Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
- Thread starter
- #21
Asante.Mkuu Bams kawaida una michango inayoonyesha kama vile wewe ni mtu mwerevu sana.
Contrary mtu yeyote anaetetea unnecessary loss lives kwa udini ni mtu wa hovyo.
Hamas ni wapuuzi, kwenda kuuwa vijana wasio na hatia, huku wakijua mziki utakaofuata hawataweza mudu.
Shida ya Netanyahu ni gaidi la asili, huko Israel kesho ukiitwa uchaguzi ashidi kwa siasa zake, siku uingia madarakani kwa serikali za mseto.
Ni sawa kwa watu wenye elimu ndogo kushabikia haya mambo. Lakini kwa watu wanaojinasibu ni timamu kushabikia mauaji ya watu wasio na hatia; shows how shallow you are.
Benjamin Netanyahu hata kesho ukiitishwa uchaguzi apati ushindi wa majority; maana yake kuna waisraeli wengi sana hawafurahishwi na kinachoendelea huko Middle East,
You are so shallow
Sijawahi kushabikia mauaji ya mtu yeyote, yawe ya mtu wa namna gani, labda mtu huyo awe hatari kwa uhai wa watu wengine. Ndiyo maana sijawahi kufikiria kuwa uharamia ule walioufanya Hamas dhidi ya raia wa Israrl lilikuwa ni jambo sahihi. Wapalestina wange-gain zaidi kupambania haki zao zozote zile kwa njia nyingine kuliko tendo lile la kishetani walilolifanya October mwakajana. Yawezekana kweli wapalestina walikuwa wakionewa huko Gaza, lakini kwa ugaidi ule waliokuwa wameufanya, umewasaidia au umewaangamiza zaidi?
Ni kweli kuwa Netanyahu ana upinzani mkubwa nchini mwake, siyo kwa sababu ya vita hii, bali hata kabla ya October mwakajana. Wapalestina wangekuwa na hekima, walitakiwa ku-explore hiyo oppourtunity kutetea agenda yao kwa njia ambazo zingewapa faida kuliko kupoteza.
Unapopambana na adui yako ni vema uujue udhaifu na nguvu zako vipo wapi. Kama ni kweli IDF ilikuwa inadhulumu uhai wa Wapalestina, na wao Wapalestina kama waliamua kupambana kwa mtutu wa bunduki, basi hata shambulio lao la mwakajana basi lingewalenga askari pekee bila ya kuua watoto na wasio wanajeshi. Hiyo ingewafanya kuungwa mkono zaidi na taasisi mbalimbali, hata za ndani ya Israel. Kitendo cha Hamas kumwua kila waliyeweza kumfikia, kilitoa sympathy kwa reaction ya Serikali ya Netanyahu. Ufahamu kuwa makundi ya kigaidi kama Hamas, Hezbollah na Houth, yote yanachukiwa sana na nchi zote za kiarabu kwa sababu pia yana terrorize serikali za mataifa ya kiarabu. Kuyatumia makundi hayo katika kupigania haki za wapalestina, hutegemei kupata mafanikio.