Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Hivi Israeli na USA kama hii vita imewashinda,si waachane nayo wakajipange upya??
Ushindi wa vita ni kutimiza malengo, malengo wa israel na us ilikua kuutoa huu utawala wa iran na kuweka utawala mwingine ambao watakua na total control nao kama wanavyofanya nchi zingine, au kama hapo nyuma iran kipindi cha mohammed reza maana yule shah alikua puppet wa marekani tu anafanya kila wanachotaka ndo maana alivyotoka madarakani 79, marekani hajawahi kutaka amani na iran tena

Israel na marekani walishindwa hii vita wiki ya kwanza tu ya vita, maana target yao baada ya maandamano makubwa iran mwaka jana ya wananchi kutaka kuutoa utawala wa iran, wakaona hii ndo fursa, wamuue ayatollah wakidhani raia wataingia barabarani kuupundua uongozi wa iran kama kawaida wafanye mpango wa kuchomeka puppets wao, ndo maana baada ya kifo cha ayatollah trump aliwaambia wairan " the country is now yours to take"

Wakiwa bado wanashangaa mbona raia hawana muamko, likatokea janga la shule ya wasichana kushambuliwa na kuua watoto wengi, big mistake, serikali ya iran ikatumia hii kama propaganda kuonyesha umma kwamba adui yetu ni mmoja(israel and us).... wananchi wakaonekana tena kuiunga mkono serikali kuzuia uvamizi.... japo marekani alikana kuhusika na lile shambulizi lakini wenzetu western nachowapenda kuna uhuru na uwazi sana, uchunguzi ulifanywa na taasisi nyingi tu za us zikatangaza kua us ndo kafanya lile shambulio

Vita ni kama drafti, baada ya ile kete ya kumuondoa ayatollah na kutegemea raia kuanza kupambana na serikali yao kufeli hapo wengi tulijua ITS GAME OVER... hii kete waliitegemea sana nadhani hawakua na strong plan b mkononi..... hii vita hata wafanye vipi itabidi wakubali kushindwa tu maana target ilikua kuitoa iran regime madarakani, naona sasa wanahamisha kua ilikua kuharibu nuclear enrichment plants

Tuangalie vita ya vietnam, us alipigana vita ya miaka mingi na official war data zinaonyesha alipoteza wanajeshi takribani 60000 wakati north vietnam walipoteza zaidi ya laki 8, lakini official war statement zinadeclare ushindi kwa vietnam maana us alishindwa kutimiza primary objective yake ya kuzuia u communist vietnam..... unaua watu wengi ila hutimizi lengo, maana yakr unakua umeshindwa....

Rejea vita ya afghanstan, japokua us iliua waafghnstan wengi sana na kuweka kambi zake nchini kwa zaidi ya miaka ishirini lakini official war status inawatambua taliban kama washindi wa vita, japokua wao ndo waliuliwa wengi na kushindwa kwa kila kitu mpaka wakawa wanakaa mafichoni na ukimbizi, unajua kwanini, primary objective ya us ilikua kutoa utawala wa taliban madarakani, sasa after 20 years unaondoka taliban anarudi madarakani unakua umefanya nini sasa....

Sipendi ushabiki wa vita, ila ukweli ni kua israel na us wamemzidi mbali sana iran kivita, huwezi kupigana na adui ambae ana control airspace yako anaingia kwako anapiga anavyotaka anaondoka..... ndo maana iran kaamua kufanya hii vita iwe ya kiuchumi, ndo maana anakomaa na ile strait maana ndo karata yake kubwa, anakubali kuumia lakini na yeye anaona ni bora dunia yote iumie watu wapaze sauti us na israel waachane na hii vita....

Iran alishatoa onyo kua akivamiwa lazima afunge ile strait, ndo maana nasema us na israel hawakua na plan b kabisa walijua wakimuua ayatollah raia watapindua serikali wachomeke watu wao, marekani akitaka total win ya hii vita anabidi apeleke wanajeshi wake ardhini(boots on ground)... huwezi kutake total control ya nchi ukiwa juu tu, utaishia kuharibu miundombinu, kuua viongozi waandamizi na raia bure and then what???

Ila kwa wanaojua jeografia ya iran na aina ya jeshi lake la ardhini, marekani akisema aingize wanajeshi ardhini aisee watapata casualties nyingi sana....

No one is winning hapa, naona marekani watajitangazia ushindi tu kua wameharibu nuclear enrichment plants tu waachane na vita, ila ndo watakua wamewapa kiburi iran maana iran ita focus kwenye kuunda silaha na sea mines za kulinda strait of hormuz kwa gharama kubwa sana maana wanajua ndo roho yao ilipo

Ila huwezi kujua maana lolote linaweza kutokea maana trump nae ni kichaa aliyechangamka
 
Hivi Israeli na USA kama hii vita imewashinda,si waachane nayo wakajipange upya??
Ingekua wao ndio wanaamua iishe siku nyingi Tu ingeshaisha, the issue is Iran hataki iishe, zaidi ya wiki sasa vita ishabadilika Iran ndio yupo offensive mode.

Kila siku ikifika usiku Wanatuma mawimbi mawili ama matatu Israel, wakiamka wanaenda kuokoa mchezo unaendelea tena usiku unaofuatia.
 
Iran imesema kuwa vikosi vyake vya kijeshi vimeshambulia vyombo sita vya kijeshi vya Marekani, na kusababisha kuuawa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani waliowataja kama magaidi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa Ijumaa na Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), mashambulizi hayo ni sehemu ya awamu ya 84 ya operesheni iitwayo “Ahadi ya Kweli 4”.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa jeshi la majini la IRGC lilifanya mashambulizi ya usahihi dhidi ya malengo ya Marekani na Israel katika bandari ya Al-Shuwaikh pamoja na fukwe na bandari ya Dubai, likilenga wanajeshi wa Marekani na vifaa vyao vya kijeshi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo ilihusisha matumizi ya makombora ya masafa marefu (ballistic missiles) pamoja na makombora ya cruise aina ya Qadr 380. Vyombo sita vya kutua vikosi (LCU) vya Marekani viliripotiwa kupigwa katika bandari ya Al-Shuwaikh, ambapo vitatu vilizama na vingine vinaendelea kuungua.

Aidha, Iran ilisema ilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya maeneo ya kukusanyika wanajeshi wa Marekani, ikiwemo ufukweni na katika moja ya hoteli jijini Dubai, na kwamba malengo hayo yalipigwa kwa usahihi mkubwa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mbali na kuharibiwa kwa vyombo hivyo vya kijeshi, idadi kubwa ya wanajeshi wa Marekani waliuawa katika operesheni hiyo.

Source;Salim kikeke
 
Wale wanajeshi wa parachutu 5000 wameshaanza kupunguzwa tayari baada ya kutua middle East,wameshabaki 3100 wakijichanganya kuingia Iran yanarudi majeneza 3100 Marekani
 
Back
Top Bottom