kusema kapigwa Israel na Iran kutokea Yemen. Au nasema uwongo ndugu zangu,
 
Mambo mengine yana historia ndefu ya uhasama nyuma yake.

Marekani ana ugomvi wa muda mrefu na Hezbollah it must be said ukisikiliza upande wao nao wana sababu ya kulipa kisasi.

Huu mzozo umeanza 1982/83 na hezbollah ndio mchokozi.

Tafuta declassified files za CIA, wazungu wanakiri hata wao walikosea kwenye intelligence wakaua zaidi ya watu 63 na kujeruhi watu 200 kwenye hasira za kulipa kisasi.

Sasa sisemi uhuni wa Israel ndani ya Palestine ni halali. Lakini hii mizozo ina historia, hezbollah ni shida ukianza kuwafuatilia toka mwanzo wao.
 
Unajua ukweli haufichiki
Rafiki kipigo hua hakijifichi,Sawa tuseme kweli Israeli alipigwa na Irani kwa mamia ya makombora makubwa makubwa (ICBM) Ni ishara ipi inaonesha kuwa Israeli imepigwa?

Ishara ya kwanza tungeona Kiburi na kujiamini kwa Israeli kinapungua na huenda hata Gaza angeondoka

Ishara ya Irani kupigwa ipo wazi,baada ya kipigo cha hv punde toka Israeli Iran iliiamuru Hesbolah kukubali masharti ya Israeli ambayo ni kuondoka mpakani na Israeli ili raia wa Israeli waishi kwa amani kaskazini mwa Israeli,kuacha kurusha maroketi kwa Israeli

Baada ya kipigo kutoka Israeli Irani aliahidi kujibu mapigo Kwa promise Ill,lakini wajuzi wa mambo walisema Irani kaumia sana hawezi kutekeleza promise lll kama alivyoahidi kwani akifanya hivyo atakuwa anajimaliza na kweli tunaona Ayatola mpaka Leo anatetemeka kuitimiza

Ishara nyingine kuwa Irani kapigwa ni kupoteza mamlaka yake nchini Syria,kutokana na kidhoofishwa na Israeli majeshi ya Irani yaliokuwa Syria yalipigwa na waasi na baadhi kuuwawa na kuacha silaha nyingi nyuma na Asad kipenzi Chao akafurushwa

Ishara zipo nyingi nimekea hizo chache Sasa nipe ishara za kupigwa Israeli ulizonazo mwenyewe bila kutegemea maneno matupu
 
Tusi liko wapi!?..'raia wote askari ndiyo maana makombora yakirushwa hukimbilia kwenye shelta'..hii ni kauli inayoakisi fikra jadidi?.. unahitaji kuwa askari Ili kukimbilia kwenye shelta!?
Unafahamu maana ya Shelta lkn,au nikurahisishie swali unafahamu matymizi ya handaki katika vita?
 
Irani yuko sahihi kuwekeza kwenye jeshi kuliko sehem yoyote ile maana anawindwa kutolewa pale. Huo ndio njia wameichagua wao bora wauze bei pungufu kuliko kumuachia bure Marekani kama wanavyofaidi mafuta nchi nyingine za kiarabu, mafuta ya Iran yamewashinda hawabebi hata lita 1 kudadadeki Ayatollah kashakataa wanaharamu kugusa rasilimali za Iran wao waseme waweke vikwazo watawazoea waarabu tu
 
Siyo kweli kuwa Iran imewekeza kwenye jeshi kwa kiasi kikubwa, Bajeti ya kijeshi ya Iran ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine kwenye eneo hilo.
 
Wameshapigwa juzi hapa rada zao nyang'anyan'ga na askari kibao wamekufa halafu unaleta hadithi za Alf lela ulela,waliahidi kulipiza Kwa promise lll lkn ahadi Yao imekuwa ya moto walipewa vitu vzito sana😥
Lete ushahidi wa kupigwa hapo juzi na askari kibao kuuawa.
 
Ni hiki watakipata kama walivyokipata kabla.
 
Iran Hawanunuai silaha Kama Saudi’s na Israeli . Labda ndege baathi tu . Nchi inauwezo wa kuzalisha silaha zake yenyewe . Mwakani inafikisha drone za shaheed 136 million 2 na makombora ya ballistic 700000 kwa ajili ya kujitosheleza , Israel ajiandae kupokea kipigo cha makombora 1200 hii itakuwa ni sawa na 0.17%
 
Basi hiyo ilikupita naona maana iliandikwa sana baada ya Myahudi kutuma ndege zake huko kwa Ayatola
Kama unazungumzia shambulio la ndege basi pole yako lilifeli.
Hakuna asiyejua humu kama lile shambulizi ni failure na walitumia anga la Iraq kushambulia hawakuingia anga la Iran.
Hata satellite images hazikutoa picha zenye ushahidi kamili.
Tofauti na promise 2 ambayo kila mtu aliona Israel ikiungua.
 
Siyo kweli kuwa Iran imewekeza kwenye jeshi kwa kiasi kikubwa, Bajeti ya kijeshi ya Iran ni ndogo ukilinganisha na nchi nyingine kwenye eneo hilo.
Ishu sio udogo wa bajeti ishu ni focus nliyoizugumzia hapa kafocus kwenye eneo hilo leo Hii Iran wanaproduce makombora kuliko taifa lolote lile, na wanaprogram ya nuklia ambayo karibuni itakamilika
 
Kinachowaumiza israeli ni aibu na kujimwambafai kwa israeli pale Middle East. West wakiangalie ile clips wanatahayari. Kwa upande wangu nana lile shambulio la pili lilibeba mchanganyiko wa aina ya makombora Kama nne hivi kwa hiyo mpaka sasa iran anafahamu ni aina gani ya makombura ayatumie na ayazalishe kwa wingi kwa ajili ya isreli, kwa hiyo octoba 1. Ili kuwa ni kulipa kisasi lakini pia iran ilijaribu silaha zake kwenye uwanja wa vita kuwa ni ipi aitumie kama apperhand kwa battle inayofuata. Kwa hit promise 3 itakuwa more efficient na hapo ndo soko la mifumo Yao ya ulinzi litakapo kufa rasmi
 
Unafahamu maana ya Shelta lkn,au nikurahisishie swali unafahamu matymizi ya handaki katika vita?
Shelters za israel ni kwa ajili ya raia kujilinda na mashambulizi,huhitaji kuwa askari kukimbilia kwenye shelter, period!
 
Kimbe upon nyuma ya wakati soma hii
Shelters za israel ni kwa ajili ya raia kujilinda na mashambulizi,huhitaji kuwa askari kukimbilia kwenye shelter, period!
Asilimia kubwa ya wayahudi wanamfunzo ya kijeshi likiwemo la kukimbilia kwenye handaki wakati wa hatari na hii inawatofautisha sana na waarabu na waafrika wengi
 
Kimbe upon nyuma ya wakati soma hii

Asilimia kubwa ya wayahudi wanamfunzo ya kijeshi likiwemo la kukimbilia kwenye handaki wakati wa hatari na hii inawatofautisha sana na waarabu na waafrika wengi
Kukimbilia kwenye handaki haihusiani na mafunzo ya kijeshi, sisi tuliokua kusini mwa tz miaka ya 80,tuliambiwa tuchimbe mahandaki kipindi hicho jwtz ipo msumbiji huko,nilijua habari za handaki nikiwa na miaka 4,5,7,8..
 
Kukimbilia kwenye handaki haihusiani na mafunzo ya kijeshi, sisi tuliokua kusini mwa tz miaka ya 80,tuliambiwa tuchimbe mahandaki kipindi hicho jwtz ipo msumbiji huko,nilijua habari za handaki nikiwa na miaka 4,5,7,8..
Basi kama ulikuwa hujui hiyo ni mbinu ya kijeshi mlipewa kama ulikuwa hujui,
Kukimbilia kwenye handaki haihusiani na mafunzo ya kijeshi, sisi tuliokua kusini mwa tz miaka ya 80,tuliambiwa tuchimbe mahandaki kipindi hicho jwtz ipo msumbiji huko,nilijua habari za handaki nikiwa na miaka 4,5,7,8..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…