Ndo tatizo la jukwaa hili kuruhusu kila mtu kujiunga, matokeo yake watu wasiokuwa na elimu kama wewe mnakuja humu kuandika ujinga bila kuweka facts na ushahidi wa kile ulichoandika. Vitabu vya dini na historia vinaonesha kuwa Iran au Persia iliwahi kuwa na Empire zaidi ya miaka elfu 3 iliyopita, waliweza kuwa na nguvu na kutawala eneo kubwa ikiwemo Mashariki ya kati yote, kabla ya Israel, Uyahudi, Farao, Musa, Ibrahim, Yakobo, Yesu na Muhammad kuzaliwa. Alaf wewe leo unakuja kuandika matapishi yako hapa kuhusu Urusi. Wakati wenzako walianza kujitambua na kupigana vita miaka hiyo elfu 3 iliyopita kabla hata haijajulikana kama kuna nchi itakuja kuitwa Urusi, Israel, Saudi Arabia, Marekani nk. Hivyo kila wanachotengeneza na kukifanya hakikuanza leo, ni cha miaka mingi mno iliyopita.
Tukija kwenye vita ya siku 12, hapo ndo unaonesha ulivyo mweupe kichwani. Hivi kiuhalisia Israel anaweza kutawala anga akiwa ndani ya Iran halaf aruhusu jeshi la Iran lirushe makombora katika ardhi yake hadi kupelekea Netanyahu kuomba vita isimame baada ya Tel Aviv kugeuzwa Gaza namba 2?
Look bro wewe unaandika habari zako kishabiki tu bila kuwa na facts yoyote kutoka katika historia au uhalisia.
Unaposema nchi za kizungu huingia kwenye kila vita ya mwenzao hata akipigana na nchi ni uongo. Tumeona juzi Marekani akiienda kufanya mashambulizi Venezuela bila kuwa na backup yoyote kutoka kwenye hizo nchi za kizungu. Ukweli ni kwamba hizi nchi huingilia kati pale tu wanapoona mwenzao anabondwa na kuzidiwa nguvu na Yule anaepambana nae.
Kingine kama Iran haina nguvu ni kwanini inawanyima usingizi Israel, Marekani na nchi zingine za Magharibi?
Israel ni nchi dhaifu sana, na ndiomaana haiwezi kuingia kwenye vita hata na wanamgambo bila kuwa na backup ya nchi za Magharibi zenye nguvu kijeshi. Vita ya siku 12 tu tayar mamia ya waisrael walikuwa wameshakimbia nchi yao, Netanyahu alilia na kushindwa kupata usingizi (picha inajieleza wazi). Je mziki ungeendelea kwa miezi mi3 kuna nyumba au jengo lolote lingekuwa salama kweli Israel?
Na usisahau Iran ipo kwenye vikwazo vya kiuchumi na kijeshi kwa zaidi ya miaka 50, lkn imeihenyesha nchi isiyokuwa na vikwazo hata kimoja tena inayotegemea msaada wa kiulinzi na kiuchumi kutoka Marekani, UK, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Uholanzi nk.
View attachment 3536965