Mimi ninaona wote wanaogopana. Iran Karusha drones na Ballistic missiles ambazo anajua zitatumai almost za tisa kufika Israel ambayo iko 700 miles away from Iran ikiwa ina maana alijua watajiandaa kuzidungua. Angekuwa ana lengo la kusababisha hasara kwa Israel angempiga shambulizi la ghafla. Sasa wewe unarusha kitu kinifikie masaa tisa, Israel na wapambe wake wakasema wanatrack kila drone na kila missile kabla ya kuingia kwenye anga ya Israel.
Upande wa pili ngoja tuone ila sidhani kama Israel naye atajibu kwa kurusha makombora au ndege kwenye anga ya Iran labda kama atapiga proxy wa Iran.
Ila la msingi naombea hawa watuw asiingie vitani maana dunia naona inaanza kuchanganyikiwa. Nikisoma comments za raia wa Marekani, wanaomba serikali yao iache Israel apambane na matatizo yake maana wanadai serikali iko busy na Israel wakati mambo yao ndani yanaharibika uchumi unayumba china anasonga kwa sababu ya kujifanya wanatia mkono kwenye mambo yasiyo wahusu.