Maalim
Mohamed Said, naomba mualiko huu kwa
Mag3 niusambaze pia kwa
Nguruvi3,
Yericko Nyerere,
Mzee Mwanakijiji na wenzao wote, mjumuike mtupatie historia ya
Cecil Matola zaidi ya tuijuayo kutoka kwa Maalim
Mohamed Said.
Thanks in advance.
Asante
FaizaFoxy, mimi siye mwana historia na si mwandishi by profession na muda kusema kweli ni tatizo kubwa kwangu...hata hivyo kabla sijajibu swali lako ningependa ufahamu kuwa wengi wa vijana wasomi wa mwanzoni mwa miaka ya 1920 kuendelea walikuwa ni wahitimu wa shule maarufu iliyoitwa
Kiungani kisiwani Zanzibar. Mwaka
1866 dhehebu la Kikristo,
UMCA, lilinunua sehemu ya ardhi nje kidogo ya mji wa Zanzibar na kujenga hosteli kubwa katika juhudi zao za kuwapa hifadhi wahanga wa Utumwa. Baada ya miaka saba,
1873 walijenga Kanisa lao la kwanza mjini Zanzibar lililojulikana kama
Christ Church Cathedral na kufungua kituo cha afya mwaka
1877 ambacho kiliweza kuwa hospitali kamili mwaka
1893.
UMCA ilianzisha shule Kiungani iliyojulikana kama
St. Andrew's College, U.M.C.A. lakini baadaye kwa sababu mbalimbali ilibidi wahamie bara kama inavyosimuliwa hapa;
Minakischool.blogspot.com said:
Since 1869 the Anglican Missionaries established St. Andrew's College at Kiungani, Zanzibar for the main purpose of getting Christian converts by 1920 they had failed completely. The church had failed in getting converts and students to join their school.When the first world war broke out in 1914 there were a total of 80 students at kiungani of which 9 were came from Zanzibar and 71 from Mainland. The war broke during the holiday so all 71 students from the main land failed to return to school so only 9 student remained. This failure forced the missionaries to consider closing the school in Zanzibar and moving it to the mainland where most of the students originated. Official opening of the school St Andrews College, Minaki was conducted by the colonial governor, Sir Dolnald Cameron on 5th December 1925.
Kwa nini nasimulia haya? Ni kwa sababu ukitaka kuwajua watu ambao ungeweza kuwaita "elite" wa mji wa Dar es Salaam kwa nyakati hizo, wasomi wa wakati huo wanachukua daraja la kwanza.
Cecil Matola alikuwa ni moja wa alumni wa Kiungani na Mwalimu Mwandamizi katika shule ya serikali mjini Dar es Salaam. Wahitimu wa Kiungani walijulikana ndani na nje ya nchi na kulingana na simulizi za
John Iliffe ambayo
Mohamed Said anazinukuu kila mara, nanukuu;
Cecil Matola was a senior African Teacher at the Dar es Salaam School which made him almost an ex officio leader of the capital's educated Africans. Nyakati hizo Ualimu ulikuwa ni profession yenye heshima kubwa katika jamii na haikuwa ajabu kwa mtu maarufu kama
Cecil Matola kuchaguliwa kuwa
Raisi wa kwanza African Association mwaka
1929.
African Association ilianzishwa kwa baraka za aliyekuwa Gavana wa Tanganyika
David Cameron na mkutano wake wa kwanza ulifanyika nyumbani kwa Raisi wake muasisi
Cecil Matola. Hii ilifanyika kwa sababu tatu; kwanza hapakuwepo na klabu ama nyumba iliyotosheleza kama ya Cecil Matola, pili hakuwepo mtu aliyeheshimika kama yeye na tatu
Cecil Matola alikuwa
Mtanganyika halisi, Myao. Mpaka anakuwa Raisi wa AA, alishafanya kazi sehemu mbali mbali ndani na nje ya Tanganyika na kukutana na wasomi mbalimbali wenye mawazo mapya. Sababu kuu ya
Mohamed Said kutotaka kujua historia ya
Cecil Matola ni kwamba inawaweka wazee wake mamluki wa Kimanyema, Kizulu na Kinubi pakavu. Watu mamluki waliopigana vita dhidi ya Watanganyika wakiwa upande wa Mkoloni eti ndio waongoze harakati dhidi ya mkoloni, wapi na wapi!
Chama cha kwanza kabisa cha wasomi na kilichowakutanisha Waafrika, wafanyakazi na wafanya biashara, kilianzishwa mjini Tanga na Mtanganyika wa kwanza mhitimu wa Kiungani Zanzibar aliyekuwa na cheo cha juu kabisa serikalini mwaka 1922,
Martin Kayamba. Kwa bahati mbaya sana
Mohamed Said katika kuhangaikia namna ya kuwakweza wazee wake ambao hawakuwa na uwezo wala sifa za kiuongozi amejikita sana katika kuwachafua wengine. Ikumbukwe maraisi wa
AA, TAA na baadaye
TANU walikuwa ndio wenyeviti na watendaji wakuu wa hivyo vyama lakini kwa
Mohamed Said, maraisi hawa hawakuwa chochote na sifa zote anawapa eti makatibu.
Cecil Matola alikuwa ni
Raisi muasisi na Mtendaji Mkuu wa AA hadi anafariki katika mazingira yasiyoeleweka wakati huo tayari
AA wana nyumba ambayo kiwanja chake walipewa na
Gavana David Cameron mtaa wa
New Street.
Kusema kweli kukosekana kwetu wengine kwenye huu mjadala kunatokana na kukosa muda lakini nina hakika tupo wengi wenye historia inayopingana na hizi hadithi za mtaani za
Mohamed Said...a fellow so obsessed with hatred, so bent on distorting facts and so bent on sowing seeds of discord he will stop at nothing till he accomplishes his evil plans but thank God, that chance he wont get,
not on our watch...we wont allow him or his stooges/cronies.
Mohamed Said hawezi hata kusema ni lini
Mzee Kleist Sykes aliuacha
Ukristo na kuingia
Uislaam, hawezi kusema lini
Chief Kidaha Makwaia aliuacha
Uislaam na kuingia
Ukatoliki na hawezi kuacha kuonesha chuki yake kwa msomi
Martin Kayamba mjukuu wa
Chifu Kimweri Zanyumbai Mfalme wa
Wakilindi waliowatawala Wasambaa na makabila mengi ya Tanga hata kabla ya Wajerumani.
Kwa leo yatosha
FaizaFoxy, ni muda tu unakosekana...
CC:
Nguruvi3