Upo mbali sana na ukweli. Afadhali ungetaja Taifa jingine lakini siyo China. China bado sana kufika ilipofika US. China kikubwa kilichoongezeka kwa haraka ni GDP baada ya kuachana na uchumi wa kijamaa na kuukumbatia uchumi wa kiriberali uliowezesha makampuni mengi makubwa ya Ulaya na America kuwekeza China.
Baada ya hilo kufanyika, kulikofanyila uchumi wa China kukua haraka, hali hii ilikuwa ya kipindi fulani tu. Kwa hiyo uchumi wa China hautaweza kukua kama ulivyokuwa unakua. Kipindi cha ubinafsishaji uchumi wa China ulikuwa unakua kwa 9.7% lakini sasa hivi ni 3 - 4% tu na hautarajiwi kuvuka hapo.
China bado ni maskini. Wapo kwenye ukomo wa chini wa kipato cha kati, na wapo chini sana ya wastani wa mapato ya nchi za kipato cha kati.
Per capita income ya China ni chini ya $10,000 wakati ya U S ni zaidi ya $60,000. Kwenye human development China ni ya 89. Maana yake ni kuwa China imezidiwa na mataifa 88. Hii ndiyo sababu ya Waziri Mkuu wa China kutamka kuwa China bado ni nchi maskini.