Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Wao ni sawa kwa muumini kushinda kidimbwi Kula gambe hawana shida na huyo atapokea tu sakramenti , Ila mtu anaeenda kutafuta uso wa Mungu ndio shida
Mwamposa nyomi alilopiga Iringa ni kisanga na nusu wameumia.
Alafu alivyo muhuni aliwaonyesha namna anavyokusanya mapato 😝😝

Amepata mahela ya kutosha
 
Wala Kanisa halijatumia mabavu kama unavyodhani. Siku zote Kanisa Katoliki lina misingi na kanuni zake. Ukikiuka, lazima uwajibishwe ipasavyo. Haijalishi wewe ni muumini wa kawaida, mtawa, Padre, au Askofu!

Hivyo hakuna jipya hapo.
Linaishi katika misingi ya Torati?
 
Kuna comments zinachekesha sana HUMU. Ila Mwamposa atabakia kuwa Man of The Match.

Gwajima ...chali
Mzee wa upako...chali
Suguye....chali
Geordavie...chali
Malisa...chali
Rwakatare...kaburini

Tusubiri baada ya Mwamposa na ni ataibuka.

Hivi Nabii Frank aliishia wapi????
 
Katotoizi simuoni kwenye list au nae chali
 
Sasa wamerudi katoliki kufata nin
 
Wanatishia hawakuziki. Hawajui MTU ukiwa mtakatifu hata ukiliwa na Simba mbinguni unaingia.
Kuna baadhi ya viongozi huwa wanajiona ni watakatifu sana, kuna msiba fulani mwamba alifariki kwa tungi yani alilala hakuamka tena na aligundulika baada ya siku tatu ameshaharibika.

Wakaleta hayo mambo alikuja kuzikwa na muinjilisti na ule ukoo wote ukaachana na ulutheri
 
Dah walimnyanyapaa, HIYO haifai.
 
Hii inataka iwe battle kama ya Kanisa Katoliki Jimbo la Ifakara&Mahenge na Bibi Kalembwana aliyekuwa ananyoa watu kutoa uchawi, illikuwa Ukienda kunyolewa unatengwa na kanisa. Askofu Ndorobo ilibidi amfate Bibi Kalembwana
Kkkkk noma sana.
 
Kwa hili kanisa limezingua sana..walitakiwa wajue sababu ya kwanini hao waumini wameenda kwa mwaposa.

Itafute chanzo na itibu chanzo..sio vitisho vya kanoni laws.

Dini ni imani na imani inaweza badilika muda wowote mtu akiamua..kulazimisha watu ni kukosa na kukiuka uhuru wa kuabudu.

Sisi kama wakristo tu wa moja katika kristo.

Hao maporoko wajichunguze wao kwanza...waje na majibu ya kwanini waumini wanakimbilia haya makanisa ya kiroho.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kanisa la Roman Catholic Iringa limefukuza na kutoa onyo kali kwa washirika wake waliohudhuria kongamano la Mwamposa na wengine walionunua maji na mafuta kwenye mkutano wake

View attachment 2236071
View attachment 2236072
Kwa kweli watanzania ni watu wasiojitambua, Mwamposa anawauzia maji na mafuta toka Israel wakati Waisrael wenyewe wana matatizo lukuki na hivyo vitu haviwasaidii hata kidogo, hivi mtu unashindwa nini kujiuliza au ni kule kuchotwa akili kama afanyavyo T.B. Joshua?
 
Kanisa katoliki linachukia kupiteza sadaka .

Maana wanajua waumini wao wakienda kwa mwamposa wanatoa sadaka ambazo walipaswa wapokee wao katoliki

Hizi dini ni upigaji tu
Mtu yeyote mwenye akili akisoma huo waraka atakuwa upande wa kanisa, Yani watu wanaambiwa waombewe ili wawe matajiri kitu ambacho hata Yesu hakufanya, Kama hufanyi kazi huwezi kuwa tajiri
 
Mwamposa ni kama Gwajima, Antony Lusekelo, Nabii Shilla, Masanja Makandamizaji, Mc Pilipili, Bon Mwaitege, na wengineo wengi!

Ni wapigaji tu.
Umemkosea Sana mzee wa Upako ,yeye huwa anasema kabisa kwamba yeye ni Kama Mwalimu anafundisha yaliyo mema na ya kumpendeza Mungu na yeye ni Binadamu so wewe fuata mafundisho yake tu
 
Wao ni sawa kwa muumini kushinda kidimbwi Kula gambe hawana shida na huyo atapokea tu sakramenti , Ila mtu anaeenda kutafuta uso wa Mungu ndio shida
Kuna Padre amewahi kushauri unywe Bia ? Msichafue imani za watu humu,kanisani huwa wanakataza ulevi
By the way mlevi ni mtu mzima,kanisa halina muda wa kukufuatilia Bar hayo ni Maisha yako Mana ukikatazwa haliwezi kutuma mapadre Bar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…