Israel na Hamas wakubaliana kusitisha Mapigano

Israel na Hamas wakubaliana kusitisha Mapigano

Mashambulizi baina ya Israel na Palestina yamesimamishwa, baada ya siku 11 za ghasia kati ya pande hizo mbili.

Israeli imeukubali mpango wa Misri wa kusitisha mapigano mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2014, na imekubali bila masharti yoyote.

Misri sasa inatarajiwa kutuma wajumbe nchini Israeli na Ukanda wa Gaza katika siku chache zijazo kwa lengo la kuumaliza kabisa mgogoro huu.

Maafisa wa Hamas wanasema huenda makubaliano ya sasa yakawa na nguvu iwapo tu Israel itaacha kutumia nguvu katika masuala ambayo yanahitaji diplomasia, huku Israel ikisema Hamas inahitaji kushauriana vyema na mamlaka ya Palestina ili kunusuru machafuko mengine.

Sababu 6 zinazoeleza kwanini Israel inaweza kufanya lolote bila Marekani kuizuia

Je, ni kipi kinacholifanya shirika la ujasusi la Israel Mossad kuogopwa?
Nchi kadhaa zimehusika katika majadiliano hayo ya muda mrefu ikiwemo Misri, ambayo ni mshirika wa karibu wa pande zote mbili kwa sasa.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema mazungumzo ya siku 11 yamesaidia kufikia mafanikio hayo.

Rais wa Marekani Joe Biden aliitaka Israel kuwanusuru raia wasio na hatia

Baada ya habari hiyo kutangazwa, kulikuwa na mashambulio zaidi ya anga ya Israeli huko Gaza na makombora yalirushwa kuelekea Israeli. Wakati huo huo, uwanja mkuu wa ndege wa nchi hiyo, Ben Gurion, ulifungwa kwa muda mfupi kutokana na hofu ya usalama.

Inaarifiwa kuwa muda mfupi baada ya kutangazwa kusitishwa kwa mapigano, mamia ya watu wameanza kurejea katika makazi yao, licha ya miundombinu na nyumba zao kuharibiwa vibaya.

Hamas imeadhibiwa, na Wapalestina wa Gaza wameteseka sana. Wachambuzi wa siasa za Mashariki ya kati wanasema ili kuepuka mgogoro mwingine, ni vyema mahitaji ya pande hizi mbili yakafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Rais Biden alisema nini ?
Akiongea katika Ikulu ya White House, Rais Joe Biden alisema alimpongeza Bw Netanyahu kupitia simu baada ya kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

"Marekani inaunga mkono kikamilifu haki ya Israeli ya kujilinda dhidi ya mashambulio ya roketi ya kiholela kutoka Hamas na vikundi vingine vya kigaidi vya Gaza ambavyo vimeua watu wasio na hatia nchini Israeli," Bwana Biden alisema.

Alisema waziri mkuu wa Israeli alitambua kama yeye mfumo wa ulinzi unaojulikana kama Iron Dome, "ambao mataifa yetu yalitengeneza pamoja na ambao umeokoa maisha ya raia wa Israeli - wote Waarabu na Wayahudi".

Bwana Biden pia alimsifu Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kwa kufanikisha kusitisha mapigano, kabla hayajasababisha maafa ya watu wengi.

"Natuma pole zangu za dhati kwa familia zote, Israeli na Palestina, ambao wamepoteza wapendwa wao na kuwatakia afueni ya haraka kabisa waliojeruhiwa," alisema.

Rais alisema Marekani "inaendelea kujitolea kufanya kazi na Umoja wa Mataifa" katika kutoa msaada wa kibinadamu kwa Gaza na katika juhudi za ujenzi wa eneo hilo. Aliongeza kuwa hii itafanywa "kwa ushirikiano kamili na Mamlaka ya Palestina, sio Hamas".

Rais Sisi alisema alikuwa amepokea simu ya Bwana Biden na "furaha kabisa", na kuongeza kuwa "walibadilishana maono kuhusu jinsi ya kutafuta suluhisho ya kudumu kwa mzozo wa Gaza.

Nini kilipeleka mapigano kusistishwa?
Pande zote mbili zimekuwa zikikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka jamii ya kimataifa kumaliza uhasama.

Siku ya Jumatano, Rais wa Marekani Joe Biden alimwambia Bw Netanyahu "kwamba alitarajia kushuka kwa kiwango kikubwa kwa mapigano'.

Misri, Qatar na UN vimekuwa na jukumu la kuongoza mazungumzo ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na Hamas, ambayo inatawala Gaza.

Rais Sisi aliamuru makundi ya jumbe mbili za usalama kwenda Israeli na maeneo yaliyokaliwa ya Palestina kufanya kazi ili kufanikisha usitishaji wa vita, kulingana na Televisheni ya serikali ya Misri.

BBC Swahili
 
Hawa jamaa wamepigana tokea nina umri wa miaka 11 hadi leo nina umri wa miaka 37. Nashindwa kuelewa sababu ya wao kugombana ni Nini? Wanachogombania hadi leo hakuna hata mmoja kati yao aliyekipata? Umoja wa mataifa ni nini jukumu lao katika vita hii? Wahanga wa hii vita wanafidiwa na nani?
 
kwa majengo yaliyoharibiwa Gaza, hasara yake ni kubwa mno, vifo zaidi ya 200 wakati israel 12 tu.
 
Hawawez hata siku moja Israel kutumia nguvu kubwa kivile kwa watu wasio na hata silaha ni dalili nzur inayoonesha ni waoga Hamasa iliooneshwa na HAMAS watoto wa kipalestina na wanawake wao ni uzalendo mzuri na ipo siku IPO siku ipo siku WANYAMA haww wataanguka ktk mikono ya wanaume wa KWELI
Iran waliapa wataifuta israel wajaribu sasa na makobaz yao waingie hata hapo gaza frontline tuone najua utasema israel kaizunguka gaza kama iran ni powerful si anawapga tu hao wayahudi waliozunguka kisha anazama

Kawaida ya myahudi huwa hachokoz mtu huwa anavzia mtu ulianzshe sasa iran walianzshe tuone wachakazwe
 
Hivi 1967 ile ilikua Ni vita? Au wale wayahud fake wali wawahi kabla hawajatoka? MWAKA 1973 wayahud fake na wenyewe wali wahiwa na waarabu kilichowakuta hawaamini isingekua sifa za mwarabu Hilo Taifa lisingekuepo DUNIANI bila msaada wa RAIS NIXON mzee wa watar gate scandal wayahud fake walipelelekwa mpk bahari ya Mediterranean

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Ya 67 nishawahi isoma sehemu, nigusie na hii ya 73 chief.
 
Netanyahu atakuwa na hali mbaya maana Wazayuni wamemind walisema Netanyahu asijefikiria kabisa kuunda serikali ya muungano kama akisitisha mapigano bila kurejeshwa kwa Mateka wa Kiislaeli waliotekwa na pia walitaka Hamas aangamizwe kabisa na Gaza iwe chini ya Israel tena ili wasahau kabisa maroketi yasio na shabaha.. Alichofanikiwa Netanyahu kwa Hamas ni usitishwaji wa vita bila Masharti yeyote ya Hamas kuhusu Jerusalem ambapo ndio ilisababisha vita so Hamas chali na lengo lao...

Habari za hivi Punde Iran imetangaza Ushindi mkubwa kwa Hamas dhidi ya Israel.. utadhani yeye ndio alikuwa refaree
Iran anafanya propaganda ila Misri ana nafasi nzuri ya usuluhishi maana ana mahusiano mazuri nq pande zote
 
Shukrani kwa juhudi kubwa za Serikali ya Misri.

Serikali ya Israel na Wanamgambo wa Hamas & Islamic Jihad hatimaye wamekubaliana kusitisha mapigano yaliyodumu kwa siku kumi na moja.

Kwa mujibu wa muafaka huo wa pande mbili na usio na masharti mapigano yatasitishwa kuanzia saa 8:00 usiku huu kwa saa Israel.

Serikali ya Misri itatuma Wajumbe wa Usalama ili kusimamia utekelezwaji wa makubaliano hayo muhimu.

Mapigano hayo yamepelekea vifo vya watu 232 huko Gaza na 12 Israel.
Afadhali asee. Wasio na hatia walikuwa wakiangamia wengi.
 
Hawawez hata siku moja Israel kutumia nguvu kubwa kivile kwa watu wasio na hata silaha ni dalili nzur inayoonesha ni waoga Hamasa iliooneshwa na HAMAS watoto wa kipalestina na wanawake wao ni uzalendo mzuri na ipo siku IPO siku ipo siku WANYAMA haww wataanguka ktk mikono ya wanaume wa KWELI
Eti wanaume wa ukweli [emoji1787][emoji1787][emoji1787] tangu lini magaidi yakawa na akili?
 
Waisraeli siyo watu wazuri. Na hawa watu wanamiliki vyombo vya habari kwa hiyo hutaona habari njema kuhusu Hamas imeandikwa.
Siyo kwamba Mwisraeli anafanya uovu,ni kwamba ile dini yake inamsukuma kuchinjachinja watu. Dini siyo religion,ni anti religion,anti thesis.
Na wanaochinja binadamu huku wameshika kuran ni akina nani? Kuna wanyama zaidi ya hao?
 
Pamoja na kusimamisha vita kwa sasa ipo siku wataanza kujipima upya, yaani hawa jamaa mapigano kwao ni swala la kawaida tu ndo maana mataifa ya nje hawastuki kihivyo, washazoea kusikia Israel na Palestina wanarushiana marocket.
 
Hatimaye magaidi ya Hamas wataliona jua baada ya siku 10. Hayana aibu midume mizima inatumia wanawake na watoto kama ngao.
.... wajinga kweli! Unajiuliza la maana walilopata ni lipi baada ya tafrani waliyoianzisha wenyewe? Hakuna zaidi ya maafa kwa raia wasio na hatia - wanawake na watoto!
 
Netanyahu atakuwa na hali mbaya maana Wazayuni wamemind walisema Netanyahu asijefikiria kabisa kuunda serikali ya muungano kama akisitisha mapigano bila kurejeshwa kwa Mateka wa Kiislaeli waliotekwa na pia walitaka Hamas aangamizwe kabisa na Gaza iwe chini ya Israel tena ili wasahau kabisa maroketi yasio na shabaha..

Alichofanikiwa Netanyahu kwa Hamas ni usitishwaji wa vita bila Masharti yeyote ya Hamas kuhusu Jerusalem ambapo ndio ilisababisha vita so Hamas chali na lengo lao...

Habari za hivi Punde Iran imetangaza Ushindi mkubwa kwa Hamas dhidi ya Israel.. utadhani yeye ndio alikuwa refaree
... mafilisti wajinga sana! Walishaambiwa Yerusalemu ni ardhi "walipopumzika" manabii wa Mungu wa Yakobo sio pahala pa kuzika magaidi! Hivi kwa akili yao wanadhani kuna siku wataumiliki Mji wa Daudi?
 
Misri ndio mlezi wa hao watoto wawili wa baba mmoja anawajua in and out hata walipotaka kuuawa walikimbilia kwake, hata walipo patwa na baa la njaa waliponea kwake

Sasa linaibuka jitu jeusi tii kama mkaa linataka kujifanya ama ni li izrael zaidi ya izrael wenyewe au li arabu zaidi ya waarabu wenyewe

Linaanza kutoa matamko kwenye nyumba za ibada na mitnsaoni kitu ambacho hata asili ya mgogoro halijui linaishi kiisia tuu kutokana na lilivyokaririshwa na chuki lililonyweshwa na viongozi makanjanja wa dini

👏👏👏👏👏MISRI👏👏👏👏👏👏
 
Hawawez hata siku moja Israel kutumia nguvu kubwa kivile kwa watu wasio na hata silaha ni dalili nzur inayoonesha ni waoga Hamasa iliooneshwa na HAMAS watoto wa kipalestina na wanawake wao ni uzalendo mzuri na ipo siku IPO siku ipo siku WANYAMA haww wataanguka ktk mikono ya wanaume wa KWELI
... Ottoman Empire ilikuwa na nafasi nzuri sana kuwamaliza kabisa Israel lakini ndio hivyo bahati mbaya haikuwezekana. Will take millennia matamanio yako at least kuwa ndoto!
 
kwa majengo yaliyoharibiwa Gaza, hasara yake ni kubwa mno, vifo zaidi ya 200 wakati israel 12 tu.
Hizo taarifa za madhara waliyoyapata wa izrael ni za uongo wamepata madhara makubwa sana na wao hawakuona umuhimu wa kucheza na media na kujilizaliza bali kupambana kwa ajili ya wananchi wema wa nchi zote mbilo

Kumbuka hii vita ilitengenezwa na kuratibiwa na baadhi ya mataifa ya kiarabu na izrael kwa mfumo wa kisasa wa technolojia alikuwa anawaona kila kitu

Kitendo cha kushusha jengo la aljazeera ni ushahidi tosha kabisa kuwa aliona jinsi vyombo hivyo vilivyokuwa ninashiriki kuandaa propaganda na kutumia ofisi hizo kuhifadhi na kurusha makombora dhidi ya izrael kwa kisingizio cha uhuru wa habari

Ukitaka kuona aljzeera ni MAZANDIKI ni kuwa hawajawahi kitoa taarifa yoyote ya madhara waliopata izrael
 
Back
Top Bottom