TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

CCM wamezoea kuuana kwaajili ya vyeo.

Hapo uchunguzi unatakiwa uanzie kwa kuangalia huyu katibu alikuwa upande gani miongoni mwa watakaogombea ubunge mwakani.

Kutokana na nafasi yake, kama alionekana kuegemea upande mmojawapo wa wanaotaka kugombea uchaguzi wa mwakani, kwa hulka na ushetani uliopo ndani ya CCM, siajabu upande mwingine, wameamua kumwondoa ili asuwe kikwazo kwenye kura za maoni.

'CCM hawaachiani maji kwenye glass mezani' - Jakaya Kikwete.

Wamezoea kuteka na kuwaua wapinzani na wanaomkosoa Rais. Sasa wameanza kumalizana ndani kwa ndani!! Laana imeanza kufanya kazi.
 
Mauaji ya yasiyo na mwisho ya wasiojulikana yataligharimu taifa.
Viongozi wetu wanacheza na moto.
 
Kwahiyo yeye alipuuza ushauri wako.
Gentleman,
nikishawajibika kushauri, sina haja kufuatilia nani kazingatia au kupuuzia mawaidha yangu mujarabu kwa wadau wote JF. hilo ni juu yako..

huna haja kuja kunishukuru au kunilaumu gentleman 🐒
 
Kama ambavyo tunapiga kelele haya kutokea kwa viongozi wa CDM, vivyo hivyo kwa CCM.

Haya hayapaswi kutokea katika jamii yetu, tuungane kuupinga unyama huu.
Ushetani ukishaingia katika taasisi, kuuondoa ni kazi ngumu sana, labda uifute kabisa hiyo taasisi.

CCM kwa sasa imekuwa taasisi ya kishetani. Kwao kuuondoa uhai wa mtu kwaajili ya madaraka wamekwishaiweka miongoni mwa mbinu za ushindi. Watu wakishaamini hivyo, ni kazi sana kuwabadilisha. Maadam CCM bado ipo, na ipo na watu wale wale wanaowarithisha watoto wao mbinu zile zile za kishetani, tutarajie kuona huu ushetani ukiendelea.
 
Katibu Mkuu wa CCM Dr Nchimbi ataongoza Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kwenye mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kilolo

Mazishi hayo yatahudhuriwa na Wapenda Amani wa kitaifa na Kimataifa wakiwemo Mitume na Manabii pamoja na Mashehe na Maaskofu

Ahsanteni sana 🐼
 
Mohamed kawaida kamjibu Twaha Mwaipaya kuwa tukio la utekaji jana ni drama, kwahyo Mohamed Kawaida ajitokeze aseme kuuwawa kwa katibu wa CCM ni drama???
 
Karma has begun to work
First they came for the socialists, and I did not speak out—because I was not a socialist.

Then they came for the trade unionists, and I did not speak out—because I was not a trade unionist.

Then they came for the Jews, and I did not speak out—because I was not a Jew.

Then they came for me—and there was no one left to speak for me.

—Martin Niemöller
 
Watu Wasiojulikana Wanadaiwa wamemvamia aliyekuwa Katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi.

Taarifa ambayo Matukio Daima Media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia leo Novemba 13, 2024 katika Kijiji cha Njia Panda ya Tosa, Wilaya ya Iringa Vijijini nje kidogo na Mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.
Kuwa baada ya kumshambulia kwa risasi alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ya Tosamaganga ambako amefariki Dunia.

Matukio Daima Media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve amesema tukio hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo.

Huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi hajapatikana ili kuthibitisha tukio hilo, bado Matukio Daima Media inaendelea kufuatilia zaidi.

Chanzo: Matukio Daima Media

==============================

JamiiForums imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, simu imepokelewa na msaidizi wake ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tukio hilo akasema “Kamanda yupo kikaoni, tukio hilo bado hajalizungumzia.”


Pia, Soma:
Kifo kinauma, lakini nionavyo ni sawa na KIFO CHA KIBAO wa CHADEMA, taratibu tunaelekea mahali kuzuri, ambalo tutaelewana, amesalia mmoja ABDUL, siku ikitokea yule saa 💯 mamake atakoma kusema ni DRAMA!!!🤔🤔🤔🤔
 
Hii habari siiamini kabisa maana najua sisi Wana CCM huwa hatutekwi.wanaotekwa ni wavyama pinzani tu fullstop
 

Attachments

  • 20241112_212858.jpg
    20241112_212858.jpg
    108.3 KB · Views: 2
Back
Top Bottom