TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Wadau haya maombo yanatofanywa na jeshi la polisi ni mambo ya kutafakari kwa makini sana.Kwa mtazamo na maoni yangu hii inaweza kuwa ni mbinu ya kutafuta sababu ya kukifuta chama hiki ambacho kwakweli ni tishio kwa ccm.Haya mauji kwenye mikutano ya chadema yanaweza kutumika kama sababu ya kuhalalisha hujuma hii dhidi ya chadema.

Tukumbuke kauli iliyotolewa na Wassira hivi karibuni ya kutishia kukifuta chama hiki na muendelezo wa matukio kama haya.Hawa jamaa kwao kitu cha muhimu ni kuhakikisha wanabaki madarakani kwa gharama yoyote ile.Watanzania tusisahau ukweli kwamba hofu yao kubwa ni kuja kuwajibika kwa madhambi yao mbali mbali kama mauaji,ufisadi wizi n.k.Hivyo njia pekee kwa wao kuwa salama ni kuhakikisha wanabaki madarakani.Wanajua kabisa endapo chadema itakamata dola watafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka.

Tutarajia machafuko zaidi ya haya siku zijazo kwani hata chadema nao hawatakubali kunyanyaswa na kuonewa na serikali hii.

Kibaya zaidi wakuu msisahau kuwa msajili wa vyama vya siasa nchini ni mteule wa raisi na utendaji wake unajulikana.

Lets wait and see, but we have to do something as a nation to defeat this new colonialism.
 
Hivi kwa nini Dr Slaa na genge la wahuni wenzake hawakamatwi na kuwekwa korokoroni?
 
Namsikitikia sana huyu RPC na kikundi chake. Akumbuke Makaburu hawakuwahi kufikiria kuwa watatawaliwa na waafrika.


Moi hakuwahi kufikiria kuwa kuna siku atarudi mtaani na kuwa mwuuza magazeti.


Kuwa kuna siku Gadafi atakufa na kuzikwa kama mbwa.....


Hata akifariki salama kwa huyo aliyetoa roho ya Mwandishi wetu.,.... Kizazi chake kitahukumiwa na damu ya huyu kamanda. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen
cheki kamanda wa iringa hata kifungo cha kati hakifungi afu hanatoa maagizo feki siku zinahesabiwa
 
colleagues! hali ni tete! divide and rule inonekana wazi hapa jamving(jf). kuna members ambao in the near future watahesabika kama 'interahamwe'. ee Mungu saidia Tanzania
 
Chadema walianza na mauaji iramba wakaendelea morogoro,na sasa wameua iringa wataendelea mikoa mingine kadri watakavohitaji kumwaga damu

hayakuanza iramba, umesahau arusha, igunga, nyamongo nk. usiwe na hofu tundu lissu anaisuka mahakama iwe more professional than political na ameishasema wauaji watatafutwa leo, kesho na hata kesho kutwa, wakiwa kwenye uniform au nje ya uniform zinazowapa jeuri, haki itapatikana tu, hata kama itacheleweshwa. Ile sheria ya inquest inayompa mamlaka coroner kuchunguza vifo vyenye utata, sheria inayopigwa dana dana na ccm ili kuficha mauaji na uovu wao kwa jamii itaanza kutumika muda siyo mrefu wapende wasipende. Iliwachukua miaka zaidi ya 40 wairaq kuweza kumnyonga saddam hussein kwa mauji yake kwa raia, nawahurumia sana hawa wanaotumiwa na ccm kuua, siku watakaposimamishwa vizimbani ccm haitakuwa pamoja nao kama vile baath party ilivyoshindwa kumsaidia saddam hussein siku ya hukumu yake
 
Si majulikana kwa kutukana na nani asiyejuwa kuwa mnauwa? lakini naona sasa mnajipalilia mkaa wenyewe. Damu za watu hazipotei bure. Tumewashtukia.

Na mimi ninakuhakikishia kabisa kwamba damu ya mtu haipotei bure ndugu yangu zomba. Kama ni CDM wameua basi adhabu ipo kwao na kama ni policeccm au ccm yenyewe basi mungu huyu ni wa ajabu. Ila ninakuomba sana usifikirie kwa kutumia hayo ya nyuma yako (Makal)
 
izi mbinu chafu kabisa za magamba hali ni mbaya hasa kwa ccm
 
Wajaribu kufanya hivyo waone,2015 mbali sana,here we go!
 
Iweje ajeruhiwe Polisi na afe Mwandishi kwa risasi? Hao ni chadema tu hakuna mwingine.

Nasema chadema si chama cha siasa na hata bendera yao inaashiria umwagaji damu.

Mwenye akili timamu anaweza kujua kilichojilia kwamba ni mbinu zinazofanywa kuonyeshwa kwamba Chadema kimefanya hivyo, tujiulize, kwa nini matukio ya maafa hutokea polisi wanapotumia nguvu na pale ambapo polisi hawatumii nguvu hakuna maafa? Hawa wanaotunga mbinu hizo hawatumii ujuzi ulio na upeo, kwani matukio haya hata mtoto mdogo tu najua ni njama za polisi wanaotumiwa, na si polisi wote, ni baadhi tu waliochomekwa, na yatokeayo hata polisi wengine waliopo wanashangaa kilichotokea na wahusika kutochukuliwa hatua stahiki.

Jambo hili nimetonywa na mmoja wa polisi toka ndani ya chungu kunakopakuliwa vyakula. Siri hizi zitafichuka zaidi kwani unaposhindana na adui usiyejua matawi yake yalivyoenea ni sawa na kugongesha mpira ukutani.


HATARI YAONYESHA VIONGOZI WA KITAIFA CHADEMA WALINDWE
Matukio haya ipo siku watatumia njia hizo hizo kuua viongozi wa upinzania wanaoonekana kuwa tishio kwao. Kuwa waangalifu katika maandamano na matukio ya kuchangamana na watu, lo lote laweza kutokeka kadiri ya utabiri wa kinabii, na tunaomba Mungu apishe mbali hayo (God forbid).

Viongozi wa Chadema watangulize zaidi hekima na busara na kuwa na subira katika harakati zao, ili hoja dhaifu zisitumike kuleta maafa kwa taifa letu.

Kumbukeni hoja ya kuchagua nani wa kumwua ni kama la kupangwa ili kuleta chuki ya wananchi kwa Chadema. Huwezi kuamini kulengwa mwandishi huyo zaidi ya wale waliokuwa mbele yake.
Ni jambo la kujiuliza sana tu na jibu lake ni la mbinu za kimafya ambazo hata unayefanya kazi naye hajui kama una kazi mbili.
 
Doubts on reasoning capacity.
Rest in Peace Daudi Mwangosi.
Hawa polisi wetu hatuwaelewi kwani bomu la machozi linaweza kumuua mtu au wametumia silaha za moto? Tunaomba tupewe taarifa kamili inaonekana polisi wamezoea kuua na kila mara inapotokea hakuna taarifa yoyote ya maana au kufukuzwa kazi kwa polisi aliyehusika. IGP mwema kuwa makini na vijana wako wabakuharibia.
But all in all hawa chadema hawasikii na wamezoea kutoa watu kafara manake ni juzi tu amekufa mtu moro na leo iringa. Kwani hawa cdm wangesimama mpaka sensa ikaisha wangekupukiwa nini? Cdm wauaji wakubwa lawana sio kwa polisi tu hata kwao wenyewe.
Huyu slaa na mwenzie mbowe ndio viongozi wakuu wa cdm na wameshindwa kabisa kuendesha chama kishawapwaya. Kama wao ndio wangeongoza nchi lets say wao ndio watawala jambo ambalo haliwezi kutokea hata wakiua watanzania wote wangekubali kuona watu hawawatii kama wao wanavyodharau serikali iliyoko madarakani?
Cdm kilikuwa ni chama changu nakipenda lakini siku zunavyoenda nimekichoka na kadi yangu ya uanachama nimeichana, wasipoangalia kama wataendelea kufikiri kwa kutumia masaburi basi hata uchaguzi ujao wataambulia majimbo machache sana.
 
I still remain non loving polisi. Iron boyz! No reasoning no thinking. Shiiit!
 
Hiki chama cha wauaji kifutwe tu. Kila wanapokwenda wanauwa.
 
Watanzania tuache utani, Hawa Police tunaona wanafanya mambo mazuri hadi siku watakapoua mkeo, mumeo, mtoto wako, shemeji yako, baba yako, mama yako nk. Jamani tatizo hapa ni police na siyo raia. Hawa raia wanakua hawana chochote tena wapo kwenye tawi lao. Je ingekuwa CCM wangewafyatulia risasi na mabomu. Hapa Damu ya mtanzania mwingine asiye na hatia imemwagika!!!!
:A S cry:
 
sio siri chadema hata kama hamhusiki ni rahisi kabisa kuunganisha hizi vurugu na haya maandamano kumbukeni kuwa watanzania wengi hawajaelimika na msifananishe hata kidogo maandaman yenu na yale yaliyotokea kule Misri kwa sababu zifuatazo:
. maandamano ya misri yalikuwa yanaongozwa na wananchi wa kati( middle class)
.maandamano ya cdm yanahusu vijana ambao hawajui watapata nini siku ya mwisho

Wewee!! Sijui makupe mnadhani sifa kwa hayo myafanyayo,hukumu yenu ina karibu si muda mrefu, watanzania wa sasa si wa enzi za mwalim,subiri utaona,OMBA UZIMA.
 
Remmy,ile thread niliyoianzisha kupata maoni ya kuhusu umuhimu pamoja na namna ambayo wananchi wanaweza kujilinda imeshafutwa.Sijui kwanini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom