Islam’s role in Tanzania’s freedom struggle

Kumbe ilikuwa hoja yako mbona ulikuwa anawasingizia Waislam hawana akili wanajadili barabara wakati wenye akili wanadali maendeleo.
Kilete kifungu kizima uthibitishe maneno yako.
Hata hivyo hiyo isiwe njia ya kutokea maana naona maji mazito hali ngumu sasa ni shoot any moving object.

Tubaki katika mada ya namna ya kwaenzi akina mshume na wenzake. Nini kifanyike na mnashauri nini.
 
Bandiko lako ili hapa jisome, unafurahisha sana anaandika mwenyewe kisha unajisifia mara maji mazito teh teh teh mimi naweza kukaa peke yangu kwenye huu uzi hata mwezi naweka mapandiko yako ya Chadema.
 
Last edited by a moderator:
Hapana wametaka kujua kwani kulikoni? Kilichowashtua ni mvua ya matusi wakauliza hoja gani inagomba? Nikawashauri wasome nyuzi vema.
Wanaogopa kuja kwasababu hawana uzoefu wa matusi wala roho ngumu ya kupokea.

Lipi geni kwao hata wakaogopa hayo unayoita matusi?
 
Nguruvi3, mtu yoyote akisoma hilo bandiko lako ataona chuki zako za wazi dhidi ya Waislam na Uslam.

Matusi na kashfa ulizoandika zimekushusha sana nakushauri pambana na CCM siyo Uislam.

Uislam kwangu ni kama mchoro wa jengo uliorembwa vizuri. Sehemu zake zote zinaonekana kushikanb na kutegemeana vizuri, hakuna kilichopungua, na hii ni matokeo ya mpangilio bora na makini.

Wewe na Chadema wenzako mnapoteza muda wenu bure kupambana na Uislam.
 
Last edited by a moderator:
Angalia ulivyokuwa mnafiki eti tubaki kwenye mada ya kuwaenzi Mshume na wenzake, wakati unamtaja Mshume kwenye bandiko lako kuwa madai ya Waislam ni majina ya barabara nani alikutuma kuwasemea Waislam?
 

Ndugu usiwe na shaka data sio tatizo nitazileta tu na wala sio tatizo kwangu kuhakiki kwa sababu nimeshafanya hivyo kwa kuangalia vyanzo rasmi kama Taasisi ya Takwimu ya Taifa, na kuangalia orodha ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na TCU na kumbukumbu nyinginezo katika maduka ya vitabu vya serikali na kote huko sijaona takwimu zinazoshabihiana na zako.

Lakini kwa kuzingatia kwamba hapa wewe ndio ulioleta hizo takwimu za vyuo vikuu vya umma 25, kwa faida ya wasomaji wengine ingekuwa vema ukachukua muda kidogo tu ukabadilisha hiyo namba kwa kuorodhesha majina ya vyuo kwa kuwa tayari unayo idadi ina maana unavifahamu.

Pili Umesema umechagua Baraza la mitihani kama mfano kwa sababu ya unyeti wake na kigezo kingine kilichopelekea uchague baraza la mitihani ni kwamba Baraza hilo halijawahi kuongozwa na Muislam.

Tukiangalia utendaji wa baraza la mitihani lipo chini ya wizara ya elimu. Na hili halijawahi kubadilika tangu tupate uhuru hadi leo.

Mkurugenzi wa idara hii ki-utumishi anawajibika kwa katibu mkuu wa wizara. Hata mipango yote ya baraza haiwezi kutekelezwa bila baraka za katibu wa wizara pamoja na waziri wa elimu.

Kwa maana nyingine ni kwamba mkurugenzi wa baraza la mitihani ni sehemu tu ya wakurugenzi wengine wa wizara ya elimu na wala hana kauli ya mwisho katika mambo ya mitihani. Ndio maana wizara ilipoamua kuchakachua mitihani ya kidato cha nne hakuwa na ubavu wowote wa kupinga kulingana na muundo mbovu wa wizara na utataratibu mbovu wa nchi yetu na viongozi wengi wa sasa kutoheshimu sheria inayounda Baraza la mitihani

Waziri wa elimu ndio kiongozi mkuu wa sera ya elimu ambayo inatekelezwa na baraza la mitihani.

Kwa vile mkurugenzi ni mtekelezaji tu (executive) wa maelekezo na sera za wizara kuhusu elimu na mitihani inashangaza unaposema kwa ujasiri kwamba chombo hicho hakijawahi kuongozwa na muislam.

Sasa tukirejea historia ya wizara husika miongoni mwa viongozi maarufu waislam waliopata kuongoza wizara ya elimu ni pamoja Kighoma Malima na Athumani Kapuya. Hawa walikuwa viongozi wa wizara ya elimu wakiwa tayari ni maprofesa na Profesa maana yake anao upeo wa juu kabisa katika maswala yahusuyo taaluma. Kwa hiyo wao kipindi chote hicho walichoongoza wizara hiyo hawakuona tatizo ambalo nyie mmeliona sasa.

Pia hivi karibuni kabla ya mabadiliko waziri na katibu mkuu wa wizara ya elimu wote walikuwa ni waislam. Na matokeo ya shule za kiislam yamekuwa mabovu tangu enzi hizo za kina Malima na yamekuwa mabaya zaidi mwaka jana ambapo Viongozi wakuu wa wizara ya elimu wote ni waislam (katibu mkuu na waziri).

Ni vema kufahamu kwamba hata kama mtendaji wa baraza akiwa muislam bado hatawafanyia mitihani watoto wa kiislam na haitatungwa mitihani maalum ya waislam ili wafaulu. Hata wakifaulishwa kwa udanganyifu watapata vyeti lakini hawatapata elimu inayohitajika kuwasaidia kutatua changamoto zinazowazunguka, sana sana watakaa kusubiri ofa nyingine tena kwa sababu wameshajengewa fikra tegemezi badala ya kutumia vichwa vyao.

Hawa viongozi lukuki waislamu waliopo madarakani sasa wamewasaidia nini waislamu makabwela?.
Tuchukue Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara kama mfano ambako asilimia kubwa viongozi wake ni waislam, mahospitalini ukienda mwananyamala temeke muhimbili n.k wajawazito waislam na wasio waislam wote wamelala chini. Ukienda mikoa ya kusini hospitali za serikali ziko hoi, wengi wanategemea huduma za hospitali za makanisa.

Shule nyingi za umma watoto wanakaa chini wakiwemo waislam, shule zilizo chini ya taasisi za kiislam na zile za umma katika mikoa hiyo ndizo zilizo na matokeo mabaya zaidi.

Mikoa hiyo ndio inaongoza kwa watoto kupata mimba katika umri mdogo, kuolewa na kuacha shule. Watoto wanatoroka shule au wanafika shule kwa kuchelewa na hakuna mzazi anayeshtuka kufuatilia mtoto wake amejifunza nini, ila wanatarajia malaika atawashushia majibu siku ya mitihani wafaulu.

Wakifeli wanajua kuna sehemu ya kupeleka lawama, mfumo kristo wa baraza la mitihani na Mkurugenzi wake.

Hizo siasa za misikitini zinatumika kama madaraja na vichaka tu, wakishawatumia wanawatupilia mbali kama kondomu.

Mfano halisi ni huu: Mgombea wa urais muislam na makamu wake muislam walitembea nchi nzima wakiwalaghai muwachague ili wawape mahakama ya kadhi huku wakijua katiba ya nchi hairuhusu kitu kama hicho. Walipopata madaraka hayo wamewapeni hiyo mahakama?.

Mwisho narudia kusisitiza acheni kuwadanganya wenzenu na kuwaangamiza.

Wanaoshabikia na kueneza sumu kwa watoto wa maskini watoto wao wapo shule nzuri tu wala hutawakuta shule kama Jabal-Hilal.


Kwa kukumbusha tu ni kwamba, Tangu Julius anga'atuke ni miaka 28 sasa imepita. Katika kipindi hicho marais waislam wameongoza mika 18 hadi sasa na katika kipindi cha miaka 28 kumekuwa na makamu wa rais waislam kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20.

Kwa kuzingatia mamlaka ya uteuzi aliyonayo rais ni wazi kwamba wengi kati ya uliyowataja (iwapo tutakubaliana na takwimu zako) wengi wao wameteuliwa na marais waislam.

Huo mfumo kristo unajengwa na waislam?.

Tafakari chukua hatua.

Mtu Mzima
 
Last edited by a moderator:
"Islami's role in Tanzania's freedom struggle" ndiyo hoja iliyopo mbele. Wewe kwenye bandiko lako si umeishasema wenye akili wanajadili maendelo wengine wanajadili kuwapa majina za barabara watu wao!
 
Last edited by a moderator:
I think you would have posted "Islam's role in killing people in the name of their God and get gifted 72 virgins"
so you mean, they are craving for virgin enchantress/goddess:amen:. ha ha ha ha

with respect of freedom of speech, i think we all aware of our differences and similarities in perception. i'm personally neither fan of Nyerere nor his predecessors. but with all due respect, we are all aware of popularity and reputation which Nyerere gained, that made him the father of this nation, who fight against all inequalities and has successful unite Tanzanians. so our freedom of thinking will be in jeopardy if we allow few people who carrying bad intentions to brainwash us through perpetuating their irrational and narrow minded thought against the father of the nation.
 
Eid Mubarak Polite, nakutakia heri ili ufunguke macho na ufuate imani yako vema. Ritz kasema Uislam ni mfumo mzima wa maisha, je hayo uliyoandika ndio yanawakilisha mfumo huo?


minalfaidhina.ndo naingia jf xaxa.

ndio.hayo niliyoandika ndo yanawakilisha mfumo huo.kupinga uongo na dhulma.

biblia inasema wapumbavu tuwakatae huo ni mfumo wa wakristu.

unastajabu nilichoandika wakati biblia unayo mkononi.

mabubu viziwi na vipofu hawatorejea= quran 2

Wewe ni bubu kiziwi na kipofu.
 
Last edited by a moderator:

Vipi unashauri ukoo wa Mshume Kiyate ulipwe kwa kumsaidia Julius Nyerere?

Unadhani Mshume Kiyate angekuwa hai angedai malipo?

Au angesimama na kutangaza haya kama ufanyavyo?

Je watanzania tumfanyaje Mshume Kiyate?

Wakati wa uhai wa Mzee Kiyate aliwahi kusimama-hadharani ama mafichoni na kudai fidia/malipo ya kumsaidi Nyerere wakati wa ukombozi?

Unapokuwa mzee halafu ukawa mnafiki na mzandiki unakosa thamani hata kwa Mungu wako
 

ha ha yeye ni bubu kiziwi na kipofu.ni kama kutwanga maji kwenye kinu
 
Last edited by a moderator:
@Ritz hebu onyesha kwa dhati matusi na kashfa dhidi ya imani. Siku zote msimamo wangu ni kuheshimu kile mtu anachokiamini na wala si kubambikia mtu au kushinikiza kwa namna yoyote. Nasema thibitisha maneno yako kuwa ninachuki na Uislam.

Kama hutaweza kuonyesha tafuta spinning nyingine.

Hoja zinapiga mfupa, nasikitika lakini ndio mnakasha
 

Kijana nilishakuonya huko nyuma!
Unapoongea na wazee wenye elimu kuliko hao unao waheshimu jaribu kuwa na adabu!

Mbona nyie vijana mnakuwa kama watoto wa mitaani?
Au ulilelewa bila baba wewe?
Mnfnssssssssss!

Huna adabu kabisa!
 

Ntakukumbusha msemo mmoja hapa!
Waungwana wanasema! AFANYAE DHULMA ADUI ! LKN ATETEAE DHULMA NI ADUI NA DHALIM!

Wewe jamaa yetu juu ya dhulma iliyofanyika miaka hio na inayo endelea kuhusu hawa waungwana na huyo swahiba yako Nyerere! SI TU UMESHINDWA KUIKEMEA BALI UNAITETEA NA KUJARIBU KULETA MANENO YA FEDHEHA NA KEJELI!
Amma ubaya huu utakudhuru mwenyewe!

Uzi unaongelea ISLAM'S ROLE in Tanzania freedom!

Sasa kama huyo MSHUTE ALIKUWA PART OF ISLAM anaweza kujadiliwa pamoja na wale mashujaa wengine!

La! Kama sio, wewe na wenzako kumtaja hapa ni KUJARIBU KUUHARIBU HUU UZI! na kupoteza lengo lote la mnakasha huu.

Hamtaki kukubali yale waliofanyiwa hao tuliowataja mbeleni . Mnamuingiza Mshute!!.

Grow up! Usimwige yule mzee wa butiama kuwa na tabia ya sura nyingi!

Kama unakereheka na hili basi anzisha uzi wako wenye TITLE INGINE.


THIS thread remains' as:-

ISLAM'S ROLE IN TANZANIA FREEDOM STRUGGLE.
 
Last edited by a moderator:

Wewe ni ktk wale fisi waliovaa ngozi ya mbuzi!
Unashusha thamani yako kwa bei ndoogo kabisa! Huna aibu kutetea dhulma wewe?
Halafu tuseme wewe na huyo nyerere ni tumbo moja! Iweje wewe unatumia maneno kama " inshallah" Mwenyezi Mungu" na mengi yatumiwayo na waungwana bila hata HAYA KIDOGO??
Hata yule maluun wa taifa hakufikia kusema inshallah!! We umepitiliza!

Unasingizia kuwa eti sisi tunataka mitaa ibadilishwe hali ukisisitiza tujenge hoja!
Mtu mzima huna aibu? Wapi ktk jukwaa hili umeskia mimi au shariff Ritz au maulana gombesugu au al akhiy Tayeb au maalim CHAMVIGA na ustaadh Boko haram na waungwana wengi tumesema hayo unayo tutilia midomoni kwetu??
Hebu onyesha hapa kama wewe si ktk wale majahill wanao tetea dhulma!
Halafu ukiambiwa wewe ni munafiq unasema unatukanwa!
Sasa labd tukae kimya! Manake kukwambia uyatayo wewe haiwezekani!!
 
Last edited by a moderator:
Religion is the Opium of the masses ~Karl Max

The problem of copy and paste sometime could bit your back!
So pinno what you said here! What is got to do with what we are discussing here!!?

Au ndio nyie mnaodandia treni kwa mbele!

I wonder!!
 
Last edited by a moderator:

Haya maswali unatakiwa uwatatfute ukoo wa mzee Kiyate uwaulize wao!

Mzee Mohamed Said alichofanya ni kukuwekea wewe na hao wenzako chakula juu ya meza!
Wewe unataka bado akulishe??
Ajabu!

Hio Ndio tunaiita ihsani ya punda! Ni teke la utupu!

Cc Manundu 1
 
Last edited by a moderator:
Wrong! dear Daktari.
Please read the following synopsis on same thread. Katika habari iliyopo Mzee Mshume Kiyate ametajwa mara 6 na ndiye aliyetajwa mara nyingi kuliko watu wote katika thread.
kahtaan, si mimi ninaye mtaja ni thread inamtaja na kumpa hadhi.
Mohaemd Said ameleta picha na maelezo ya Mshume Kiyate kuthibitisha umuhimu wake katika nyuzi.

U
muhimu zaidi ni pale alipotajwa kama mentor wa Nyerere the young leader ambaye hukuwa acknowledged.
Kiyate ametajwa miongoni mwa watu wasiojulikana leo hii(maandishi mekundu)
Mzee mshume ametajwa kufariki akiwa mwenyewe na masikini.

Kwa mantiki hiyo mimi kumtaja mzee Kiyate si kejeli kama ni kejeli basi aliyeanzisha ni Mohamed Said kama nilivyomnukuu hapo juu na mara ngapi amemtaja.

Hoja ya pili, nina sababu za msingi kuhoji kuwa ni vipi tuwaenzi wazee hawa.
Swali hilo kauliza chamvinga na Mohamed Said. Ukisoma nukuu hapo juu Mohamed Said amesema maneno yanayohitaji watu hawa kuenziwa.

Kama unadhani mimi kuuliza ni karaha basi Mohamed Said akane maneno yake na chamvinga aombe radhi nami nitakuwa wa mwisho kwasababu ni wa mwisho kutumia na kuuliza swali yale yale yalioulizwa na wenzenu.

Kwa muktadha huo SWALI LA NI KWA NJIA GANI ninyi mnapendekeza wazee hao waenziwe linabaki na umuhimu wake. Hoja ya kusema title ni Islam's role ni njia ya kukwepa msumari mzito unaowakabili.

Tatu, hata unaposema title ni Islam's role in Tanzania's freedom struggle bado kuna utata.
Mohamed Said mwenye maandiko amesema hapo mwisho '....history of nationalism in Tanzania' akimaanisha historia ya utaifaTanzania.

Ukinisoma vizuri nimeepuka sana kusema historia ya imani fulani kwasababu ninasoma between the lines, ninaelewa ninasoma nini na kina maana gani kwasababu zipi.

Swali langu limekuwa vipi tuwaenzi wazee hawa. Sijasema tuwaenzi wazee hawa wa imani fulani.
Nafahamu mwisho wa maadishi Mwandishi Mohamed alikusudia nini.

Utaweza kuelewa kama mimi ukiacha jazba, ushabiki. Ukitanguliza fikra zaidi ya mitusi.
Hili ndugu Daktari ninaona aibu lakini sinabudi kukuambia off point you have no ground to stand.

Mwisho sipo hapa kumpendeza mtu, sipo hapa kupongezana nipo hapa kueleza maoni yangu kama mtu huru.

Uzi umekuja na tunautendea haki, kama kukupa facts ni kuharibu uzi, guess what I'm here to stay.
I will stand toe to toe with contender not pretender. If you can take the heat get out kitchen.

Daktari mjulie hali ahli na familia, hakika sisi hatujambo.

Maslaam
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…