Moise Aimar
JF-Expert Member
- Sep 26, 2012
- 216
- 406
Watu Wasiojulikana Wanadaiwa wamemvamia aliyekuwa Katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi.
Taarifa ambayo Matukio Daima Media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia leo Novemba 13, 2024 katika Kitongoji cha Banawanu, Kijiji cha Ugwachanya, Kata ya Mseke Tarafa ya Mlolo nje kidogo na Mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.
Kuwa baada ya kumshambulia kwa risasi alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ya Tosamaganga ambako amefariki Dunia.
Matukio Daima Media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve amesema tukio hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo.
Huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi hajapatikana ili kuthibitisha tukio hilo, bado Matukio Daima Media inaendelea kufuatilia zaidi.
Chanzo: Matukio Daima Media
JamiiForums imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, simu imepokelewa na msaidizi wake ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tukio hilo akasema “Kamanda yupo kikaoni, tukio hilo bado hajalizungumzia.”
Pia, Soma:
Taarifa ambayo Matukio Daima Media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia leo Novemba 13, 2024 katika Kitongoji cha Banawanu, Kijiji cha Ugwachanya, Kata ya Mseke Tarafa ya Mlolo nje kidogo na Mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.
Matukio Daima Media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve amesema tukio hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo.
Huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi hajapatikana ili kuthibitisha tukio hilo, bado Matukio Daima Media inaendelea kufuatilia zaidi.
Chanzo: Matukio Daima Media
==============================