Hiki cha kutamka laana hovyo hovyo kwenye dini yenu ndio kinachofanya niichukie kupita maelezo.
.
Mwenye uwezo wa kulaani duniani yuko mmoja tu naye ni aliyekuzaa wewe na mimi na wengineo yani (mama) na si vinginevyo nyie hata muwe organized wote muilaani katu nakwambia mtakuwa itakuwa ni wastage of time.
.
Magroup mbalimbali ya maislamu hili neno laana limewatawala sana ninyi hamfundishwi huko madrasa laana ni nini?
.
Answer (1 of 63): Disclaimer Don't judge my political stands and national preferences. I am neither an employee in any government office nor a practitioner in any academic institution. What I have said is just what I have said, don’t take it seriously. Fact-checking 1: South Xinjiang isn’t shor...
Fungua hiyo link ujifunze
Wewe Khaligraph ni mchanga mno katika masuala ya dini kwa ujumla, nakushauri kaa kitako na ujifunze elimu ya dini kwa ujumla, kwa muda mfupi nimejadiliana nawe masuala ya dini nimegundua hivyo.
1---- unasema kitendo cha kulaani kwenye dini yetu (uislamu) kinakufanya uichukie kupita maelezo.
Jibu:- Unatakiwa utofautishe kati ya dini na wafuasi wa dini, mimi ndiye mfuasi wa dini na ndiye niliye laani sasa iweje Uislamu ulaumiwe kwa "kosa" lisikokuwa lake??-- kama ni kosa ungalipasa unilaumu mimi mwenyewe na sio Uislamu.
Yesu anatufundisha kulaani, ukisoma Biblia utaona Yesu ndiye Mwalimu wa kutoa laana na akawafundisha wanafunzi wake kufanya hivyo, mbaya zaidi yeye aliulaani mti bila kosa kwani mti haukuwa na matunda sababu haukuwa ni msimu wake, sasa usinilaumu mimi kuomba laana kwa wahalifu mlaumu kwanza yesu kuulaani mti bila ya hatia na mti ukakauka kesho yake. Marko 11:12-14, Marko 11:20-25, Mathayo 21:18-22.
2---- Unasema anayetakiwa kuomba laana ni yule aliyetuzaa, yaani mama.
Jibu:- Ukisoma Wagalatia 3:13, Inasema Yesu alifanywa kuwa laana, sasa uniambie; je Bikira Maria ndiye alimtolea laana Yesu???
3--- Unasema, magrupu mbalimbali ya waislamu neno laana limetawala sana, unauliza tena; je, nyinyi (sisi waislamu) hatufundishwi huko madrasa laana nini??.
Jibu:- Ilikupasa wewe ndiye utuambie laana nini na madhara yake ni yapi kwa muombaji laana, cha ajabu umeleta porojo tu na kelele bila kunukuu hata maandiko ya Kamusi kuelezea laana ni kitu gani, sasa mimi nipo "different", hapa nimenukuu maana ya neno laana (CURSE) kutoka katika kamusi ya Merriam Webster;
Curse definition:-- is a prayer or invocation for harm or injury to come upon one.
Sasa mkuu Khaligraph umeona kwamba mtu unapoomba laana ni sawa na kuomba dua kwa Mungu dhidi ya Muhalifu basi ni juu ya Mungu kukubali au kuikataa, sisi tunapeleka kilio chetu kwa Mungu naye anapoona kilio chetu ni cha haki basi atapokea dua yetu lakini anapoona hakuna haki basi haeezi kupokea. Neno invocation lililopo katika hiyo definition limetokana na neno invoke likiwa na maana; call on deity or spirit in prayer as witness.
Kwa hiyo kuomba laana ni maombi yanayopelekwa kwa Mungu atoe hukumu kwani hatuna uwezo mwingine "at our disposal" .