RC kanisa kuuubwa ila hawana nguvu za MUNGU. Wao ni porojo tu hata uwapelekee mgonjwa wa Mafia HAWAWEZI kumuombea.
Wanasubiri uumwe, uzidiwe wakupe sala ya mwisho kama PENGO alivyomfanyia Magufuli 17/03/2021.
YAANI WANAVAA MAMISALABA MAKUBWA ILA UPAKO ZERO.
ACHENI WIVU.
Mzee wewe umeombea wangapi wakapona?,Sana sana mnaombeana tu ktk vitu vyepesi na vidogo mmejaa janjajanja tu!!. Mnaombeana tu kwenye ishu ya mapepo ambayo kimsingi sehemu kubwa si mapepo kiuhalisia bali ni msongo wa mawazo na ndio maana wengi wao ni wanawake.Km Kweli ninyi ni waombaji wazuri nendeni pale Muhimbili,Mlongazila,KCMC,Bugando na Hospitali zingine maana huko ndio kuna Wagonjwa wa Kweli na sio Wagonjwa wa mchongo (Wagonjwa waigizaji),Mimi mwenyewe Baba yangu ni Kipofu njooni mumuombee enyi manabii wa uongo msio na soni;Nyie ni watu wa ajabu sana mnafanya utapeli wa wazi wazi mchana kweupe.
Ninyi hamna Roho Mtakatifu, kwasababu Roho Mtakatifu hachagui kipi aponye na kipi asiponye,kifupi yeye hana mipaka ktk utendaji wake.Ni kwambie tu kuwa Yesu Kristo mwenyewe alitenda miujiza mingi sana, ambayo tunaweza kuiweka ktk Makundi makuu matano,yaani
1.Miujiza ya uponyaji -Kuponya wakoma,viwete,waliopooza,wenye pepo,vipofu,bubu,n.k.
2.Miujiza ya kufufua wafu-Alimfufua Lazaro
3.Miujiza ya Kutawala maumbile-Kuongeza idadi ya mikate na samaki hadi watu kushiba na kusaza,kugeuza maji kuwa divai,kutembea juu ya bahari, kugeuka sura,kupaa mbinguni.
4.Miujiza ya Kiunabii-Ndio kutabiri mambo ya baadaye, matharani alimwambia Petro kuwa kabla jogoo hajawika atamkana mara tatu na Kweli ikawa hivyo.
5.Muujiza wa Kuyashinda mauti, ndio kufa na kufufuka km alivyosema yeye mwenyewe.
Sasa ktk Makundi hayo ya miujiza ninyi hampo hata ktk kundi moja bali ni kakipengere kadogo tu ka kukemea mapepo ambayo nayo ni ya kuigiza tu!,
Utasema huyo alikuwa ni Yesu lkn unasahau kuwa hata Wanafunzi wa Yesu walitenda miujiza mingi mikubwa km vile Kuponya kiwete, Wagonjwa, Kufufua wafu (sio wafu wa mchongo bali wafu waliokufa Kweli),Sasa waliweza kufanya hayo yote kwasababu walikuwa Kweli na Roho Mtakatifu sio Roho mtakasifa na majivuno na masilahi mliye nae Ninyi.Ninyi hamna Roho Mtakatifu ndio maana mnajikita tu kuhangaika na Kuponya mapepo ya kuigiza.