Mtu Mzima kama nilivyo sema mwanzo wa malumbano haya! Mimi hupenda kuja na takwimu ambazo zina ushahidi.
Sasa unaposema ziko idara nyingine NYETI KAMA HII YA ELIMU ILIYO ONGOZWA NA WAISLAMU MIAKA MIINGI! BASI NINGEFURAHI KAMA UTALETA HIZO TAKWIMU HAPA!
Kuhusu mimi kuchagua wizara ya ELIMU!
Nimechagua kukuonyesha data za wizara hii kwa sababu HAKUNA WIZARA MUHIMU KTK NCHI YYT DUNIA KAMA WIZARA YA ELIMU!
Sasa ukija hapa na data za wizara ya mifugo au maendeleo vijijini au wizara ya mipango miji Sidhani kama utaweza kulinganisha hatta kidogo na wizara hii.
Kama nilivyoonya mwanzo kuwa wasio kuwa na ufahamu mara zote hukimbilia kusema waislamu hawakusoma kwa sababu 1.2.3.4 na kuendelea! Na hilo umelisema hapo juu! Halafu hapo hapo unasema kulikuwa na wasomi wengi tu wa kiislamu ambao walikuwapo wakati huo na ukauliza ni kwanini wao wasiliandike hilo alilo litamka nyerere?
Umeuliza kuhusu idadi ya vyuo! Kuliko mimi kuanza kukuorodheshea kimoja kimoja! Kwa nini wewe usiende kuhakiki mwenyewe kuhusu hizi data nilozo kupa??
La mwisho. Ili kukuonyesha kuwa si waislami pekee wenye kufahamu udhalimu wa Nyerere na serikali yake wakati huo!
Hebu pitia kidogo hii link hapa chini.
Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy -
Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy
Ludovick Mwijage: The Dark Side of Nyerere's Legacy
Cc
gombesugu
Ndugu usiwe na shaka data sio tatizo nitazileta tu na wala sio tatizo kwangu kuhakiki kwa sababu nimeshafanya hivyo kwa kuangalia vyanzo rasmi kama Taasisi ya Takwimu ya Taifa, na kuangalia orodha ya vyuo vikuu vilivyosajiliwa na TCU na kumbukumbu nyinginezo katika maduka ya vitabu vya serikali na kote huko sijaona takwimu zinazoshabihiana na zako.
Lakini kwa kuzingatia kwamba hapa wewe ndio ulioleta hizo takwimu za vyuo vikuu vya umma 25, kwa faida ya wasomaji wengine ingekuwa vema ukachukua muda kidogo tu ukabadilisha hiyo namba kwa kuorodhesha majina ya vyuo kwa kuwa tayari unayo idadi ina maana unavifahamu.
Pili Umesema umechagua Baraza la mitihani kama mfano kwa sababu ya unyeti wake na kigezo kingine kilichopelekea uchague baraza la mitihani ni kwamba Baraza hilo halijawahi kuongozwa na Muislam.
Tukiangalia utendaji wa baraza la mitihani lipo chini ya wizara ya elimu. Na hili halijawahi kubadilika tangu tupate uhuru hadi leo.
Mkurugenzi wa idara hii ki-utumishi anawajibika kwa katibu mkuu wa wizara. Hata mipango yote ya baraza haiwezi kutekelezwa bila baraka za katibu wa wizara pamoja na waziri wa elimu.
Kwa maana nyingine ni kwamba mkurugenzi wa baraza la mitihani ni sehemu tu ya wakurugenzi wengine wa wizara ya elimu na wala hana kauli ya mwisho katika mambo ya mitihani. Ndio maana wizara ilipoamua kuchakachua mitihani ya kidato cha nne hakuwa na ubavu wowote wa kupinga kulingana na muundo mbovu wa wizara na utataratibu mbovu wa nchi yetu na viongozi wengi wa sasa kutoheshimu sheria inayounda Baraza la mitihani
Waziri wa elimu ndio kiongozi mkuu wa sera ya elimu ambayo inatekelezwa na baraza la mitihani.
Kwa vile mkurugenzi ni mtekelezaji tu (executive) wa maelekezo na sera za wizara kuhusu elimu na mitihani inashangaza unaposema kwa ujasiri kwamba chombo hicho hakijawahi kuongozwa na muislam.
Sasa tukirejea historia ya wizara husika miongoni mwa viongozi maarufu waislam waliopata kuongoza wizara ya elimu ni pamoja Kighoma Malima na Athumani Kapuya. Hawa walikuwa viongozi wa wizara ya elimu wakiwa tayari ni maprofesa na Profesa maana yake anao upeo wa juu kabisa katika maswala yahusuyo taaluma. Kwa hiyo wao kipindi chote hicho walichoongoza wizara hiyo hawakuona tatizo ambalo nyie mmeliona sasa.
Pia hivi karibuni kabla ya mabadiliko waziri na katibu mkuu wa wizara ya elimu wote walikuwa ni waislam. Na matokeo ya shule za kiislam yamekuwa mabovu tangu enzi hizo za kina Malima na yamekuwa mabaya zaidi mwaka jana ambapo Viongozi wakuu wa wizara ya elimu wote ni waislam (katibu mkuu na waziri).
Ni vema kufahamu kwamba hata kama mtendaji wa baraza akiwa muislam bado hatawafanyia mitihani watoto wa kiislam na haitatungwa mitihani maalum ya waislam ili wafaulu. Hata wakifaulishwa kwa udanganyifu watapata vyeti lakini hawatapata elimu inayohitajika kuwasaidia kutatua changamoto zinazowazunguka, sana sana watakaa kusubiri ofa nyingine tena kwa sababu wameshajengewa fikra tegemezi badala ya kutumia vichwa vyao.
Hawa viongozi lukuki waislamu waliopo madarakani sasa wamewasaidia nini waislamu makabwela?.
Tuchukue Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara kama mfano ambako asilimia kubwa viongozi wake ni waislam, mahospitalini ukienda mwananyamala temeke muhimbili n.k wajawazito waislam na wasio waislam wote wamelala chini. Ukienda mikoa ya kusini hospitali za serikali ziko hoi, wengi wanategemea huduma za hospitali za makanisa.
Shule nyingi za umma watoto wanakaa chini wakiwemo waislam, shule zilizo chini ya taasisi za kiislam na zile za umma katika mikoa hiyo ndizo zilizo na matokeo mabaya zaidi.
Mikoa hiyo ndio inaongoza kwa watoto kupata mimba katika umri mdogo, kuolewa na kuacha shule. Watoto wanatoroka shule au wanafika shule kwa kuchelewa na hakuna mzazi anayeshtuka kufuatilia mtoto wake amejifunza nini, ila wanatarajia malaika atawashushia majibu siku ya mitihani wafaulu.
Wakifeli wanajua kuna sehemu ya kupeleka lawama, mfumo kristo wa baraza la mitihani na Mkurugenzi wake.
Hizo siasa za misikitini zinatumika kama madaraja na vichaka tu, wakishawatumia wanawatupilia mbali kama kondomu.
Mfano halisi ni huu: Mgombea wa urais muislam na makamu wake muislam walitembea nchi nzima wakiwalaghai muwachague ili wawape mahakama ya kadhi huku wakijua katiba ya nchi hairuhusu kitu kama hicho. Walipopata madaraka hayo wamewapeni hiyo mahakama?.
Mwisho narudia kusisitiza acheni kuwadanganya wenzenu na kuwaangamiza.
Wanaoshabikia na kueneza sumu kwa watoto wa maskini watoto wao wapo shule nzuri tu wala hutawakuta shule kama Jabal-Hilal.
Kwa kukumbusha tu ni kwamba, Tangu Julius anga'atuke ni miaka 28 sasa imepita. Katika kipindi hicho marais waislam wameongoza mika 18 hadi sasa na katika kipindi cha miaka 28 kumekuwa na makamu wa rais waislam kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20.
Kwa kuzingatia mamlaka ya uteuzi aliyonayo rais ni wazi kwamba wengi kati ya uliyowataja (iwapo tutakubaliana na takwimu zako) wengi wao wameteuliwa na marais waislam.
Huo mfumo kristo unajengwa na waislam?.
Tafakari chukua hatua.
Mtu Mzima