Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Tuachane na vita vya Israel na Hamas.Hivi vita vimeisha na Israel haiwezi kuwapata Hamas wala mateka.
Uchunguzi wa kitaalamu ukihusisha mizozo mengine ya kivita ya miaka ya karibuni unaonesha Hamas wameyeyuka kabisa na kilichobakia ni mahandaki na alama zao nyengine kuwa walikuwepo
Uchunguzi unaonesha kuwa Hamas wataibuka mbeleni na kuendeleza vita ambavyo kamwe Israel hatoviweza kuvimaliza.Hilo limeshajulikana na Israel na sasa inapiga kwa malengo hayo ya kuzuia vita vya mbeleni jukumu ambalo ni gumu sana.
Sasa kwanini Israel inaachwa ifanye vitendo vya kifirauni mbele za walimwengu,ambavyo ni kuuwa watoto inaodhani wanaoweza kuchukua majukumu ya Hamas miaka ijayo..Lakini hizo zitabaki ni dhana na haiwezi kuhalalisha unyama inaofanya sasa.
Shule moja baada ya nyengine zinapigwa kwa mabomu mazito na kuua watoto.Vitoto vinakujfa mbele ya wenzao na watu dunia nzima wanaona.
Nimeangalia matukio ya kutisha sana ya wazee wakiokota vipande vya watoto wao waliokuwa wakisafiri nao kuelekea kusini.Vijana wenye njaa wanachimba vifusi kwa mikono yao kutafuta waliofukiwa.Huko ni kuchanganyikiwa kwani mikono haiwezi kuinua mazege na kubinua nondo zilizojengewa majengo hayo.Ndio maana kuna idadi kubwa mpaka sasa wamebaki chini ya vifusi.
Wanawake wanalia mpaka machozi yanakauka kuomba msaada kwa wanaume wa dunia nzima. Sauti zao ni ushahidi wa kuIshiwa na nguvu kwa majonzi
Wenye uwezo wa kuzuia hayo,huu ni wakati wao na sio matamko ya kisiasa kwa jambazi ambaye hasikilizi maneno hayo.Kuacha kufanya hivyo kwa hakika ni kukaribisha majanga kwa dunia nzima katika mfumo wa mabalaa yanayofanana na corona ambapo kila mmoja wetu hatoishi kwa raha tena bila kujjali dini zetu.
Wapo wengi katika nchi za mbali na eneo la tukio wameacha kuzungumzia vita vya Israel na Hamas na wanazaungumzia maangamizi (genocide) basi.