Iran yarusha Makombora takriban 200 kuelekea Israel, Rais Biden aagiza Jeshi la Marekani kuyazuia

Iran - Mtoto kautana nasubiri response ya myahudi
Naona vinu vya nyuklia na oil refinery za iran zitakuwa na wageni wazito sana
Kwani mara ya kwanza alifanya nini si alirushiwa makombora na majibu yake ikawa vile vidroni vya kushoot video,, labda aingie baba yake USA sio yahudi
 
Angalia hii clip, hio ni Air base ya Israel inakuwa decimated, wanapohifadhi ndege zao, ni eneo ambalo bila shaka linalindwa vibaya mno, hili eneo sio muhimu?

View: https://x.com/MyLordBebo/status/1841210221659615450

Hakuna cha makombora 10 wala nini vitu vinatua tu.

In short sijaona video hata moja ambayo inaonesha hizi Missile zikiwa Intercepted hata kwa 50% ni zinatua tu, na Iran wamepiga maeneo ya kijeshi kwa Asilimia kubwa.

Mbona naona miti, kwani Israel wanahifadhi ndege kwenye bustani za miti.
Airbases kwenye runways na karibu na hardened shelters hakunaga miti kabisa maana huleta hatari kwa ajari ndogo ndogo za ndege.

Kama hujaona interception makombora almost 200 yamefanya nini. Gaidi wawili wameua watu nane, makombora over 180 yameharibu nini kikubwa au kuua wanajeshi wangapi. Subiri Israel ikijibu hata kwa mabomu 10 tu uone matokeo.
 
Angalia clip ya pili sio ya kwanza,

Pia tunaongelea defensive system ya kuzuia Balistic, huwa sipendi kudiscuss na watu wanadandia hiki na kile hawatulii kwenye topic. Israel akipiga makombora 10 Iran ina maana ana battery za kuzuia Balistic?
 
Kwa ujumla Iran imeonesha professionalism kwenye medan ya vita kwani haijaua raia kama Sheria za zinavyotaka.

Pili amelenga military sites TU na inaonekana zimepigwa vilivyo. Suala La wanajeshi wangapi wamekufa au kujeruhiwa sahau Huwa ni siri.

Kuna mambo yatakuwa wazi mfano ndege zilizoharibiwa, vifaru magari vita, viwanja vya ndege n.k.

Ukiona mtu analipiza kwa kujua raia hajui vita zaidi kuitumia mihemko. Wakihisi kwa kufanya hivyo raia watawageuka viongozi wao na hata kuwapindua.

Hivyo kama ni kuchapana basi Rais wasiuwawe ndio tuone mbabe.

Tumeshuhudia Ukraine Russia akipiga maeneo ya jeshi TU tofauti na Ukraine wanapiga maeneo ya raia na huo ni ugaidi.
 
Israel ina eneo dogo sana haiwezi zuia saturation attack. Na pia inapenda kujibu kwa kutoa onyo kali.

Ila nadhania Israel itajibu kwa miundombinu muhimu Iran kama ya mafuta kwanza kama angalizo kuwa inaweza shambulia nuclear sites. Na hata Iran ikijibu tena sitarajii itarnda direct kushambulia Dimona nuclear site ya Israel badala yake ishambulie kama gas facilities kuonyesha inaweza piga Dimona ikiamua.

Israel ikipiga vinu vya Iran moja kwa moja Iran itashindwa kujizuia, Israel ingeshambuliwa kinu cha nyuklia Iran ingekuwa inachakaa vibaya kwa sasa. Wote wakienda kwa uangalifu itakuwa showdown. Yawezekana Iran kupitia Russia ikaitaarifu Israel izuge yaishe, kama ilivyo fanya al Assad airbase kule Iraq to save face baada ya Soleimani kuuwawa na Marekani.
Israel haina uwezo kupiga vinu vya nuclear vya Iran...

Iran imejifunza kwa vinu vya nuclear vilivyoshambuliwa na Israel nchini Iraq na Syria...

Operation opera Israel ilipiga vinu vya nuclear Iraq mwaka 1981, Israel ikashambulia kinu cha nuclear Syria katika operation waliita outside the box mwaka 2007... Hivyo vinu vya nuclear vyote vilijengwa kama majengo ya kawaida ambapo hata CIA waliweza kufuatilia kila kitu kinachoendelea, walijitahidi kuficha vinu hivyo jangwani lakini haikusaidia... Kwa satellite kila kitu kilikuwa wazi...

Kwa kutumia ndege vita Israel wakashambulia...

Iran haikutaka kufanya makosa, vinu vyao vipo deep underground, sio deep underground tu , vimewekwa chini kabisa ya milima.. Halafu vipo locations tofauti tofauti..

Kwa jiografia Iran ni nchi yenye milima mikubwa na ipo mingi, wameweka vinu vyao chini ya milima na kuweka concrete juu ngumu sana...

Mbali na hapo vinu vyao vinalindwa na air defenses na AAA(anti aircraft artillery) , kwa kutumia bomber kama F16 lazima ndege iruke usawa wa target na kuachia bunker buster... Kitu ambacho air defenses zitashambulia ndege..

Hata bunker buster ya tons 16 ambayo US wanayo haiwezi haribu hivyo vinu...

Israel bomber anazotumia ni F15 na F16 labda kwa sasa na F35..

Kingine F15 na F16 hazina uwezo ku handle uzito wa bunker buster kwenda kupiga Iran kwa huo umbali, fuel haiwezi kutosha kuifikisha ndege kama F15 au F16 kupiga nuclear facility Iran... Bunker buster ni nzito mno kumbuka...

Operation opera na outside the box pale Syria ndege vita zilibeba tanks za ziada na baada ya mashambulizi walitupa tanks hizo kupunguza mzigo ili ku manage fuel consumption, walitumia pia mbinu ya kuruka kwenye high altitude wakati wa kurudi baada ya shambulizi...

Ndege vita kama F15 au F16 zinaporuka altitude ndogo huwa zinakula mafuta zaidi kuipa ndege thrust kwenda mbele tofauti na ikiwa anga za juu zaidi... Lakini wanapita chini kukwepa radars...

Hapo umeona kuna ugumu kiasi gani kushambulia vinu vya nuclear Iran...

Ndio maana Israel imekuwa ikitumia njia kama kuua wanasayansi wa atomic wa Iran ili kuzuia zoezi hilo ambapo imeshindikana pia...

Vinu vya nuclear Iran vingekuwa vimejengwa kama uwanja wa Mkapa, tayari Israel ingeshalipua muda mrefu sana..
 
Attachments

  • FB_IMG_1727710655586.jpg
    FB_IMG_1727710655586.jpg
    21.7 KB · Views: 1
  • FB_IMG_1727704540043.jpg
    FB_IMG_1727704540043.jpg
    58 KB · Views: 1
“Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.

— Kutoka 14:14 (Biblia Takatifu)
Bwana wako atampigania nani wewe mbona unakuwa fala, huyo Bwana wako hao waisrael wenyewe hawamkubali,, kama ni udini basi hii mbungi ni ya myahudi na muislam wee mkristo kaa pembeni, huyo yahudi unaemshobokea ye hakutaki
 
Israel haina uwezo kupiga vinu vya nuclear vya Iran...

Iran imejifunza kwa vinu vya nuclear vilivyoshambuliwa na Israel nchini Iraq na Syria...

Operation opera Israel ilipiga vinu vya nuclear Iraq mwaka 1981, Israel ikashambulia kinu cha nuclear Syria katika operation waliita outside the box mwaka 2007... Hivyo vinu vya nuclear vyote vilijengwa kama majengo ya kawaida ambapo hata CIA waliweza kufuatilia kila kitu kinachoendelea, walijitahidi kuficha vinu hivyo jangwani lakini haikusaidia... Kwa satellite kila kitu kilikuwa wazi...

Kwa kutumia ndege vita Israel wakashambulia...

Iran haikutaka kufanya makosa, vinu vyao vipo deep underground, sio deep underground tu , vimewekwa chini kabisa ya milima.. Halafu vipo locations tofauti tofauti..

Kwa jiografia Iran ni nchi yenye milima mikubwa na ipo mingi, wameweka vinu vyao chini ya milima na kuweka concrete juu ngumu sana...

Mbali na hapo vinu vyao vinalindwa na air defenses na AAA(anti aircraft artillery) , kwa kutumia bomber kama F16 lazima ndege iruke usawa wa target na kuachia bunker buster... Kitu ambacho air defenses zitashambulia ndege..

Hata bunker buster ya tons 16 ambayo US wanayo haiwezi haribu hivyo vinu...

Israel bomber anazotumia ni F15 na F16 labda kwa sasa na F35..

Kingine F15 na F16 hazina uwezo ku handle uzito wa bunker buster kwenda kupiga Iran kwa huo umbali, fuel haiwezi kutosha kuifikisha ndege kama F15 au F16 kupiga nuclear facility Iran... Bunker buster ni nzito mno kumbuka...

Operation opera na outside the box pale Syria ndege vita zilibeba tanks za ziada na baada ya mashambulizi walitupa tanks hizo kupunguza mzigo ili ku manage fuel consumption, walitumia pia mbinu ya kuruka kwenye high altitude wakati wa kurudi baada ya shambulizi...

Ndege vita kama F15 au F16 zinaporuka altitude ndogo huwa zinakula mafuta zaidi kuipa ndege thrust kwenda mbele tofauti na ikiwa anga za juu zaidi... Lakini wanapita chini kukwepa radars...

Hapo umeona kuna ugumu kiasi gani kushambulia vinu vya nuclear Iran...

Ndio maana Israel imekuwa ikitumia njia kama kuua wanasayansi wa atomic wa Iran ili kuzuia zoezi hilo ambapo imeshindikana pia...

Vinu vya nuclear Iran vingekuwa vimejengwa kama uwanja wa Mkapa, tayari Israel ingeshalipua muda mrefu sana..
Halafu hii delayed response ya Iran si ajabu ilikuwa ni kwa ajili ya kujiandaa kwa retaliation ya Israel.

Yule Haniya si kauliwa zaidi ya mwezi sasa?

Ooh pia, nilikuwa naangalia Al Jazeera hapa sasa hivi na kuna mtaalamu mmoja wa masuala ya Mashariki ya Kati kasema Israel inaitegemea Marekani kwenye karibu kila kitu….kuanzia ndege za kivita, mabomu, makombora, ujasusi, na kadhalika.

Ila watu walivyo na fantasies, wanakwambia Marekani ndo inaitegemea Israel 🤣.
 
Iran sio Israel anapiga Military target na strategy target sio huyo Israel target zake kuvunja majumba na kuwauwa watu wasio na hatia. Israel ni muwaji wa watoto akikosea step akauwe wa iran watoto Tela Aviv itakuwa History
Unaongea nini wewe ? Israel inatarget zaidi maadui wao, raia huwa ni casualities, hakuna vita isiyo na civilian casualities lakini bado Israel wanajitahidi sana kuzipunguza japo hazikwepeki

Ushahidi ni Israel kuwamaliza viongozi wa juu wote wa Hezbollah, Viongozi kibao wa Hamaas, Rais wa Iran, Shambulizi la pagers lililoua magaidi wengi, n.k.

Iran imelenga makombora 200 kwa nia ya kulipua makazi ya watu, Iran inawafadhili Hamas walioua watu kikatili sana october 7 tuliona magaidi yanayamka maneno takatifu kabla ya kumiminia risasi wayahudi kwa kudhani ni jambo takatifu kuua wayahudi.
 
Kwa ujumla Iran imeonesha professionalism kwenye medan ya vita kwani haijaua raia kama Sheria za zinavyotaka.

Pili amelenga military sites TU na inaonekana zimepigwa vilivyo. Suala La wanajeshi wangapi wamekufa au kujeruhiwa sahau Huwa ni siri.

Kuna mambo yatakuwa wazi mfano ndege zilizoharibiwa, vifaru magari vita, viwanja vya ndege n.k.

Ukiona mtu analipiza kwa kujua raia hajui vita zaidi kuitumia mihemko. Wakihisi kwa kufanya hivyo raia watawageuka viongozi wao na hata kuwapindua.

Hivyo kama ni kuchapana basi Rais wasiuwawe ndio tuone mbabe.

Tumeshuhudia Ukraine Russia akipiga maeneo ya jeshi TU tofauti na Ukraine wanapiga maeneo ya raia na huo ni ugaidi.
Hakuna professionism yoyote, Kabla makombora hayajafika Israel huwa kuna vingora vinalia watu wanakimbilia kwenye nyumba maalum za kujikinga na mabomu, Raia waliokufa ni kwa upande wa Palestina, Iran imeua mpalestina.

Pili, Makombora yaliyokuwa yanaelekea maeneo ya makazi ya watu mengi yamelipuliwa angani kwa mfumo wa Iron Dome, yaliyoachwa kwa maksudi yatue ni yale yanayoangukia sehemu za wazi zisizo na madhara ya milipuko
 
Iran sio Israel anapiga Military target na strategy target sio huyo Israel target zake kuvunja majumba na kuwauwa watu wasio na hatia. Israel ni muwaji wa watoto akikosea step akauwe wa iran watoto Tela Aviv itakuwa History
Akitaka anaua tu kaua Ibrahim rais na haniyah itakuwa vitoto mtapiamlo vya kiajemi?
 
Hata kama,lakn teknolojia ilio tumika ni ya myaud,mbona hata Iran anasaidiwa sana kwahyo Israeli nae akipata saport sio mbaya kikubwa lengo litimie, hakuna gaidi kuachwa

Teknolojia ya myahudi?

Iran anasaidiwa?

Kwamba hujui Israel Kwa Marekani ni sawa na Hezbollah au Houthi Kwa Iran?

Kwamba Israel ni ka proxy ka Marekani?
 
Hakuna professionism yoyote, Kabla makombora hayajafika Israel huwa kuna vingora vinalia watu wanakimbilia kwenye nyumba maalum za kujikinga na mabomu, Raia waliokufa ni kwa upande wa Palestina, Iran imeua mpalestina.

Pili, Makombora yaliyokuwa yanaelekea maeneo ya makazi ya watu mengi yamelipuliwa angani kwa mfumo wa Iron Dome, yaliyoachwa kwa maksudi yatue ni yale yanayoangukia sehemu za wazi zisizo na madhara ya milipuko

Hii ya kwako uswahilini inaitwa mahaba niue.
 
Back
Top Bottom