Iran - Nchi inayohofiwa zaidi ulimwenguni na Marekani kuliko Taifa lolote lile duniani

Nimependa ufafanuzi wako ambao mtu yoyote mwenye akili timamu lazima akuelewe 👍
 
[URL

 
Iran zaidi ya teknolojia ya drone na makombora aliyowekeza kwa muda mrefu hakuna Cha zaidi alichonacho..kiburi chake chote ni anaringia makombora yake
Iran yupo vizuri kwenye biochemical engineering na pharmaceutical science.
Kipindi cha covid miongoni mwa mataifa yaliyofanikiwa kuwa na active covid-19 vaccine ni Iran.
Nenda kafuatilie mkuu. Hawa jamaa kielimu wamejipanga japo kwa kiasi kikubwa tuwasifu China maana ndio walioingia nao ushirikiano wa kusimamia taasisi zao za kielimu.
Ikatokea wameondolewa vikwazo watapaa sana kiuchumi.
 
Trump na mikwara yake yote lkn kwa Iran kanywea.
 
Kwa hiyo wana uwezo wa kuishamblia Marekani?.
 
Kwa hiyo wana uwezo wa kuishamblia Marekani?.
Uwezo huo wanao, na ndio maana Marekani imesitisha mikwara yake. Kumbuka Iran ni nchi yenye historia ndefu kivita.

Wakati Marekani imegunduliwa na waingereza miaka 400 iliyopita, miaka 200 tu toka Uhuru wake, na miaka 100 tu imepita toka iingie katika nchi zenye nguvu.

Iran yenyewe ina maelfu ya miaka kama nchi yenye kujitawala. Persia Empire (Iran ya leo) iliwahi kutawala eneo kubwa kabla hata kina Ibrahim, Farao, Musa, Yesu, Muhammad, wayahudi na nchi ya kiyahudi haijazaliwa. Hivyo uwezo wao wa mapambano hauna shaka toka miaka na miaka. Ndomaana pamoja na vikwazo lukuki vya uchumi na kijeshi, vilivyowekwa kwao Kwa zaidi ya miaka 50 havijawahi kuwaangusha wala kuwayumbisha kijeshi.

Hii ni tofauti na Israel ambayo haikuwahi kuwa na Empire yoyote katika Dunia hii. Haina vikwazo vya uchumi wala silaha. Inabebwa kila siku na nchi za Magharibi hasa Marekani. Kuanzia ulinzi wa nchi yao hadi uchumi wao unabebwa na Marekani. Bila Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya Israel ingekuwa nyepesi mno.

Tukija kwa swali lako, ni kweli Iran sio mchokozi na haijawahi kuichokoza nchi yoyote. Ila unapoichokoza, ni lazima itakujibu tu, tena kwa kiwango kile wanachotaka wao.
 
Kifiro alichopata Israel toka kwa Iran hatamani tena kuchezea kende za Hayatollah
 
kwa mujibu wa Ufunuo wa mtu wa Mungu aliyefunumiwa na Yesu mwenyewe kwa kuoneshwa yale yatakayotokea mbeleni .

IRANI INA SILAHA YA BOMU LA NYUKILIA (NUCLEAR)HATARI ZAIDI ambalo YESU hataruhusu litumike kabla hajawaondoa watakatifu wake waliopo duniani/unyakuo wa kanisa(watakatifu wa Yesu) RAPTURE waondolewe duniani .
Yesu alimuonyesha mpaka sehemu ya SIRI ambapo IRANI imeyaficha hayo mabomu ya nyukilia hatari zaidi duniani ambayo hakuna nchi yeyote duniani ,endapo siku ikiyatumia ya taleta madhara maakubwa sana sana sana kwa dunia .
 
Hivyo ni sahihi kusema kwamba IRANI ndiye mbabe wa dunia kww kumiliki silaha hatari yenye madhara makubwa zaidi zaidi kwa dunia nzima .
Habari njema ni kwamba YESU hataruhusu zitumike kabla hajawaondoa watu wake hapa duniani..
Kwa kifupi UNYAKUO UMEKARIBIA.

kiunabii unyakuo unatokea kabla
ya 2030.
 
Iran hana uwezo wa kutengeneza Kila kitu acha uongo.. Iran hana technologia yeyote, Kila kitu amecopy urusi Yani Kila kitu amecopy urusi, anachofanya yeye anapeleka vijana urusi wanasoma engineering alafu Ile mifumo ya urusi wanaileta nchini kwao wanabadilisha majina wanaweka majina yao. Alivopigana na isael kilichomsaidia ni hayo makombora yake isingekua hayo angemalizwa vibaya sana sababu siku zote zile za vita Israel alitawala anga yote Yan Iran alipigwa na adui Ambae alikua ndani ya ardhi yake tofauti na Israel alikua anashambuliwa na makombora kutoka nje ya nchi.

Alafu hao wazungu wote unaowataja kama hujui hiyo ni damu Moja kwa hivo suala la kwenda vitani wote Hilo kwao ni kawaida ndo utaratibu wao huo hata wakija kupigana na nchi ndoogo kama Tanzania wanakuja wote usifikiri eti atakuja mmoja
 
Alafu usiseme Israel anategemea misaada jua kwamba Iran imepitwa Sana kiuchumi na Israel Yan kaachwa mbali sana...hapo mashariki ya kati nchi zenye uchumi mkubwa ni saudia, uturuki na Israel.. pia Iran Bado hana ujanja kiivo angalia mauaji mangapi yametokea ndani ya nchi yake na amebaki anashangaa Hadi leo hajui hata yametokea vipi Yani Bado yupo mdomo wazi.. Sasa adui Ambae anakupigia akiwa ndani kwako ni wa kumuogopa zaidi kuliko yule anaerusha silaha kutoka nje...sababu yule wa ndanni hujui amejifichia wapi
 
Sa
Sasa hayo mambo ya persia ni zilipendwa Sasa unaleta zilipendwa kwenye huu ulimwengu wa kupigana kwa drones? pili Iran hana uwezo wa kupigana na Marekani ata nukta..achilia Iran mtoto Mdogo hata baba yake china hawezi mtu pekee anayeweza kupigana na marekani kwa Sasa ni urusi peke yake..Iran tu hapo kwake kapigwa kabaki Mdogo wazi kuipiga Marekani ataanzia wapi?
 
Bro muda mwingine nyamazeni kama hamjui.
Iran teknolojia aliyokopi kwa Mrusi ni NUCLEAR SCIENCE PEKE YAKE.
-Teknolojia ya drone ni yake.
-Teknolojia ya makombora ni yake na mwaka juzi North Korea wakamuita ili awasaidie kwenye uundwaji wa Hypersonic missiles.
-Teknolojia ya madawa ni ya kwao.Usisahau kama baadhi ya vifaa vya upasuaji unavyotumia mgunduzi ni MUAJEMI.
-Teknolojia ya reli ni reverse engineering kutoka China.
-Teknolojia ya magari ni reverse engineering kutoka China.
-Air defense system kama Bavaar na Khordak waliunda wenyewe pasi na msaada wa nje kutoka Urusi na China.

Kilichomsaidia kwenye 12 days war ni mifumo yake ya ulinzi sio nguvu ya makombora tu. Kama angekua ana mifumo ya ulinzi dhaifu basi Iran ingegeuzwa Gaza taratibu.
 
Serikali ya Iran wapo vizuri
 
China usiitaje maana USA HANA UWEZO HATA KIDOGO kupigana na China.
Vita ya mgawanyo wa Korea ilionesha nguvu ya China kwa USA. Embu kaisome battle of Jangsari uone wachina walivyowachoma moto Korea kusini na Marekani.
-Iran uwezo wa kupigana na USA anao tena saanaa sio kidogo. Reference na nazitaja hapa.
1.Iraq-Iran war;USA alipigana nyuma ya mgongo wa Saddam Hussein na alitoa silaha hadi jeshi ili kuupindua utawala wa Khomeini. Iran ilipigana ikiwa imepewa msaada wa silaha pekee kutoka nchi chache sana na ikahimili vita ya miaka nane. Kama USA angekua na uwezo angeshaiangusha serikali ya Iran wakati ule 1980.
2.Vita za utawala wa Yemeni 2014. USA ili deploy silaha hata askari ili kumbakisha kibaraka wao Mansour. 2016 Iran alipoisaidia Houthi kijeshi muelekeo ukabadilika wa kivita.
3.2006 Israel-Lebanese war. Aliyefanikisha urejeshwaji wa Bint Jubeir ni Iran kwa kujipenyeza ndani ya Hizbollah.

Reference zipo nyingi sana hizo zinakutosha. Na Iran ameshafanya jaribio la intercontinental missile la masafa ya 20000kms. Ina maana Iran akiamua kurusha kombora Marekani anaweza.
Kama Iran ingekua nyepesi Trump asingekua anarusha tarehe za uvamizi tangu December 2025 hadi tunaingia February 2026.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…