kissa anyigulile
JF-Expert Member
- Apr 21, 2017
- 1,550
- 1,742
Na hizo Benki nazo tatizo.Wamefanya makosa mengi, Kuhamisha kwenda benki, hilo kosa la Kwanza, kujihamishia kwenda kwenye namba zao binafsi, ilitakiwa kabisa wakishapiga hivo kwanza wanazipoza wanaziweka kwenye bitcoin wallet zoote, kule amna udubwasha zinakua safe na private kabisa.
Wangetafta mchaga mmoja hapo wangewin deal. [emoji16][emoji16]
Mhhhh!!!,Ndo nini Mkuu??.Inflated
Kumbe harrier zimepanda bei. Milioni 72 sio mchezoKamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ametoa ripoti ya matukio kadhaa ikiwemo lililohusisha wizi wa zaidi ya Shilingi Bilioni mbili mkoani humo.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000= mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED ambapo wakala wa Selcom aitwaye TYSON KASISI wa mkoani Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda nambari mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki.
Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya tarehe 9 Novemba 2021 hadi 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo TYSON KASISI kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.
Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho cha TSh 2,129,856,000=.
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000= kutoka kwa watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.
Aidha, kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783= zimezuiliwa katika moja ya benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.
Upelelezi uliofanyika mpaka sasa umebaini kuwa genge la uhalifu na wizi wa fedha za Selcom uliongozwa na watu watatu ambao ni TYSON KASISI, PATRICK CHALAMILA na EVARISTO CHALAMILA ambao wamebainika kuwa wanufaika wakuu wa uhalifu huo.
Halikadhalika, mali ambazo ni mazalia ya uhalifu zimekamatwa na kuhifadhiwa ikiwa ni magari manne (4) yenye thamani ya TSh 303,000,000= ambayo ni;
i. SCANIA yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 128, 000,000=.
ii. MITSUBISH FUSO usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 75,000,000=.
iii. TOYOTA HARRIER usajili namba T 719 DXX yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 72,000,000=.
iv. NISSAN JUKE usajili namba T 605 DXV yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 28,000,000=.
Pia imekamatwa gari Toyota IST yenye namba za usajili T 576 DRN mali ya PATRICK CHALAMILA lililotumika kufanikisha uhalifu kwa kusafirisha fedha za wizi kutoka Madibira Wilayani Mbarali na Ilula Wilayani Kilolo kwenda kuzificha Kilombero mkoani Morogoro.
Ushahidi uliokusanywa mpaka sasa umetosha kuwafikisha watuhumiwa kumi (10) Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa makosa ya Kuongoza Genge la Uhalifu na Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu.
Kama puto, hiyo bei ya 72m kwa Harrier, hiyo bei imepigwa juu kwajuu!Mhhhh!!!,Ndo nini Mkuu??.
Acha uongo!Wamefanya makosa mengi, Kuhamisha kwenda benki, hilo kosa la Kwanza, kujihamishia kwenda kwenye namba zao binafsi, ilitakiwa kabisa wakishapiga hivo kwanza wanazipoza wanaziweka kwenye bitcoin wallet zoote, kule amna udubwasha zinakua safe na private kabisa.
Wangetafta mchaga mmoja hapo wangewin deal. [emoji16][emoji16]
Haha sio uongo mzeee, Means utakua na line fake kama zotee, Ukishajihamishia mzigo, unaingia kwenye simu yako alafu unanunua local bitcoins Hapo inakua imeishaAcha uongo!
Utahamishaje pesa zote hizo kwenda e-wallet bila kupitia mfumo rasmi wa kifedha (bank/mobile money transfer).
Fedha yoyote kwenda account ya nje lazima ipite BoT.
Pale ukipita mzigo mrefu lazima wapate red alarm. Wanazuia
Wenzetu mnaishi dunia ya peke yenu kabisa. Achana na harrier , zipo Crown hadi za mil 150.Toyota Harrier ya million 72, ikoje hiyo??.
Niliwahi kukuambia huna akili, hiyo harrier kweye picha unaweza kununua kwa sh ngapi?Inflated
Wewe huyoWapuuzi hao wanaibaje hela kizembe hivyo? Si wangeniambia niwape njia iliyo nyooka wangepiga pesa washangae
Utakua unaishi kijijini na huna elimu, thamani ya gari huendana na mwaka uliotengenezwa(model)Kama puto, hiyo bei ya 72m kwa Harrier, hiyo bei imepigwa juu kwajuu!
Huenda hao polisi lile la ntwara limewashtua ndio maana wakaamua kuwa wazi bila hivyo............Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ametoa ripoti ya matukio kadhaa ikiwemo lililohusisha wizi wa zaidi ya Shilingi Bilioni mbili mkoani humo.
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000= mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED ambapo wakala wa Selcom aitwaye TYSON KASISI wa mkoani Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda nambari mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki.
Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya tarehe 9 Novemba 2021 hadi 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo TYSON KASISI kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.
Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho cha TSh 2,129,856,000=.
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000= kutoka kwa watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.
Aidha, kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783= zimezuiliwa katika moja ya benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.
Upelelezi uliofanyika mpaka sasa umebaini kuwa genge la uhalifu na wizi wa fedha za Selcom uliongozwa na watu watatu ambao ni TYSON KASISI, PATRICK CHALAMILA na EVARISTO CHALAMILA ambao wamebainika kuwa wanufaika wakuu wa uhalifu huo.
Halikadhalika, mali ambazo ni mazalia ya uhalifu zimekamatwa na kuhifadhiwa ikiwa ni magari manne (4) yenye thamani ya TSh 303,000,000= ambayo ni;
i. SCANIA yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 128, 000,000=.
ii. MITSUBISH FUSO usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 75,000,000=.
iii. TOYOTA HARRIER usajili namba T 719 DXX yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 72,000,000=.
iv. NISSAN JUKE usajili namba T 605 DXV yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 28,000,000=.
Pia imekamatwa gari Toyota IST yenye namba za usajili T 576 DRN mali ya PATRICK CHALAMILA lililotumika kufanikisha uhalifu kwa kusafirisha fedha za wizi kutoka Madibira Wilayani Mbarali na Ilula Wilayani Kilolo kwenda kuzificha Kilombero mkoani Morogoro.
Ushahidi uliokusanywa mpaka sasa umetosha kuwafikisha watuhumiwa kumi (10) Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa makosa ya Kuongoza Genge la Uhalifu na Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu.
Umeona like yangu hukoWangemshirikisha mchagga hata mmoja kwenye dili lao wasingekamatwa [emoji16]
[emoji23][emoji23][emoji134]Aisee!..
Labda new model aiseeHarrier 72M
Model mpya hyooo achana na tako la nyaniKumbe harrier zimepanda bei. Milioni 72 sio mchezo
Harrier 72M
Hatari sana.[emoji23][emoji23][emoji134]