TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

Watuhumiwa watakamatwa na watauwawa kwa adhabu ya firing squad
 
hakuna Kijiji Cha njaapanda ya tosa Bali Kijiji Cha ugwachanya

Huyo ,mama namfahamu vizuri sana ,wale tuliohitimu kidato Cha 6 2000 tosamaganga high school ,mama huyu alikuwa mke wa kibiki aliyekuwa afsa ugani na kwao palikuwa hapa kitongoji Cha banawanu lilipo sanamu la bikira maria ukitokea njaapanda nyuma hapa kabla hujavuka mto kiporyi

imeniuma sana ,mumewe na alikanyagwa na gari nyang'anyang'a ipogolo

RIP....katibu ,ubunge huu SHIDA sana na alikuwa na misimamo sana kama alionyesha ubungeni upande itakuwa hivyo
 
Watu Wasiojulikana Wanadaiwa wamemvamia aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi .

Taarifa ambayo Matukio Daima media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia Leo katika Kijiji Cha njia panda ya Tosa wilaya ya Iringa Vijijini nje kidogo na mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.
Kuwa baada ya kumshambulia kwa risasi alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ya Tosamaganga ambako amefariki Dunia.

Matukio Daima media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo John Kiteve amesema tukio Hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo .

Huku kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi hajaweza kupatikana ili kuthibitisha tukio Hilo Bado Matukio Daima media inaendelea kufuatilia zaidi.

Chanzo: Matukio Daima Media
Mwenyekiti wao alisema "Kifo ni Kifo Tu"
 
hakuna Kijiji Cha njaapanda ya tosa Bali Kijiji Cha ugwachanya

Huyo ,mama namfahamu vizuri sana ,wale tuliohitimu kidato Cha 6 2000 tosamaganga high school ,mama huyu alikuwa mke wa kibiki aliyekuwa afsa ugani na kwao palikuwa hapa kitongoji Cha banawanu lilipo sanamu la bikira maria ukitokea njaapanda nyuma hapa kabla hujavuka mto kiporyi

imeniuma sana ,mumewe na alikanyagwa na gari nyang'anyang'a ipogolo

RIP....katibu ,ubunge huu SHIDA sana na alikuwa na misimamo sana kama alionyesha ubungeni upande itakuwa hivyo
Anhaa kumbe ndio ilivyo, polen sana
 
Back
Top Bottom