FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Niwia radhi kwa kungia kati ya hii bayana yako kwa mwenzio Mujitahid Wabara.
Nipa fursa ya kuzungumza nawe kiduchu kuhusu hapo nilipo-bold kwenye hiyo bayana yako!?
Yaani nimesoma hiyo bayana yako na kuacha mdomo wazi kabisa! Duh! Khalaf,mtu kama wewe unaweza kujiita ati ndo "msomi" kweli!?
Kutokana na hizo intellectual discrimination/selective views zako(as you seem to discourage historical facts!?),na hizo pia sexist remarks,primitive attitudes...ndo maana nyinyi wengi wenu mnashindwa asilan japo hata kiduchu ku-empathy na madhila na dhuluma wapitiazo wenzenu Waislam. Yaani sasa ndo nazidi kutanabahi,niliposoma hiyo bayana yako!
Bila hata ya kugusia kabisa mambo ya Dini/Imani,lakini embu wewe mwenyewe binafsi jaribu kupitia tena hapo kwenye hiyo bayana yako nilipo-bold!?
Yaani,wewe unashindwa kufahamu kabisa madhila,dhuluma,ubakaji,uporaj i,mauaji ya halaiki,mateso yaso kiasi...ambayo ndugu zetu Wanawake wamepitia tangia enzi za Cain na Abel,na bado yanawakumba mpaka kesho kwenye jamii/nchi nyingi tu humu duniani!?
Hivi wewe unafikiri,kama historia ya ndugu zetu Wanawake isingalikua ni ya mateso,dhuluma,ubakaji,unyang' anyi,mauaji na kunyimwa haki zao nyingi mno wanazostahili,je kungalikua na haja ipi ya hao Wanawake kujaribu kudai haki au watambuliwe as equals hivi leo humu duniani!?
Jamaa yangu Mgibeon,yaani umeshindwa kabisa kuliona hilo,na umekuja na arrogant remarks tena kwa mbwembwe nyingi,huku ukilinganisha madhila na dharuba za Wanawake na zile za Waislam!?...yaani,kama vile unajua mambo meengi ya maana!?
Ni kweli yawezekana kabisa yakuwa pana similarities nyingi mno,kwa madhila,dhuluma na nakma walizopitia/wapitiazo Waislam na ndugu zetu Wanawake,kama ulivyojitahidi kuyakinisha...sasa badala ya kuwabeza na kuwafanzia tahstit ,nafikiri la muhimu ni kutafuta ufumbuzi kwayo!?
Na hii itakua ni kwa manufaa yetu soote,Taifa letu changa na Vizazi vyetu vyoote vijavyo!
However,you sound a sincere person and I respect you for that.
No need for me to question the premise of your moral fundamentals.
But,but,when you can afford a little chance,read with understanding...I mean re-read your post and just think, Sir!
Wanawake ndugu zetu maskini,wamepitia mateso na dharuba nyingi mno na mpaka kesho wanaendelea kuteseka pita kiasi kwenye mikono ya hao Wanaume ati unaojaribu kuwasifia.
Mifano ni mingi mno pita kiasi...jaribu kuchungulia kuanzia kwenye medieval history na contemporary history;
Afrikan civilizations,Whites/European Civilizations,Hindus/Indian sub-continent,Arab/middle Eastern Civilizations,Chinese Civilization,Mayans,Aztecs na wengineo wengi mno.
Pitia hata recent history ya hata hizo nchi wajiitazo at ndo cradle of "democracy"/Western World...chungulia unyama,ubakaji,mauaji na unyanyasaji wa pale Amerika,Britain,France dhidi ya Wanawake for centuries and centuries na mpaka kesho bado kuna vitimbi na vituko kadhaa,ambavyo nina hakika wajua mangi mno!
Yaani ukatazama yayo na huko koote,ndugu zetu Wanawake,ni wa kuhurumiwa na pia...it's our moral and legal responsibility yetu sisi kuwasaidia na kushughulika nao pamoja ili kutokomeza hiyo gender discrimination.
Nastaajabu mno,yawaje leo katika hii 21th Century,mtu ajiitae ati ndo "msomi",khalafu unakua na hizo primitive views/attitudes!? Dah! Lazim nikubali yakuwa nimehuzunika kukusoma.
Next time when you write,please try to be guided by solid evidences and influenced by events,Ok Sir!?
Nipa fursa niwaite Dada zangu,King'asti,Angel Nylon na Faizafoxy ili tuone nao watatoa maoni yapi kwa hiyo bayana yako dhaifu/discriminatory!?
Natamani mno kuona Mujitahid Wabara,yeye naye atakwambani kwayo ulonena!?
Shukran kwa kunisikiza,na niwia radhi kama kuna lolote nimenena kwenye huo uchechefu wangu,nawe labda hukupendezwa nalo!?
Ahsanta.
Ahsante sana kwa kunialika kuchangia yatuhusuyo wanawake, ingawa sipendi kutoka nje ya mada ya mjadala huu, kwa mualiko inanilazim kidogo kwani inagusia wanawake.
Naomba kuwawekea kipande kidogo cha video kuhusu moja ya swali linalowatatiza sana wanawake wasio Waislaam ambalo kwa mwanamke wa Kiislaam ni kitu cha kawaida na wala hakifikirii:
[video=youtube_share;v6kR2XvZqgI]http://youtu.be/v6kR2XvZqgI[/video]