Sasa mbona unateseka? Mimi nimesema kilichotokea wewe unakuja na lugha chafu, kwa maneno haya unaonekana una stress.
Na usiwapangie watu cha kufanya, mbona wakiwapa magaidi mabomu washambulie hamsemi, yani ni ajabu kuona kuna raia wabongo wanaamini Iran inaiogopa Israel.
Iran huyuhuyu aliyeteka meli ya Uingereza mchana kweupe, mbele ya kamera huku akitoa taarifa kwenye vyombo vyote vya habari ndiye aiogope Israel? Kwamba Israel inaishinda UK kijeshi?
Basi tufanye UK ni mtoto kwa Israel, vipi kuhusu kuteka meli ya jeshi la Marekani. Vipi kushambulia kambi yake ya Iraq. Mnaichukulia Iran kama Mbao FC, mna matatizo sana nyinyi hao mnaowaona wababe kila siku wanaishitaki na kuisakama mbele ya mataifa. Wewe ulishawahi kuona WCB wanamdiss Harmorapa? Ni kwa sababu Harmorapa ni negligible, lakini si unawaona wanamdiss Ali Kiba. Ni kwakuwa Ali Kiba anatoa upinzani.
Nasisitiza, Iran akisema atalipiza kisasi ni sawa na kusema jua litazama. Its inevitable hata ulete sarakasi za aina gani. Na hawajibu siku hiyohiyo, wanakuacha utumie gharama nyingi za kujihadhari kisha wanashtukiza.