Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

...,siwezi kukaa naumwa wakati kuna Mtumishi ana suluhisho la shida yangu!!,
Sasa umekatazwa kwenda? Mbona unalialia bure tu humu? Si umeenda kupona? Umezuiwa usiende tena na tena? Hivi mnajadili nini? Kama umeona kwenda kule na ukapona maradhi yako ndio chaguo sahihi, basi upo sahihi kabisa maana nchi hii ina uhuru wa kuabudu. Sijajua unacholalamika ni nini tena wakati mtu sahihi wa kuhudhuria ibada zake umempata
 
Utajiri ni bahati Mkuu,kazi wote tunafanya ila inategemea na connection ulizonazo.Ata Elon Musk Baba yake alikuwa anamiliki mgodi wa Emerald kipindi Cha apartheid regime kule South.Boss wa Facebook Mama yake alikuwa Board member wa IBM,Dangote Babu yake alikuwa tajiri mkubwa Nigeria.Mmiliki wa Amazon alianza Biashara na mtaji wa Dola 300,000.Warren Bufet Baba yake alikuwa Mbunge wa Congress na alikuwa tajiri.Aya matajiri wa Bongo wengi wanaendesha Biashara kwa pesa za wanasiasa mafisadi.Mo na Manji hawa Historia inajulikana!
Kwani wewe kazi unayo fanya umekuwa tajiri?
Ata Wakina-Mwamposa wakikuombea au mapadri wakikuombea upate utajiri bila connection ni zero!
Kwaiyo kila Mtu aachwe aabudu anacho amini!

Mtu yeyote mwenye akili akisoma huo waraka atakuwa upande wa kanisa, Yani watu wanaambiwa waombewe ili wawe matajiri kitu ambacho hata Yesu hakufanya, Kama hufanyi kazi huwezi kuwa tajiri
 
Na Padri anayeongoza ibada kuwa waumini wamuombe Marehemu Mariam awaombee kwa Yesu,ile ni nini siyo uganga?
Bado kuna Rozali, inasaidia nini?
Acheni Double standard!
Mwamposa Ni mganga wa kienyeji anayevaa suti
 
Kwaiyo kila Mtu aachwe aabudu anacho amini!
Hilo ndilo jambo la msingi. Kila mtu aachwe aabudu anachoamini. Lakini baadhi ya wachangiaji humu wanataka RC iwaache waabudu kule na kwao, wakati RC imewaacha wakaabudu huko wanakoamini tu
 
Na Padri anayeongoza ibada kuwa waumini wamuombe Marehemu Mariam awaombee kwa Yesu,ile ni nini siyo uganga?
Bado kuna Rozali, inasaidia nini?
Acheni Double standard!
Mzee unalalamika nini? Si ukaabudu huko? Double standard za nini wakati upo huru kuabudu popote katika nchi hii nzuri? Nenda baba, sio lazima ulinganishe na RC, kama umeamua kuchagua mafuta, maji, keki na leso, nenda tu, usipoteze muda, jambo la msingi ni kwamba usiwe huku na kule, chagua sehemu inakokufaa
 
Kuna Padre amewahi kushauri unywe Bia ? Msichafue imani za watu humu,kanisani huwa wanakataza ulevi
By the way mlevi ni mtu mzima,kanisa halina muda wa kukufuatilia Bar hayo ni Maisha yako Mana ukikatazwa haliwezi kutuma mapadre Bar
Sasa mtu kwenda kwa mwamposa ndio mnatoa Hadi notisi?
 
Wala Kanisa halijatumia mabavu kama unavyodhani. Siku zote Kanisa Katoliki lina misingi na kanuni zake. Ukikiuka, lazima uwajibishwe ipasavyo. Haijalishi wewe ni muumini wa kawaida, mtawa, Padre, au Askofu!

Hivyo hakuna jipya hapo.
Sawa, kila kanisa na misingi yake iliyojiwekea, Ila tumtangulize Yesu Kwanza.
 
Kwani RC hamna Mafuta?
Unafiki siyo mzuri?heshimuni Imani za madhehebu mengine,msijifanye nyie watakatifu wakati na nyie mna upungufu.Kama RC ipo sahihi sana pasingekuwepo na Anglican,KKKT, Moravian na sasa makanisa ya uamsho.Aya madhehebu yote yalijitenga na RC kwa sababu za kutofautiana kiimani.
 
Ya mwisho inaitwa sadaka ya KUJIMALIZA! 😂 😂 😂
Wajinga wanatoa Hadi nauli za kurudia majumbani wanakosa!
Mwamposa ni NIOKO na ana kanguvu kakubwa sana kaushawishi.
Bado tunamsubiri Suguye aanze ziara za uwizi baba yao Kakobe ameshazeeka sasa
 
Ebhana Israel wanakunywa Canadian kumbe😂😂
 
Nadhani hujanipata, na pengine itakuwia vigumu kunipata kama hautaweka akili yako kuwa flexible. Point yangu ni hii; Bila haja ya kulinganisha imani tofauti, kila mtu aabudu anapoamini. Hakuna haja ya kusema, mbona wale wanafanya vile! Abudu hapo hapo kwa kujiachia, usipende kulinganisha, labda kama unaendelea kutafuta mahali palipo sahihi kwako. Lakini usilalamike kama umeshachagua. Kila mmoja azingatie anachoamini bila kulazimisha wengine. Hiyo ndio maana ya imani
 
Unaweza kuta watu wanacomment tu hata huo waraka hawajajisumbua kuusoma
 
Kwani wameambiwa wakihama watachapwa?
Hakuna mtu alielazimishwa kuwa mkatoliki hapo,
Kikubwa mtu yupo huru kuchagua moja Kati ya ukatoliki au mwamposa lakini sio mwamposa/katoliki hii ndio kitu kanisa limekataa.
Ofcoz katoliki wanamisimamo fulani hivi smtz inaboa.
 
Na RC HUWA hawatanii utasikia na ukifa hatukuziki hata kama mkisafirisha hatuwapi barua ya utambulisho huko muendako.
Kanisa lipo sahihi kabisa hata kufukuzwa ni sawa tu . huko ni kutangatanga kiimani na kunajis kanisa. Hawa wanaweza kuleta mapepokanisani na kuwaambukiza wengine.pia ni wapotoshaji wataliharibu kanisa. Kwakweli waungame na kutubu wamekosea sana. Katoliki hawafumbii macho uchafu kama vipi hao wasaliti wahame kabisa ndio watajua hawajui. Hongera kanisa katoliki.Hata wasabato waliwapiga marufuku na kuwatenga waliokwenda kwa babu loliondo kupata kikombe. Sasa Leo huyo babu yuko wapi? Eti ameonyeshwa dawa ya ukimwi subutuuuu. Niwapobgeze sana kanisa kwa kuwa makini na kuwalinda waumini wao wasitapeliwe
 
Eti Biblia anasoma Padri tu!!!,Wapi huko ambako Biblia anasoma Padri tu??, Mbona mmekalilishwa vibaya sana nyie!!.
 
Mzee wewe umeombea wangapi wakapona?,Sana sana mnaombeana tu ktk vitu vyepesi na vidogo mmejaa janjajanja tu!!. Mnaombeana tu kwenye ishu ya mapepo ambayo kimsingi sehemu kubwa si mapepo kiuhalisia bali ni msongo wa mawazo na ndio maana wengi wao ni wanawake.Km Kweli ninyi ni waombaji wazuri nendeni pale Muhimbili,Mlongazila,KCMC,Bugando na Hospitali zingine maana huko ndio kuna Wagonjwa wa Kweli na sio Wagonjwa wa mchongo (Wagonjwa waigizaji),Mimi mwenyewe Baba yangu ni Kipofu njooni mumuombee enyi manabii wa uongo msio na soni;Nyie ni watu wa ajabu sana mnafanya utapeli wa wazi wazi mchana kweupe.

Ninyi hamna Roho Mtakatifu, kwasababu Roho Mtakatifu hachagui kipi aponye na kipi asiponye,kifupi yeye hana mipaka ktk utendaji wake.Ni kwambie tu kuwa Yesu Kristo mwenyewe alitenda miujiza mingi sana, ambayo tunaweza kuiweka ktk Makundi makuu matano,yaani
1.Miujiza ya uponyaji -Kuponya wakoma,viwete,waliopooza,wenye pepo,vipofu,bubu,n.k.
2.Miujiza ya kufufua wafu-Alimfufua Lazaro
3.Miujiza ya Kutawala maumbile-Kuongeza idadi ya mikate na samaki hadi watu kushiba na kusaza,kugeuza maji kuwa divai,kutembea juu ya bahari, kugeuka sura,kupaa mbinguni.
4.Miujiza ya Kiunabii-Ndio kutabiri mambo ya baadaye, matharani alimwambia Petro kuwa kabla jogoo hajawika atamkana mara tatu na Kweli ikawa hivyo.
5.Muujiza wa Kuyashinda mauti, ndio kufa na kufufuka km alivyosema yeye mwenyewe.

Sasa ktk Makundi hayo ya miujiza ninyi hampo hata ktk kundi moja bali ni kakipengere kadogo tu ka kukemea mapepo ambayo nayo ni ya kuigiza tu!,
Utasema huyo alikuwa ni Yesu lkn unasahau kuwa hata Wanafunzi wa Yesu walitenda miujiza mingi mikubwa km vile Kuponya kiwete, Wagonjwa, Kufufua wafu (sio wafu wa mchongo bali wafu waliokufa Kweli),Sasa waliweza kufanya hayo yote kwasababu walikuwa Kweli na Roho Mtakatifu sio Roho mtakasifa na majivuno na masilahi mliye nae Ninyi.Ninyi hamna Roho Mtakatifu ndio maana mnajikita tu kuhangaika na Kuponya mapepo ya kuigiza.
 
Hili povu..mtabaki watatu kanisani wewe baba paroko na sisita.

Rc hakuna mwamko wa kiroho..kuna mafundisho ya kukariri vikongwe vya zamani vilivyokufa vya warumi..wanavyo viita vitakatifu na viwaombee.

#MaendeleoHayanaChama
Pole yako,utapata taabu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…