Israel na Hamas wakubali kusitisha mapigano eneo la Gaza

osu2014

Member
Joined
Mar 31, 2014
Posts
20
Reaction score
54
Muda mchache uliopita taarifa kubwa kwenye vyombo vya habari vyote vya Kimataifa Aljazeera, CNN na nk ni juu ya Makubaliano ya Kusitisha Mapigano kati ya Israel na Hamas.

Kufikiwa kwa makubaliano haya kumefanya wakaazi wa Gaza kushangilia na kuandamana barabarani kwa furaha na vifijo.

Israel na Hamas wamefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa lengo la kumaliza miezi 15 ya mzozo katika Ukanda wa Gaza. Makubaliano haya, yaliyosimamiwa na Qatar, Misri, na Marekani, yanafanyika kwa awamu tatu ndani ya wiki sita.
Awamu ya Kwanza: Hatua za Haraka
• Kusitisha Mapigano: Kusitisha mapigano kwa muda kutaanza Jumapili, Januari 19, 2025, na kusitisha vita vilivyokuwa vikiendelea.
• Kubadilishana Wafungwa na Mateka: Hamas itawaachilia mateka 33 wa Kiyahudi, wakiwemo wanawake, watoto, na wazee. Kwa upande mwingine, Israel itawaachilia mamia ya wafungwa wa Kipalestina.
• Msaada wa Kibinadamu: Makubaliano yanaruhusu msaada wa kibinadamu kupelekwa Gaza, ambapo malori 200 ya misaada yatapita kila siku.

Awamu ya Pili: Kuachiliwa Zaidi na Kuondolewa kwa Jeshi
• Kuachiliwa Zaidi kwa Mateka: Majadiliano yataendelea kwa ajili ya kuachiliwa mateka waliobaki, wakiwemo wanajeshi wa Kiume, kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina.
• Kuondolewa kwa Jeshi la Israel: Israel itaanza kuondoa majeshi yake kutoka maeneo yenye watu wengi Gaza, ili kuruhusu Wapalestina waliokimbia kurudi nyumbani.

Awamu ya Tatu: Ujenzi Mpya na Kusitisha Mapigano ya Kudumu
• Jitihada za Ujenzi Mpya: Mipango itatekelezwa kwa ajili ya ujenzi mpya wa Gaza, ikilenga kurejesha miundombinu na kusaidia raia walioathirika.
• Majadiliano ya Kusitisha Mapigano ya Kudumu: Mazungumzo yatalenga kuanzisha amani ya kudumu kwa kushughulikia masuala ya msingi ili kuzuia migogoro ya baadaye.

Makubaliano haya yamepokelewa kwa hisia tofauti. Waisraeli wengi wanaunga mkono makubaliano hayo kwa sababu yanatoa kipaumbele kwa kuachiliwa kwa mateka. Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wa mrengo wa kulia wa Israel wanapinga, wakihofia kuwa yanaweza kudhoofisha juhudi za kumaliza Hamas.

Kwa upande mwingine, wakaazi wa Gaza wameonyesha matumaini kuwa makubaliano haya yataleta amani na fursa ya ujenzi mpya.

Kufikiwa makubaliano haya unategemea ahadi ya pande zote kufuata masharti na kushiriki kikamilifu katika mazungumzo ya awamu zinazofuata.
 
Malengo ya Israel huko Gaza, pili Lebanon (Hezbollah), na tatu Syria yamefanikiwa kwa 100%. Yemen (Houthi) in good progres. Kubwa lao (Iran) limelemazwa kwa kiwango cha kutisha. So, with that in mind, Israel kubadili msimamo ni sahihi.

Lebanon imepata rais, uongozi wa Syria umebadilishwa, cream ya makundi ya kigaidi tishio kwa Israel (Hezbollah & Hamas) imefyekwa, Israel imejitwalia maeneo for military strategic reasons hayo ni mafanikio ya kupigiwa mfano katika medani za kijeshi. Majeshi duniani yakajifunze Israel!
 
Malengo mengine ya Israel ambayo hayajifikiwa ni yapi?. Au wametimiza yote kwa 100?.
 
Baada ya vifo vingi vya Wapalestina na baada ya Sinwar na Haniyah kuuawa ndio makubaliano yamefikiwa.

Hamas imewaletea Wapalestina maafa.

Sinwar nasrallah Adiosamigo and 100 others
 
ila kiminyo walicho pigwa wapelestina hawana hamu tena na vita ,maana hapo mwanzo ilishazoeleka wapesstina kuonesha alama ya resistance pale kunapokuwa na ceaze fire lakini safiri hii wanapiga makofi na kuruka ruka kama ndama wakiona huu kama muujiza.
Vita haijawahi kuwa nzuri popote pale Duniani , sio palestina Wala Ukraine, kuwadhihaki watu kwa kushangilia kwao usitishwaji wa vita, ukiwa kama binadamu mwenye utashi sidhani kama ni sahihi.
 
Malengo ya Israel huko Gaza, pili Lebanon (Hezbollah), na tatu Syria yamefanikiwa kwa 100%. Yemen (Houthi) in good progres. Kubwa lao (Iran) limelemazwa kwa kiwango cha kutisha. So, with that in mind, Israel kubadili msimamo ni sahihi.

Lebanon imepata rais, uongozi wa Syria umebadilishwa, cream ya makundi ya kigaidi tishio kwa Israel (Hezbollah & Hamas) imefyekwa, Israel imejitwalia maeneo for military strategic reasons hayo ni mafanikio ya kupigiwa mfano katika medani za kijeshi. Majeshi duniani yakajifunze Israel!
Lengo lilikuwa kuiangamiza hamas je hamas imeangamia? Hezbollah wamesharudi kwenye mipaka ya kusini mwa Lebanon kama mwanza

Kiufupi Israeli hapo hajaambulia kitu na hamas inastahili ushindi coz imeizuia Israeli isifanye mageuzi ya kiutawala hapo ghaza
 
ila kiminyo walicho pigwa wapelestina hawana hamu tena na vita ,maana hapo mwanzo ilishazoeleka wapesstina kuonesha alama ya resistance pale kunapokuwa na ceaze fire lakini safiri hii wanapiga makofi na kuruka ruka kama ndama wakiona huu kama muujiza.
Amani haiji ila kwa ncha ya upanga! Hii vita imethibitisha huu wasia wa kale.
 
Lengo lilikuwa kuiangamiza hamas je hamas imeangamia? Hezbollah wamesharudi kwenye mipaka ya kusini mwa Lebanon kama mwanza

Kiufupi Israeli hapo hajaambulia kitu na hamas inastahili ushindi coz imeizuia Israeli isifanye mageuzi ya kiutawala hapo ghaza
Huu mtazamo wako ungekuwa perfect kama mchokozi angalikuwa Israel. In contrary, waliolianzisha wametulizwa vilivyo ushindi ni wa nani?
 
Malengo ya Israel huko Gaza, pili Lebanon (Hezbollah), na tatu Syria yamefanikiwa kwa 100%. Yemen (Houthi) in good progres. Kubwa lao (Iran) limelemazwa kwa kiwango cha kutisha. So, with that in mind, Israel kubadili msimamo ni sahihi.

Lebanon imepata rais, uongozi wa Syria umebadilishwa, cream ya makundi ya kigaidi tishio kwa Israel (Hezbollah & Hamas) imefyekwa, Israel imejitwalia maeneo for military strategic reasons hayo ni mafanikio ya kupigiwa mfano katika medani za kijeshi. Majeshi duniani yakajifunze Israel!
Lengo la Israel lilikuwa ni kuiondoa Hamas kwenye utawala wa gaza na kuiangamiza kabisa ,kukoboa mateka, lakini mpaka sasa vita imefika ukingoni mateka hawajaokolewa badala yake Israel inalazimika kulipa kwa kuwaachia maelfu ya wafungwa wa kipalesitina ili mateka waachiwe .

Mpaka sasa Hamas haijaangamizwa ,na Israel inaondoa wanajeshi wake na kuiacha gaza ikiwa chini ya utawala wa Hamas.
 
Huu mtazamo wako ungekuwa perfect kama mchokozi angalikuwa Israel. In contrary, waliolianzisha wametulizwa vilivyo ushindi ni wa nani?
Lengo la netanyau ni kulifuta kundi la hamas je hamas imefutwa?

lazima tukubali Israeli ilikutana na upinzani mkali madogo walikaza sana netanyau

Israeli ilikubali amani na Hezbollah baada ya kuona misseli za Hezbollah zinapiga target bila upinzani wowote kutoka kwenye air defense mpaka ikafika stage drone kutoka Lebanon kuipiga nyumba ya netanyau bila kikwazo
 
ila kiminyo walicho pigwa wapelestina hawana hamu tena na vita ,maana hapo mwanzo ilishazoeleka wapesstina kuonesha alama ya resistance pale kunapokuwa na ceaze fire lakini safiri hii wanapiga makofi na kuruka ruka kama ndama wakiona huu kama muujiza.
Vita haitaisha kwa sababu kiini cha mgogoro hakijatatuliwa hapa vita ime sitishwa kwa muda miaka kadhaa mbele italipuka tena na wenda yakatokea maafa zaidi ya haya.
 
HAMAS alitaka kuachia awa mateka tangu mwanzo lkn kibri cha Netanyahu kimefanya mateka kibao kufa IDF kibao kufa tena vijana wadogo baada ya majanga yoteeee!! ayo ndio Netanyahu anabaini HAMAS ni fupa gumu kwa IDF kulishinda sasa kakubali yaleyale aliokataa mwanzooo! YEMEN NDIO IMECHANGIA PAKUBWA HII AMAN.!!!!
 
Back
Top Bottom