Israel Iliitaarifu Iran Maeneo Itakayoyapiga, Lengo Lilikuwa Ni Nini?

Israel Iliitaarifu Iran Maeneo Itakayoyapiga, Lengo Lilikuwa Ni Nini?

Hoja ni kwamba hata wasingefanya wangeuwawa tu? Huko westbank hakuna hamas wala magaidi ila wanakufa maelfu kila mwaka kwa risasi za wayahudi. So ni ujinga kudai vifo vya palestina ni sababu ya October 7?
Unaenda kuchokoza nyuki aliejenga kwenye nyumba yako unategemea nini? Halafu nimeweka clip ya mdogo wako hapo sijaona kuguswa wala kurusha mate kama unavyofanya kwa hao wapalestina
 
Hawa sio makatili sijaona sehemu yyte ukianzisha thread au kuchangia nyuzi kama uliguswa na kifo cha huyu kijana
Mara nyingi tu nimesema Hamas wanakosea kuua raia kama tu Netanyahu anavyokosea labda kma umeanza kunisoma juzi. Nachosema ni kwamba kuuawa kwa wapalestina hakukuanza wala hakutaishia October 7 ni sawa na mwenye nyumba kumbaka housegirl alafu siku akivaa khanga moja aseme nimembaka kisa amenitega! Ndio maana nimekuuliza westbank hakuna magaidi mbona wanapigwa risasi kila siku?
 
Mara nyingi tu nimesema Hamas wanakosea kuua raia kama tu Netanyahu anavyokosea labda kma umeanza kunisoma juzi. Nachosema ni kwamba kuuawa kwa wapalestina hakukuanza wala hakutaishia October 7 ni sawa na mwenye nyumba kumbaka housegirl alafu siku akivaa khanga moja aseme nimembaka kisa amenitega! Ndio maana nimekuuliza westbank hakuna magaidi mbona wanapigwa risasi kila siku?
Kama kuna magaidi hapo westbank kwanini wasiuwawe? Then mbona hao raia wa palestine wana infilitrate kuingia tel aviv na miji mingine kushambulia raia je ni jambo la kuchekea?
 
Kwa hiyo unadhani wa - Israel wangetaka serikali yao chini ya Ben Netanyau ingefanyaje...?

Kwamba ishambuliwe na Hammas na Hesbollah wakisaidiwa na Iran itulie tu bila kujilinda na hapo ndiyo wa - Israel wanaweza kumpa kura PM wao iwapo kungekuwa na uchaguzi...?

Honestly, nimekusoma na mwisho nikashindwa kukuelewa hoja yako inasimama na kutetea nini hasa...

IKO HIVI:

Kama hao Hammas/Lebanon na Iran wanataka wasiendelee kufa, waache kulichokoza taifa teule la Mungu - ISRAEL...

Mungu aliapa kwa kinywa chake kusema hivi katika Neno lake - Biblia👇👇👇

AMOS 1: 6 - 7

"....‬Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Gaza, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu waliichukua katika hali ya kufungwa kabila nzima, wawatie katika mikono ya Edomu; lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake..."

There's no way kuwa Gaza itapona....

Na watu au taifa jingine lolote linalojaribu kuitetea Gaza/Lebanon iwe ni Iran au yeyote, tambua kuwa nao watahesabiwa wakosa na hukumu hiyo ya Mungu nao itawaangukia/itawahusu pia....

Kwa hiyo ukiona vifo huko, tambua kuwa vimeamuliwa na Mungu na mwenyewe hivyo. Yeye anaumba/toa uhai na anaweza kubomoa au kuutwaa uhai huo pia....

Kwa hiyo hapo hoja yako ya kushabikia au kutoshabikia vifo wala hata haina maana yoyote maana kilichosemwa na Mungu ni lazima kiwe hivyo bila kujali mwanadamu ana mtazamo gani juu ya maamuzi yake.....!!
Kama kweli Mungu kahalalisha mauaji ya watu wasio na hatia, je, Unadhani Yesu angekuja leo angetumia upanga kuitafuta amani?
 
Unaenda kuchokoza nyuki aliejenga kwenye nyumba yako unategemea nini? Halafu nimeweka clip ya mdogo wako hapo sijaona kuguswa wala kurusha mate kama unavyofanya kwa hao wapalestina
Mbona nimeshasema ni kosa kuua innocent people hii nimekemea kwa hamas na Israel pia. Nachouliza huko westbank muisrael gani aliuwawa? Mbona nao wanapigwa risasi na mabomu kila kukicha
 
kama Magufuli (ningekuwa mimi ndio yeye, kwenye nafasi yake) ningeamuru Lissu, ashughulikiwe kipindi cha mjadala wa ACCACIA
Hujitambui kabisa, yaani unaacha kina chenge waliokula mabilion kupitisha mikataba mibovu unakuja kuua ambaye hajaonja hata buku ya hiyo mikataba mibovu? Hizi akili ndio maana Afrika haiendeleei.
 
kuna magaidi hapo westbank kwanini wasiuwawe?
Nitajie gaidi mmoja tu westbank? Hao Israel wanaua watu Westbank licha ya kwamba hakuna gaidi. Ndio uone ukatili wa Israel haujalishi unamshambulia au lah. Embu Google maana ya JEWISH SETTLERS ndio utaelewa nachoongea.
 
Nitajie gaidi mmoja tu westbank? Hao Israel wanaua watu Westbank licha ya kwamba hakuna gaidi. Ndio uone ukatili wa Israel haujalishi unamshambulia au lah. Embu Google maana ya JEWISH SETTLERS ndio utaelewa nachoongea.
Wewe umeandika west bank kuna magaidi na mimi nikamalizia kama wapo kwanini wasiuwawe? Au mimi niliandika west bank kuna magaidi?
Na hitishima as long as yule dogo wa SUA alikufa kikatili basi acha na hao palestinian wafe hivyo hivyo
 
umeandika west bank kuna magaidi na mimi nikamalizia kama wapo kwanini wasiuwawe?
Sasa si uweke link hapa kwamba kuna magaidi westbank!! Mimi nachojua huko walowezi wa kiyahudi wanajitanua kwa kuua raia wasio na hatia. So hata bila October 7 hao wayahudi wanaua wapalestina bila hatia. So don't justify brutality kwa kigezo cha Mollel kwani hata hao Syria ambao kila siku wako bombarded na Israel walimuua Mollel?
 
Israel na Iran, zote zimekiri kuwa Israel, kabla ya kufanya shambulio dhidi ya Iran, kwanza iliitaarifu Iran juu ya muda na maeneo ambayo ingeyashambulia. U aweza kushangaa na kujiuliza, lengo lilikuwa ni nini? Maana ni sawa sawa mtu akuvizie ukapige kwenye mguu, ukaa kimya, halafu siku nyingine umtaarifu kuwa kesho nakuja kukupiga, nitakupiga usoni!!

Ilichofanya Israel ni uungwana wa hali ya juu katika vita. Inaonekana dhamira ya Israel ilikuwa kusiwepo na kifo cha mtu hata mmoja. Israel ilitaka maeneo itakayoyapiga, watu wote waondoke ili kusiwepo na maafa. Halafu ikaionya Iran kuwa isijibu, na kama itajibu basi Israel itafanya harsh attacks. Israel iliileza Iran kuwa haina haja ya vita na Iran kwa kuwa ipo busy na kuwamaliza Hamas na Hezbollah. Iran nayo ikajibu kuwa ina haki ya kujilinda inaposhambuliwa ndani ya nchi yake LAKINI inatambua wajibu wake wa kuhakikisha eneo la Mashariki ya Kati linakuwa na amani.
Hivi kuna jeshi lolote limewahi kufanya hivyo? Urusi iige ustaarabu wa IDF huko Ukraine.

NOTE: Kwa hali inavyoenda, kuna uwezekano Hamas na Hezbollah wakaachwa wapambane wenyewe bila ya msaada wa Iran. Kitendo cha Israel kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja, ni ishara ya kukaribiana zaidi, na uhasama mipngoni mwao unaanza kupungua. Siku ambayo Iran na Israel wakageuka na kuwa majirani wema, Mashariki ya Kati yote itatulia na kuwa na amani.

Tushukuru na kufurahia mahasimu wanapoanza kuwasiliana, maana ni ishara njema kwa siku za uson. Msisahau ule msemo wa wahenga wetu, 'wapiganao ndio wapatanao"

US outlet Axios reported that prior to the attacks, Israel sent Iran a message revealing certain details about the strikes, and warning Tehran not to respond.
That could be a sign Israel does not want to escalate the situation further - at least for now.
“We are focused on our war objectives in the Gaza Strip and Lebanon. It is Iran that continues to push for a wider regional escalation,” the IDF said in a statement.
A senior US official said "this should be the end of this direct exchange of fire between Israel and Iran".
Iran’s foreign ministry said it was "entitled and obligated to defend itself" and described the attack as a violation of international law.
But it also said that Tehran recognises its "responsibilities towards regional peace and security".

Kwa kauli hii ya Iran, haina mpango wa kuishambulia
Kumtaarifu hasimu wako kuwa unatinga kwake kwenda kumfanyia tukio na ukaenda kweli, ni mbinu ambayo hata majambazi zamani waliitumia kuwataarifu walengwa, wajitayarishe na watayarishe kiwango cha fedha kinachotakiwa, kweli walienda wakavamia na kutoka kwa heshima.

Ubabe wa namna hiyo huwa huyo mhalifu kajiandaa, kupeleleza na kujihakikishia usalama wake pindi anapoenda kufanya tukio kwamba upo 100%, ni ubabe tu.

Kwa mfano huo, Israel kumtaarifu Iran kuwa ajiandae inaenda kumpiga na ikatakeleza ujumbe huo, ni ubabe wa kuvuana nguo na si dalili ya urafiki hiyo.

Israel angehitaji mahusiano mema, asingeenda kulipiza kisasi na kuleta uharibifu mkubwa alioufanya, angelimezea na kumtaarifu Iran ama kumkalia kimya.

Kumtaarifu Iran na wakaenda kweli kupiga ni njia nyingine ya kuieleza dunia na kumweleza Iran kwamba hakuna njia ama mbinu yoyote inayoweza kumzuia Israel asitekeleze shambulio lake kwenye anga na ardhi ya Iran, hakuna kingine zaidi ya ubabe.
 
Back
Top Bottom