Iringa: Wakala wa malipo anaswa akidaiwa kuiba TSh Bilioni 2.1, Polisi wafanikiwa kuokoa TSh Milioni 956

Wamefanya makosa mengi, Kuhamisha kwenda benki, hilo kosa la Kwanza, kujihamishia kwenda kwenye namba zao binafsi, ilitakiwa kabisa wakishapiga hivo kwanza wanazipoza wanaziweka kwenye bitcoin wallet zoote, kule amna udubwasha zinakua safe na private kabisa.
Wangetafta mchaga mmoja hapo wangewin deal. [emoji16][emoji16]
Na hizo Benki nazo tatizo.
Kijana umeajiriwa juzijuzi tu leo uko kwenye kesi ya kutakatisha fedha!
Vijana acheni tamaa. Angalia mbele kwanza na ujiulize: "Hivi dili hii ikigalambuka itakuwaje?"
Show-off mbaya sana na ndiyo inayoponza vijana!
 
Ilula sokoni, ilula mtua, ilula mwaya, ilula itunda, ilula masukazi wanalima nyanya hawa jamaa utakutaga mafuso yamepakia nyanya hasa kipind Cha mwenz wa nne hadi wa Saba
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ametoa ripoti ya matukio kadhaa ikiwemo lililohusisha wizi wa zaidi ya Shilingi Bilioni mbili mkoani humo.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000= mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED ambapo wakala wa Selcom aitwaye TYSON KASISI wa mkoani Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda nambari mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki.

Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya tarehe 9 Novemba 2021 hadi 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo TYSON KASISI kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.

Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho cha TSh 2,129,856,000=.

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000= kutoka kwa watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.

Aidha, kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783= zimezuiliwa katika moja ya benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.

Upelelezi uliofanyika mpaka sasa umebaini kuwa genge la uhalifu na wizi wa fedha za Selcom uliongozwa na watu watatu ambao ni TYSON KASISI, PATRICK CHALAMILA na EVARISTO CHALAMILA ambao wamebainika kuwa wanufaika wakuu wa uhalifu huo.

Halikadhalika, mali ambazo ni mazalia ya uhalifu zimekamatwa na kuhifadhiwa ikiwa ni magari manne (4) yenye thamani ya TSh 303,000,000= ambayo ni;

i. SCANIA yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 128, 000,000=.

ii. MITSUBISH FUSO usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 75,000,000=.

iii. TOYOTA HARRIER usajili namba T 719 DXX yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 72,000,000=.

iv. NISSAN JUKE usajili namba T 605 DXV yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 28,000,000=.

Pia imekamatwa gari Toyota IST yenye namba za usajili T 576 DRN mali ya PATRICK CHALAMILA lililotumika kufanikisha uhalifu kwa kusafirisha fedha za wizi kutoka Madibira Wilayani Mbarali na Ilula Wilayani Kilolo kwenda kuzificha Kilombero mkoani Morogoro.

Ushahidi uliokusanywa mpaka sasa umetosha kuwafikisha watuhumiwa kumi (10) Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa makosa ya Kuongoza Genge la Uhalifu na Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu.

Kumbe harrier zimepanda bei. Milioni 72 sio mchezo
 
Wamefanya makosa mengi, Kuhamisha kwenda benki, hilo kosa la Kwanza, kujihamishia kwenda kwenye namba zao binafsi, ilitakiwa kabisa wakishapiga hivo kwanza wanazipoza wanaziweka kwenye bitcoin wallet zoote, kule amna udubwasha zinakua safe na private kabisa.
Wangetafta mchaga mmoja hapo wangewin deal. [emoji16][emoji16]
Acha uongo!

Utahamishaje pesa zote hizo kwenda e-wallet bila kupitia mfumo rasmi wa kifedha (bank/mobile money transfer).

Fedha yoyote kwenda account ya nje lazima ipite BoT.

Pale ukipita mzigo mrefu lazima wapate red alarm. Wanazuia
 
Haha sio uongo mzeee, Means utakua na line fake kama zotee, Ukishajihamishia mzigo, unaingia kwenye simu yako alafu unanunua local bitcoins Hapo inakua imeisha
 
Niliwahi kukuambia huna akili, hiyo harrier kweye picha unaweza kununua kwa sh ngapi?
20220211_133946.jpg
 
Kama puto, hiyo bei ya 72m kwa Harrier, hiyo bei imepigwa juu kwajuu!
Utakua unaishi kijijini na huna elimu, thamani ya gari huendana na mwaka uliotengenezwa(model)
Harrier zipo za mil 15, 25, 40, 70, 80 , 120, 150, 170
Ni wewe tu unataka ipi.
Bei ya harrier ya 2020 unataka ifanane na harrier ya 2006 mnayoiita tako la nyani?
Hiyo harrier ipo hapo chini unahisi ni sh.ngap?
20220211_133946.jpg
 
Kuna shehe mmoja kwenye kijiwe cha gahwa alipata kusema, "matanzania yote ni majizi bila kujali kabila zao".
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan L. Bukumbi ametoa ripoti ya matukio kadhaa ikiwemo lililohusisha wizi wa zaidi ya Shilingi Bilioni mbili mkoani humo.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa linafanya Uchunguzi/Upelelezi dhidi ya watuhumiwa wa wizi wa fedha za kitanzania kiasi cha TSh 2,129,856,000= mali ya kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED ambapo wakala wa Selcom aitwaye TYSON KASISI wa mkoani Iringa kupitia huduma ya ‘Selcom Pay’ isivyo halali alihamisha fedha kwenda nambari mbalimbali za simu na kisha kuchukuliwa taslimu kupitia wakala wa huduma za kifedha za mitandao mbalimbali ya simu pamoja na akaunti za Benki.

Wizi wa fedha hizo ulifanyika kwa njia ya mtandao katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa, Dar es Salaam na Morogoro kati ya tarehe 9 Novemba 2021 hadi 27 Novemba 2021 baada ya wakala huyo TYSON KASISI kufanikiwa kuchezea mfumo wa kieletroniki wa ‘Selcom Pay’ unaomilikiwa na Kampuni ya SELCOM PAYTECH LIMITED.

Wakala huyo kwa njia ya udanganyifu alianza kujitumia fedha pamoja na kuwatumia watu wengine na kwa kushirikiana na genge lake la uhalifu walifanikiwa kuiba kiasi hicho cha TSh 2,129,856,000=.

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata (Kuokoa) fedha taslimu kiasi cha TSh 956,974,000= kutoka kwa watuhumiwa na washiriki wa uhalifu huo ambao walipokea sehemu ya fedha hizo kwa ajili ya kuzificha katika maeneo mbalimbali ikiwemo makazi na shambani.

Aidha, kiasi cha fedha za kitanzania TSh 121,215,783= zimezuiliwa katika moja ya benki za biashara mkoani Iringa ikiwa ni mazalia ya uhalifu.

Upelelezi uliofanyika mpaka sasa umebaini kuwa genge la uhalifu na wizi wa fedha za Selcom uliongozwa na watu watatu ambao ni TYSON KASISI, PATRICK CHALAMILA na EVARISTO CHALAMILA ambao wamebainika kuwa wanufaika wakuu wa uhalifu huo.

Halikadhalika, mali ambazo ni mazalia ya uhalifu zimekamatwa na kuhifadhiwa ikiwa ni magari manne (4) yenye thamani ya TSh 303,000,000= ambayo ni;

i. SCANIA yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 128, 000,000=.

ii. MITSUBISH FUSO usajili namba T 796 DXV yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 75,000,000=.

iii. TOYOTA HARRIER usajili namba T 719 DXX yenye jina la mtuhumiwa TYSON KASISI kwa thamani ya Sh 72,000,000=.

iv. NISSAN JUKE usajili namba T 605 DXV yenye jina la mtuhumiwa PATRICK CHALAMILA kwa thamani ya Sh 28,000,000=.

Pia imekamatwa gari Toyota IST yenye namba za usajili T 576 DRN mali ya PATRICK CHALAMILA lililotumika kufanikisha uhalifu kwa kusafirisha fedha za wizi kutoka Madibira Wilayani Mbarali na Ilula Wilayani Kilolo kwenda kuzificha Kilombero mkoani Morogoro.

Ushahidi uliokusanywa mpaka sasa umetosha kuwafikisha watuhumiwa kumi (10) Mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kwa makosa ya Kuongoza Genge la Uhalifu na Kujipatia Fedha kwa njia ya Udanganyifu.

Huenda hao polisi lile la ntwara limewashtua ndio maana wakaamua kuwa wazi bila hivyo............
Naomba niishie hapo
 
Back
Top Bottom