Kama njia ya kulipiza kisasi kwa kitendo cha Iran kuzuia meli za baadhi ya mataifa kupita kwenye mkondo wa bahari wa Hormuz, tangu jana majira ya saa 4 asubuhi, Jeshi la Marekani limeweka zuio la meli yoyote kuingia au kutoka kwenye bandari zote za Iran. Na Marekani imeweka wazi kuwa kwenye zuio hilo, meli yoyote ya kivita ya Iran itakayozisogelea meli za kivita za Marekani zinazohakikisha hakuna meli inayoingia au kutoka bandari za Iran, itazamishwa.
Mpaka sasa Iran imeamua kutulia bila ya kupambana na Marekani kivita, badala yale waziri wa mambo ya nje wa Iran amepeleka malalamiko kwenye Baraza la Umoja wa mataifa akilalamika kuwa kitendo hicho cha Marekani ni kutoheshimu sovereignity ya Iran. Marekani nayo imesema kuwa inafanya hivyo ili kukomesha Economic Terrorism ya Iran.
Sijui kwa nini Iran inakazania kuendelea na mradi wa nuklia. Kwa nini isikubali kuachana nao, ila na yenyewe itake majirani zake wote wa Mashariki ya kati wasitengeneze wala kumiliki silaha za nuklia? Iran ipo disadvantaged kutokana na ile kauli yake na msimamo wake mpaka leo, kuwa eti Taifa la Wayahudi halitakiwi kuwepo Duniani, linatakiwa kuangamizwa, eti ni agizo la Allah.
Kutokana na msimamo huu, chochote inachokifanya Iran ili kuwa na silaha za maangamizi inatafsiriwa inataka kuiangamiza Israel. Iran ilitakiwa kuufuta msimamo huo wa kigaidi, kisha kutangaza kulitambua taifa la Israel kama taifa jirani, kama ilivyokuwa kabla ya utawala wa Ayatollah, kisha kuanzisha uhusiano mpya na majirani zake. Bila hivyo, Iran itakuwa nchi ya vita na shida kubwa kiuchumi miaka yote.