US ametumia tomahawks cruise missiles 850 kwenye hii vita na Iran ambayo imechukua zaidi ya mwezi.
Tukumbuke USA walitumia tomahawks 802 kwenye vita na Iraq ya mwaka 2003, Kule Yugoslavia walitumia tomahawks kama 200 au zaidi, Libya walitumia tomahawks 124 ile mwaka 2011 walipoangusha serikali ya Gaddafi.
Kiufupi ni kwamba katika vita zote ambazo USA amepigana middle east na duniani kote toka awe na hio cruise missiles za masafa marefu ambapo ni silaha muhimu sana kwao na ya kipekee(tomahawk) basi amevunja rekodi kwa kuzirusha nyingi zaidi kwenye hii vita na Iran.
Iran ndio nchi imeshambuliwa kwa tmahawks nyingi zaidi kwa vita ya mara moja.
Tomahawks ni cruise missiles zina usahihi mkubwa, ni aina ya silaha muhimu sana kwa jeshi la USA.
Hizi tomahawks zinarushwa kwa njia tofauti, inaweza kuwa kwa ndege, nyambizi, meli n.k...
Kwenye hii vita USA wamejikuta wanatumia tomahawks nyingi zaidi hadi zinaelekea kuisha, ndipo wakaanza kutumia gravity bombs, huwa wanachukua hizo gravity bombs wanaziwekea JDAM.
GBU 24 au GBU 31 ni gravity bombs, ni kama mawe, yakiaciwa na ndege kama B-52, au B-1B, au F-15, basi yanashuka kama yalivyo, ila wanaongeza JDAM ili kuyapa precision nzuri na pengine kuyafanya yaende kwa umbali flani.
Baada ya tomahawks kuelekea kuisha , ilibidi US waanze kutumia gravity bombs na kuyafunga JDAM, halafu ndipo wanatumia B-52s , B-1Bs na F-15E.
Kulifunga bomb kifaa cha JDAM inasaidia kukaa mbali kiasi kutoka kwenye target ili kuepuka kushambuliwa, lakini gravity bomb linapokosa hiko kifaa ili ulenge target huna budi kupita juu sambamba na target, kitu ambacho ni hatari.
Sasa issue ni kwamba mzee mzima US , tomahawks ziliisha, wakaanza kutumia gravity bombs na kufunga JDAM, ukishafanya hivyo huna budi kuikaribia target kwa ukaribu zaidi na kuachia bombs.
Ndipo hapo hizi siku za mwishoni tukaanza kusikia ndege za US zinapigwa kama maembe, baada ya muda ikabidi US waiombe sana Pakistan kuandaa mazungumzo. Maana F-15E zingeendelea kupigwa kila leo na hadi sasa B-52s zingeshapigwa.
Hizi F-15E ndio ndege ina nguvu zaidi kuliko jet yeyote ya kivita katika model yake, Israel ndipo huitumia kama bomber yao.
Kwa mtu asiyelewa concept ya gravity bomb na JDAM, ni kama baiskeli kwa kawaida haina engine, hivyo lazima uendeshe kwa nguvu zako, sasa unakuja kusikia kuna kifaa cha umeme kama motor ukikifunga wewe ni kuendesha baiskeli kama pikipiki, hio ndio JDAM, ni kifaa kinafungwa kwenye bomb la kuangusha na ndege halafu linakuwa linasafari kwa umbali flani na kulenga kwa usahihi ikitumika GPS n.k. Pasipo kufunga JDAM hilo bomu halina tofauti na pipa lililojaa mlipuko. Ambapo ukilirusha kutoka kwenye ndege linashuka kama jiwe, ili liende umbali zaidi hata kilomita 30 ama 40 toka ulipoliachia ndipo inafungwa JDAM.
US ameziuza sana hizo tomahaks kwa baadhi ya nchi, na jamaa kiukweli wanapiga pesa sana,
Japan kuna wakati fulani waliomba hizo tomahawks wauziwe na US, walitoa order ya tomahawks 400, hizi tomahawks zina models tofauti tofauti tokana na matumizi, na kuna hadi zilikuwepo tomahawks zina nuclear hapo zamani baadae wakaachana na hizo za nuclear.
Baada ya Japan kutoa order mwaka 2023 , US walisema watawauzia Japan tomahawks 400, ambapo 200 ni block IV na 200 zingine ni block V kwa gharama ya dola bilioni 2.35, Sasa hapo juzi huu mwezi wa April, US wamesema order ya Japan itachelewa tokana na vita inayoendelea kati yake na Iran.
Kibaya zaidi kingine kilichopelekea US kuomba ceasefire ni ile siku ya passover ambapo Iran walifanya mashambulizi makali zaidi na mfululizo kuliko hata ile siku Khamenei ameuawa. Kitu ambacho kilionyesha dhahiri Iran bado wana makombora mengi zaidi kitu ambacho kilikuwa ni tishio.
Jambo lingine ni hilo la ndege za US zilipoanza kupigwa baada ya kuanza kusogea zaidi ndani ya anga la Iran ili warushe hayo ma gravity bombs, kipindi cha tomahawks ndege inaweza kukaa mbali na target hata kilomita 300 na bomb na missile ikapiga target, lakini kwa haya ma gravity bomb inawalazimu marubani wasogeze ndege karibu walau kilomita 50 karibu na target, na hapo ndipo wakaanza kudunguliwa.
Na wangekamatwa hao mateka hali ilikuwa mbaya sana kwa Trump.
Kiufupi watu wengi hii vita hawaelewi, lakini tulikuwepo hapa tukawaambia Iran bado wana nuclear na haijaharibiwa, ipo chini kwenye milima, walikuja wabishi humu balaa, eti nuclear ya Iran imepigwa, haya sasa Trump na Netanyahu mbona wanalia tena kuna kilo zaidi ya 400 za uranium?
Hata hili nililosema hapa kuhusu US kutumia gravity bombs kuna wajinga watabisha halafu kesho ukweli utakuja kuelezwa, maana msema ukweli yupo mbele ya muda.
Trump aliwadanganya kwamba wameishambulia Iran nuclear facilities na kuirudisha nyuma miaka kadhaa kwenye urutubishaji, hata mwaka hujapita Trump huyu hapa akilia kuhusu uranium.