TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

uhuru kweli umezidi kiasi kwamba kina Slaa wana achwa waendelee kuwepo mitaani wakati walikua wanatakiwa kuwa milembe.

Mkuu,nilishawi kutoa ushauri hapa JF wa kumsaidia yule babu kupima afya ya kichwa wafuasi wake watiifu wakatukana.
 
Wadau haya maombo yanatofanywa na jeshi la polisi ni mambo ya kutafakari kwa makini sana.Kwa mtazamo na maoni yangu hii inaweza kuwa ni mbinu ya kutafuta sababu ya kukifuta chama hiki ambacho kwakweli ni tishio kwa ccm.Haya mauji kwenye mikutano ya chadema yanaweza kutumika kama sababu ya kuhalalisha hujuma hii dhidi ya chadema.

Tukumbuke kauli iliyotolewa na Wassira hivi karibuni ya kutishia kukifuta chama hiki na muendelezo wa matukio kama haya.Hawa jamaa kwao kitu cha muhimu ni kuhakikisha wanabaki madarakani kwa gharama yoyote ile.Watanzania tusisahau ukweli kwamba hofu yao kubwa ni kuja kuwajibika kwa madhambi yao mbali mbali kama mauaji,ufisadi wizi n.k.Hivyo njia pekee kwa wao kuwa salama ni kuhakikisha wanabaki madarakani.Wanajua kabisa endapo chadema itakamata dola watafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu mashitaka.

Tutarajia machafuko zaidi ya haya siku zijazo kwani hata chadema nao hawatakubali kunyanyaswa na kuonewa na serikali hii.

Lets wait and see, but we have to do something as a nation to defeat this new colonialism.

CDM wafutwe kwasababu zipi sa msingi?CCM hayo ndiyo maombi yenu mchana na usiku ili aliwezi kurudisha mlipoteza mbele ya Jamiii.
 
good thought..thinking in the same vein. when they scrap out chadema, what will hapen to MPs under chadema? Will they call for mini election? Anyway, I guess they don't bother of the concequences there after. Let them deregister thhis party if it will make them enjoy a good sleep with sweet dreams
 
Chadema walianza na mauaji iramba wakaendelea morogoro,na sasa wameua iringa wataendelea mikoa mingine kadri watakavohitaji kumwaga damu

Ukiona hivi ujue shida ipo. Mungu huyu ni wa ajabu hata siku moja mungu hadanganywi wala hadanganyiki lakini ukweli siku moja utajulikana na wahalifu wataadhibiwa. Ila ninakuomba uache kufikiria kwa kutumia hayo mananihii ya nyuma. hata kama ni shabiki.
 
hakika hawawezi kusafisha roho za watanzania hata wakifuta chadema tutaitoa ccm kwa garama yoyote binafsi niko tayari hata kama itagarimu maisha yangu nimechoka na manyanyasohaya
 
kuifuta chadema sio suluhisho,bali suluhisho ni kufuta ideology ya mabadiliko kitu ambacho hakiwezekani!
2015 ni tamati ya mabadiliko,hii ina maana kuwa either tuwauwe wanamabadiliko wote au tukubali mabadiliko!
 
Huyu kamanda wa polisi hawezi kuongea chochote kwani alipohojiwa na waandishi wa habari alisema "anawakaribisha" Chadema mkoani kwake na anaahidi ushirikiano na wao Chadema...........hata hivyo hicho kifo ni ushirikiano pia.
 
Labda na Chama cha magamba kifutwe!. La sivyo patakuwa padogo!. Kwa ufupi patachimbika!.
 
Mkuu,nilishawi kutoa ushauri hapa JF wa kumsaidia yule babu kupima afya ya kichwa wafuasi wake watiifu wakatukana.


Mingoi, Mwenye akili timamu anaweza kujua kilichojilia kwamba ni mbinu zinazofanywa kuonyeshwa kwamba Chadema kimefanya hivyo, tujiulize, kwa nini matukio ya maafa hutokea polisi wanapotumia nguvu na pale ambapo polisi hawatumii nguvu hakuna maafa? Hawa wanaotunga mbinu hizo hawatumii ujuzi ulio na upeo, kwani matukio haya hata mtoto mdogo tu najua ni njama za polisi wanaotumiwa, na si polisi wote, ni baadhi tu waliochomekwa, na yatokeayo hata polisi wengine waliopo wanashangaa kilichotokea na wahusika kutochukuliwa hatua stahiki.

Jambo hili nimetonywa na mmoja wa polisi toka ndani ya chungu kunakopakuliwa vyakula. Siri hizi zitafichuka zaidi kwani unaposhindana na adui usiyejua matawi yake yalivyoenea ni sawa na kugongesha mpira ukutani.


HATARI YAONYESHA VIONGOZI WA KITAIFA CHADEMA WALINDWE
Matukio haya ipo siku watatumia njia hizo hizo kuua viongozi wa upinzania wanaoonekana kuwa tishio kwao. Kuwa waangalifu katika maandamano na matukio ya kuchangamana na watu, lo lote laweza kutokeka kadiri ya utabiri wa kinabii, na tunaomba Mungu apishe mbali hayo (God forbid).

Viongozi wa Chadema watangulize zaidi hekima na busara na kuwa na subira katika harakati zao, ili hoja dhaifu zisitumike kuleta maafa kwa taifa letu.

Kumbukeni hoja ya kuchagua nani wa kumwua ni kama la kupangwa ili kuleta chuki ya wananchi kwa Chadema. Huwezi kuamini kulengwa mwandishi huyo zaidi ya wale waliokuwa mbele yake.
Ni jambo la kujiuliza sana tu na jibu lake ni la mbinu za kimafya ambazo hata unayefanya kazi naye hajui kama una kazi mbili.
 
Nadhani CCM wana akili ya kutosha kuweza kutambua jambo hilo haliwezekani...
 
Watanzania tuache utani, Hawa Police tunaona wanafanya mambo mazuri hadi siku watakapoua mkeo, mumeo, mtoto wako, shemeji yako, baba yako, mama yako nk. Jamani tatizo hapa ni police na siyo raia. Hawa raia wanakua hawana chochote tena wapo kwenye tawi lao. Je ingekuwa CCM wangewafyatulia risasi na mabomu. Hapa Damu ya mtanzania mwingine asiye na hatia imemwagika!!!!
:A S cry:
Hao wote uliowataja hapo juu Dr Slaa hana na waliobaki hai amewatelekeza.Hana cha kupoteza .
 
Kama magamba wanataka wote wakaishie The Hague basi wajaribu kukifuta CHADEMA, amani iliyopo sasa ni matunda ya chama hiki kwani kinawapa matumaini Watanzania walionyanyaswa kwa miaka mingi vile wanaamini CHADEMA watabadilisha mfumo.Hao cjui UVCCM ni mtandao wa watoto wa vigogo pamoja na vijana wachache wasiojitambua.Hakika nasema...damu yangu itakufa pamoja na CHADEMA lakini naamini hakuna awezaye kushindana na nguvu ya umma kwani ni sauti ya Mungu!
 
Polisi wakumbuke wengi woa tunaishi nao hukuhuku street, tutaanza kuwapiga hata manati tu.
 
Tunaelekea wapi sasa? Ilianzia Arusha, ikaenda huko Igunga kukawa na Majeruhi, Ndago akafa mtu, Morogoro uhai wa Ally ukazimwa na sasa uhai wa Mwangosi umezimwa kama mshumaa. Tunaenda wapi na je tutafika salama au hatutafika ama tutafika tukiwa hoi na vipande vipande? Leo mauaji kesho mauaji basi hatuko salama inabidi kama taifa tufanye kitu.
 
Hivi polisi wana nini? Wametumwa au? Hii damu inayoingia ardhini kwa sababu za maslahi ya wachache wasiotaka ushindani wa kistaharabu haitapotea bure. Italia na Mungu atasikia tu. Haki na ukweli hauwezi kuzimwa kwa mtutu.
 
Kweli nimeamini ndio kwanza tunapigania uhuru kutoka kwa wakoloni weusi ambao na hatari zaidi.RIP Mwagosi damu yako ni petrol ktk moto wa ukombozi.Huyo polisi naye kapigwa na nn?
 
Tendwa hawezi kuwa na hoja za msingi kuifuta CDM, polisi waue then CDM walaumiwe?
 
Ukiangali kwa umakini wanoua siyo polisi, bali ni kikundi maalumu ambacho kimepandikizwa ndani ya polisi ili kuhakikisha kuwa CDM wanapoteza imani kwa wananchi. Angalia mtiririko wa matukio na aina ya mauaji.
Na lazima itakuwa ni ule mkakati aliotangaza Dr Slaa.
Whats wrong with CCM? Hamkupewa hati miliki ya taifa hili JAMANI kuweni na utu hata kwa kusingiziwa, hawa wanaouawa wana familia zao hawa.
 
There are currently 1916 users browsing this thread. (365 members and 1551 guests)

JAMANI KAMA KUNA MUHUSIKA AMONG THE PEOPLE BROWSING KWA KWELI ULICHOFANYA SI SAWA INAUMA SANA SANA TENA MUNGU AWATAZAME WALIOSHIRIKI,WHY TUNAENDA WAPI?
 
Back
Top Bottom