Sisi zana zetu zitatumia siku ngapi kufika huko?

Kumbuka kwenye vituo vya mafuta harufu ya kukosekana mafuta imesha anza kunukia.
Usijali mama anaupiga mwingi, DP world itatuvusha.

Mafuta ya kupigia misele sio muhimu kabisa, tungekuwa na viwanda vinatumia mafuta ningekuelewa.
 
Acha kuhalalisha upumbavu jengo la ubalozi halitakiwi kushambuliwa kwa namna yeyote ile.

Hata kama kuna mtu hatari kwa usalama wa nchi anatafutwa akikimbilia kwenye ubalozi wa nchi fulani huruhusiwi kumkamata mpaka uwasiliane na taifa husika lenye huo ubalozi, sembuse ubalozi ambao upo nje ya nchi yako?
Kwa akili yako unadhani Iran haiwezi kushambulia balozi za Israel zilizoko kwenye mataifa mbalimbali ?
 
Kazi kuu ya airbase ni kwaajili ya shughuli za ndege vita.
Ni zipi infrastructure za airbase!?
Je, kupaa na kutua kwa ndege vita kwenye airbase sio "shughuli za ndege vita"?

Miundombinu za airbase zipo nyingi. Inategemea na mahitaji ya jeshi husika. Muhimu zaidi ni runways pamoja na kituo cha mawasiliano na uongozaji.

Picha za satellite zimeshaanza kutoka. Hiyo airbase ya Israel haijapata madhara yoyote ya kuifanya isiwe operational.
 
Israel kasema far less minor damage occurred unajua maana yake, acha unyoko

Ni shughuli moja wapo ila hazijakamilika.

-Kituo cha mawasiliano.
-Ghala la silaha.
-Parking ya ndege na drones.
N.k n.k je imethibitika kuwa hivi vyote vizima!??
 
Irani ina silaha za nyuklia, hii ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa israeli
 
Diplomasia ni hadhi na sio jengo. Jengo la ubalozi linaweza kupoteza hadhi ya kidiplomasia endapo litatumika kijeshi wakati wa migogoro ya kijeshi ama vita. Hiyo ni kulingana na sheria ya kimataifa.

Nenda katafute majina pamoja na nyadhifa za wale wanajeshi waliouawa pale Damascus katika eneo la ubalozi. Fuatilia misheni zao pale Syria kabla ya lile shambulio. Vyanzo vya ndani ya IRGC vimenukuliwa vikidai kuwa hicho kikao pale ubalozini kilikuwa kikihusu vita ya Gaza na kilihudhuriwa pia na wanamgambo wa PIJ na Hezbollah.
 
Hilo ndio kosa kubwa alilo lifanya Israel, kushambulia Ubalozi wa Iran nchini Damascus ni sawa na kuishambulia nchi hiyo.
hivyo israel ndio iliyo anzisha vita na Iran hivyo kwa mujibu wa sheria za Kimataifa Iran ina haki ya kujibu mashambulizi.
 
Hii vita itakuwa kubwa sana.

Naamini nchi zote za kiarabu zitaungana dhidi ya Israeli.
Mazungumzo yanapaswa kufanywa kuliko kuchochea mzozo.
 
Ni shughuli moja wapo ila hazijakamilika.

-Kituo cha mawasiliano.
-Ghala la silaha.
-Parking ya ndege na drones.
N.k n.k je imethibitika kuwa hivi vyote vizima!??
Hivyo vyote ulivyovitaja havijadhurika. Madhara ni kidogo sana eneo la wazi kwenye moja ya runways.

Kiufupi, hakuna madhara yoyote ya maana ukilinganisha na jinsi ambavyo Iran ilipania kuishambulia hii airbase.
 
Hilo ndio kosa kubwa alilo lifanya Israel, kushambulia Ubalozi wa Iran nchini Damascus ni sawa na kuishambulia nchi hiyo.
hivyo israel ndio iliyo anzisha vita na Iran hivyo kwa mujibu wa sheria za Kimataifa Iran ina haki ya kujibu mashambulizi.
Iran inapoitumia Hezbollah na makundi mengine kuishambulia Israel, huko sio kuanzisha vita na Israel?
 
ninachoshangaa, mashambulizi ya makombora karibia 300 lakini Israel haijaumia wala nini. biden amesema netanyahu asijibu, ila bibi kasema ndani ya masaa 48 anajibu. iran anasema yeye ameshapiga na hapigi tena, hahaha, ati anaogopa anajitetea kuwa ameshamaliza kazi hivyo hatarusha tena ila israel wakimpiga atatumia vichwa vya nukes. cha ajabu, israel ina makombora ya nukes kati ya 100 hadi 200, iran hana hata moja ila nukes aliyeenrich wanasema anaweza kutengeneza mabom 3 tu ya nukes. mtu anayetarajiwa kutengeneza bomb anamtishia mtu ambaye tayari anayo. tuombe tu Mungu vita iishe, though haipendezi kuisha wakati iran ambaye ni threat kwa kila mtu, amesimama. anatakiwa kudondoshwa ili dunia ikae salama.
 
Iran inapoitumia Hezbollah na makundi mengine kuishambulia Israel, huko sio kuanzisha vita na Israel?
hilo halina ushahidi wa moja kwa moja....ila
Israeli kuushambulia ubalozi wa Irani ni jambo liko wazi kwa dunia kujua kuwa Israeli imeishambulia Irani.
hivyo sheria za kimataifa zinairuhusu Irani kujibu mashambulizi.
 
Hivyo vyote ulivyovitaja havijadhurika. Madhara ni kidogo sana eneo la wazi kwenye moja ya runways.

Kiufupi, hakuna madhara yoyote ya maana ukilinganisha na jinsi ambavyo Iran ilipania kuishambulia hii airbase.
Uthibitisho uko wapi?
 
Drone gani zinatembea masaa kumi!?
Mbona muongo wewe jamaa!?
Drone zilitumia masaa mawili naa na silaha zilizotumika kuanzia Drone mpaka makombora yalikua ya medium range na ujazo wa kawaida.
Je angetumia long range yenye ujazo mkubwa sijui ingekuaje hapo Tel Aviv.
 
Uwezo wako wa kutambua mambo ndo umeishia hapa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…