Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,890
- 26,440
Ijumaa ilopita Iran wamezungumza na shirikisho la kandanda Duniani FIFA kuomba kuhamisha timu yake ta taifa ya kandanda na maofisa wote wanoandamana na timu hiyo nchini Mexico, baada ya kukikiri kuwa wachezaji karibu wote wamepitia mafunzo maalum kutoka jeshi maalum la mapinduzi la Iran maarufu kama IRGC.
Raisi wa shirikisho la soka la Iran bwana Mehdi Taj amesema Fifa wamekubali ombi la Iran kuhamisha timu yake na kuipeleka katika mji wa mpakani wa Tijuana nchini Mexico kutoka kwenye kambi yake mjini Tucson katika jimbo la Arizona nchini Marekani.
Tucson ni jiji kubwa lililopo kusini mwa jimbo la Arizona maarufu kama Arizona Sun Corridor na la pili kwa ukubwa baada ya jiji kuu la Phoenix.
Iran walipangiwa kambi yake katika mji huo wa Tucson lakini kutokana na vita yake inoendelea kati yake na Marekani kumekuwepo na sintofahamu khasa katika mstakabali mzima wa Usalama na ushiriki wa timu yake hiyo. Chini ya kanuni na miongozo ya FIFA kambi ya za timu zinoshiriki michuano ya kombe la Dunia ni lazima ziidhinishwe na shirikisho hilo.
Bwana Taj amesema kufuatia mazungumzo na katibu mkuu wa FIFA bwana Mattias Grafstrom maombi ya Iran kuhamisha kambi yamekubaliwa na kwa sasa yangoja kuidhinishwa rasmi. Tijuana ni mji uliopo karibu na mpaka wa Mexico na Marekani kusini mwa jimbo la California na wapakana na bahari ya Pasific. Pia Iran itaweza kusafiri kwa ndege (kama dakika 55) kuliko kusafiri umbali mkubwa kutokea Tucson.
Maandalizi ya timu ya taifa ya Iran bado yaendelea katika kambi yake mjini Antalya nchini Uturuki na mechi yake ya kwanza itakumbana na New Zealand kwenye uwanja wa Sofi kwenye kitongoji cha Inglewood na baadae kucheza na Ubelgiji katika mji wa Los Angeles kabla ya kumaliza mechi ya makundi dhidi ya Misri katika mji wa Seattle tarehe 26 Juni.
Hapo awali shirikisho la soka la Iran liliwasilisha FIFA orodha ya masharti 10 yanopaswa kufuatwa inapoteuliwa timu ya taifa na sharti mojawapo ni wachezaji , makocha na maofisa wanoandamana na timu ya taifa kuwa ni lazima wawe wamepitia mafunzo ya kijeshi kutoka IRGC.
Hapo awali waziri wa nchi aneshughulikia masuala ya nje wa Marekani bwana Marco Rubio alitoa angalizo kwamba wachezaji wa Iran wakaribishwa nchini marekani lakini watu wenye mahusiano a IRGC walikuwa wakikabiliwa na kukosa viza ya kuingia Marekani.
Kinosubiriwa kwa sasa ni hatma ya maombii ya viza kwa wachezaji, maofisa na makocha wa timu hiyo kuingia nchini Marekani kupitia ubalozi wa Marekani mjini Ankara nchini Uturuki.
Michuano ya fainali za kombe la Dunia yaanza rasmi tarehe 11 mwezi ujao na itakamilika tarehe 19 ambapo mtanange wa fainali utakuwa katika uwanja wa MetLife kwenye jimbo la New Jersey. Makao makuu ya jimbo hili yapo mji wa Trenton na mji maarufu katika jimbo hili waitwa Newark. Kaskazini mashariki ya jimbo hili kuna jimbo la New York.
Hivyo habari ndo hiyo wachezaji wa Iran ni vijana wakamavu kutoka IRGC jambo ambalo limemarisha milio ya tahadhari kwa jumuiya mbalimbali za Kijasusi katika nchi za Marekani na Canada ambayo mwezi April walimkatalia viza ya kuingia nchini humo bwana Raj sababu ikiwa ana mahusiano na IRGC.
Chanzo: Associate Press