Israel Iliitaarifu Iran Maeneo Itakayoyapiga, Lengo Lilikuwa Ni Nini?

Asante.

Sijawahi kushabikia mauaji ya mtu yeyote, yawe ya mtu wa namna gani, labda mtu huyo awe hatari kwa uhai wa watu wengine. Ndiyo maana sijawahi kufikiria kuwa uharamia ule walioufanya Hamas dhidi ya raia wa Israrl lilikuwa ni jambo sahihi. Wapalestina wange-gain zaidi kupambania haki zao zozote zile kwa njia nyingine kuliko tendo lile la kishetani walilolifanya October mwakajana. Yawezekana kweli wapalestina walikuwa wakionewa huko Gaza, lakini kwa ugaidi ule waliokuwa wameufanya, umewasaidia au umewaangamiza zaidi?

Ni kweli kuwa Netanyahu ana upinzani mkubwa nchini mwake, siyo kwa sababu ya vita hii, bali hata kabla ya October mwakajana. Wapalestina wangekuwa na hekima, walitakiwa ku-explore hiyo oppourtunity kutetea agenda yao kwa njia ambazo zingewapa faida kuliko kupoteza.

Unapopambana na adui yako ni vema uujue udhaifu na nguvu zako vipo wapi. Kama ni kweli IDF ilikuwa inadhulumu uhai wa Wapalestina, na wao Wapalestina kama waliamua kupambana kwa mtutu wa bunduki, basi hata shambulio lao la mwakajana basi lingewalenga askari pekee bila ya kuua watoto na wasio wanajeshi. Hiyo ingewafanya kuungwa mkono zaidi na taasisi mbalimbali, hata za ndani ya Israel. Kitendo cha Hamas kumwua kila waliyeweza kumfikia, kilitoa sympathy kwa reaction ya Serikali ya Netanyahu. Ufahamu kuwa makundi ya kigaidi kama Hamas, Hezbollah na Houth, yote yanachukiwa sana na nchi zote za kiarabu kwa sababu pia yana terrorize serikali za mataifa ya kiarabu. Kuyatumia makundi hayo katika kupigania haki za wapalestina, hutegemei kupata mafanikio.
 
lengo ni kutaka kujua na kujiridhisha juu ya nguvu na uwezo wa Iran wa kujilinda, kuzuia na kudhibiti mashambulizi ya Israel.

Infact,
walitaka Iran iactivate mifumo yake yote ya ulinzi ili iwe rahisi kwa Israel kuona aina tofauti ya mashambulizi yasiyoweza kuzuiliwa na mifumo hiyo active ya Iran 🐒
 
Israel ana ubinadamu huwa hataki kuua binadamu ila hutaka kuharibu miundombinu ya kivita na maghala ya silaha

Hivyo h8tangaza mapema ili binadamu yeyote aondoke hilo eneo atwange
.akibaki shauri yake atajamba cheche
Upo sahihi sn mkuu
 
Siasa za M.E ni complicated ndio maana Netanyahu kwao hawezi shinda kwa majority.

Jews sio kama tunavyodhani sisi ni hawa waliotoka ulaya. La hasha hayo makabila 12 ni vurugu machi ndio maana wana uwezo wa kuingilia usalama wa nchi zozote M.E maana ni waarabu ambao uwezi jua, wa Iran uwezi jua na ndio walio wengi.

Jews kwa makabila yao they can infiltrate anywhere in the M.E ni imani tu na kulipuana.

Halafu huo Jews na Waisalamu (wako karibu kwenye kufanya ibada) kushinda Jews na Ukristo.

Jews na Islam wote wanafanya ibada kuelekea M.E (Jews kuangalia Jerusalem, waislamu kuelekea kwenye Kaaba). Wakristo wao hawajali kanisa linaelekea wapi.

Jews na waislamu maandishi yao yanatoka kulia kwenda kushoto, wakristo maandishi yao yanatoka kushoto kwenda kulia.

Jews na waislamu namna yao kuchinja mnyama ni moja (wachinjaji wa nyama wanayokula Jews ni waislamu) Jew hawezi kula nyama ilyochinjwa na mkristo.

Kwa kifupi ni hivi kita madini Jewish na Uislamu (unafanana) kuliko Christianity na Jewish. Embu jifunzeni hizi; Israel kuna Jews hadi kutoka Afghanistan. Kuna sehemu ambayo usalama wao haiwezi infiltrate M.E

Kwa mtu unaejinasibu kuelimika kuchukua upande kwenye hii mijadala ya dini, binafsi unanishangaza.
 
Huna akili, Israel umewahi kusikia kuna wizi, rushwa, teuzi za kiukoo na ufisadi kama Tanzania?
 
Maelezo mengi Sana lakini wewe umetawaliwa na udini,hivi unyama wa Israel huuoni?, stupid man, endeleeni kujidanganya Israel ni taifa la mungu, pathetic
 
Hamas ni wapuuzi, kwenda kuuwa vijana wasio na hatia, huku wakijua mziki utakaofuata hawataweza mudu.
Je unatakiwa ufanyeje ukikaliwa kimabavu na majeshi ya wavamizi? Ni ajabu kuongelea October 7th unasahau miaka zaidi ya 60 hao wapalestina wanauawa ili kupisha makazi ya walowezi wa kiyahudi!!
 
Kwahiyo wangefanyeje ili watume ujumbe? Maana nao wameuwawa bila hatia kwa miaka minga hata bila uwepo wa vita. Mfano kuna walowezi laki 5 wamehamia mipaka ya palestina na wameua wapalestina wasio na hatia ili wajenge makazi yao je huo sio ukatili?

Pia haijawaangamiza zaidi maana hata bila vita kuanzia 2009 mpaka 2023 hao wapalestina walishauwawa zaidi ya maelfu na hakukuwepo vita. Ni ajabu sana mtu kuchukulia october 7 kama ndio chanzo cha mateso ya wapalestina wakati hata bila vita malaki walishauwawa na wayahudi huko westbank na gaza.
 
Israel ana ubinadamu huwa hataki kuua binadamu ila hutaka kuharibu miundombinu ya kivita na maghala ya silaha

Hivyo h8tangaza mapema ili binadamu yeyote aondoke hilo eneo atwange
.akibaki shauri yake atajamba cheche
Kumbe je huko westbank huwa anauwa wapalestina kwa sababu gani na hakunaga Hamas huko? Hao ni makatili acheni justification za kitoto humu. Wangekua na ubinadamu wasingefadhili makundi ya waasi huko Kivu kaskazini kuwachimbia cobalt.
 
Toa hoja usimshambulie Mtu. Hapo Ndipo unafeli Dogo
 
Je unatakiwa ufanyeje ukikaliwa kimabavu na majeshi ya wavamizi? Ni ajabu kuongelea October 7th unasahau miaka zaidi ya 60 hao wapalestina wanauawa ili kupisha makazi ya walowezi wa kiyahudi!!
Hamas walichofanya oct 7 waliwapa israel justification kuendeleza walipoishia na kutanua wigo wa makazi yake
Ila acha wapigwe naumia sana huyu mdogo wangu kuuwawa kikatili shame on you

View: https://x.com/DrewPavlou/status/1849878226195316876?t=0vwvm9pOTeJMKs-ehXFTWw&s=19
 
Kumbe je huko westbank huwa anauwa wapalestina kwa sababu gani na hakunaga Hamas huko? Hao ni makatili acheni justification za kitoto humu. Wangekua na ubinadamu wasingefadhili makundi ya waasi huko Kivu kaskazini kuwachimbia cobalt.
Hawa sio makatili sijaona sehemu yyte ukianzisha thread au kuchangia nyuzi kama uliguswa na kifo cha huyu kijana

View: https://x.com/DrewPavlou/status/1849878226195316876?t=0vwvm9pOTeJMKs-ehXFTWw&s=19Udini umekujaa unaumia waarabu kufa kuliko mtanzania mwenzako mwenye rangi nyeusi kama ww tena na lafudhi kama yako
Bure kabisa wewe acha wavune walichokipanda

View: https://x.com/DrewPavlou/status/1849878226195316876?t=0vwvm9pOTeJMKs-ehXFTWw&s=19
 
Hoja ni kwamba hata wasingefanya wangeuwawa tu? Huko westbank hakuna hamas wala magaidi ila wanakufa maelfu kila mwaka kwa risasi za wayahudi. So ni ujinga kudai vifo vya palestina ni sababu ya October 7?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…