Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

US ametumia tomahawks cruise missiles 850 kwenye hii vita na Iran ambayo imechukua zaidi ya mwezi.

Tukumbuke USA walitumia tomahawks 802 kwenye vita na Iraq ya mwaka 2003, Kule Yugoslavia walitumia tomahawks kama 200 au zaidi, Libya walitumia tomahawks 124 ile mwaka 2011 walipoangusha serikali ya Gaddafi.

Kiufupi ni kwamba katika vita zote ambazo USA amepigana middle east na duniani kote toka awe na hio cruise missiles za masafa marefu ambapo ni silaha muhimu sana kwao na ya kipekee(tomahawk) basi amevunja rekodi kwa kuzirusha nyingi zaidi kwenye hii vita na Iran.

Iran ndio nchi imeshambuliwa kwa tmahawks nyingi zaidi kwa vita ya mara moja.

Tomahawks ni cruise missiles zina usahihi mkubwa, ni aina ya silaha muhimu sana kwa jeshi la USA.

Hizi tomahawks zinarushwa kwa njia tofauti, inaweza kuwa kwa ndege, nyambizi, meli n.k...

Kwenye hii vita USA wamejikuta wanatumia tomahawks nyingi zaidi hadi zinaelekea kuisha, ndipo wakaanza kutumia gravity bombs, huwa wanachukua hizo gravity bombs wanaziwekea JDAM.

GBU 24 au GBU 31 ni gravity bombs, ni kama mawe, yakiaciwa na ndege kama B-52, au B-1B, au F-15, basi yanashuka kama yalivyo, ila wanaongeza JDAM ili kuyapa precision nzuri na pengine kuyafanya yaende kwa umbali flani.

Baada ya tomahawks kuelekea kuisha , ilibidi US waanze kutumia gravity bombs na kuyafunga JDAM, halafu ndipo wanatumia B-52s , B-1Bs na F-15E.

Kulifunga bomb kifaa cha JDAM inasaidia kukaa mbali kiasi kutoka kwenye target ili kuepuka kushambuliwa, lakini gravity bomb linapokosa hiko kifaa ili ulenge target huna budi kupita juu sambamba na target, kitu ambacho ni hatari.

Sasa issue ni kwamba mzee mzima US , tomahawks ziliisha, wakaanza kutumia gravity bombs na kufunga JDAM, ukishafanya hivyo huna budi kuikaribia target kwa ukaribu zaidi na kuachia bombs.

Ndipo hapo hizi siku za mwishoni tukaanza kusikia ndege za US zinapigwa kama maembe, baada ya muda ikabidi US waiombe sana Pakistan kuandaa mazungumzo. Maana F-15E zingeendelea kupigwa kila leo na hadi sasa B-52s zingeshapigwa.

Hizi F-15E ndio ndege ina nguvu zaidi kuliko jet yeyote ya kivita katika model yake, Israel ndipo huitumia kama bomber yao.

Kwa mtu asiyelewa concept ya gravity bomb na JDAM, ni kama baiskeli kwa kawaida haina engine, hivyo lazima uendeshe kwa nguvu zako, sasa unakuja kusikia kuna kifaa cha umeme kama motor ukikifunga wewe ni kuendesha baiskeli kama pikipiki, hio ndio JDAM, ni kifaa kinafungwa kwenye bomb la kuangusha na ndege halafu linakuwa linasafari kwa umbali flani na kulenga kwa usahihi ikitumika GPS n.k. Pasipo kufunga JDAM hilo bomu halina tofauti na pipa lililojaa mlipuko. Ambapo ukilirusha kutoka kwenye ndege linashuka kama jiwe, ili liende umbali zaidi hata kilomita 30 ama 40 toka ulipoliachia ndipo inafungwa JDAM.

US ameziuza sana hizo tomahaks kwa baadhi ya nchi, na jamaa kiukweli wanapiga pesa sana,

Japan kuna wakati fulani waliomba hizo tomahawks wauziwe na US, walitoa order ya tomahawks 400, hizi tomahawks zina models tofauti tofauti tokana na matumizi, na kuna hadi zilikuwepo tomahawks zina nuclear hapo zamani baadae wakaachana na hizo za nuclear.

Baada ya Japan kutoa order mwaka 2023 , US walisema watawauzia Japan tomahawks 400, ambapo 200 ni block IV na 200 zingine ni block V kwa gharama ya dola bilioni 2.35, Sasa hapo juzi huu mwezi wa April, US wamesema order ya Japan itachelewa tokana na vita inayoendelea kati yake na Iran.

Kibaya zaidi kingine kilichopelekea US kuomba ceasefire ni ile siku ya passover ambapo Iran walifanya mashambulizi makali zaidi na mfululizo kuliko hata ile siku Khamenei ameuawa. Kitu ambacho kilionyesha dhahiri Iran bado wana makombora mengi zaidi kitu ambacho kilikuwa ni tishio.

Jambo lingine ni hilo la ndege za US zilipoanza kupigwa baada ya kuanza kusogea zaidi ndani ya anga la Iran ili warushe hayo ma gravity bombs, kipindi cha tomahawks ndege inaweza kukaa mbali na target hata kilomita 300 na bomb na missile ikapiga target, lakini kwa haya ma gravity bomb inawalazimu marubani wasogeze ndege karibu walau kilomita 50 karibu na target, na hapo ndipo wakaanza kudunguliwa.

Na wangekamatwa hao mateka hali ilikuwa mbaya sana kwa Trump.

Kiufupi watu wengi hii vita hawaelewi, lakini tulikuwepo hapa tukawaambia Iran bado wana nuclear na haijaharibiwa, ipo chini kwenye milima, walikuja wabishi humu balaa, eti nuclear ya Iran imepigwa, haya sasa Trump na Netanyahu mbona wanalia tena kuna kilo zaidi ya 400 za uranium?

Hata hili nililosema hapa kuhusu US kutumia gravity bombs kuna wajinga watabisha halafu kesho ukweli utakuja kuelezwa, maana msema ukweli yupo mbele ya muda.

Trump aliwadanganya kwamba wameishambulia Iran nuclear facilities na kuirudisha nyuma miaka kadhaa kwenye urutubishaji, hata mwaka hujapita Trump huyu hapa akilia kuhusu uranium.
Na vita hii kuna Cruise missile nyingi zimedondoshwa intact, subiria miaka 2 Tu utaskia copy zake za dola 7000 zinazokuwa attached kwenye drones.
 
Kuna mtu anaweza kunambia sababu ya msingi ni kwanini Marekani hataki Iran asimiliki silaha za nyuklia?
Iran lilikua koloni la USA kwa Muda mrefu mno, Shah walikua ma puppet waligawa kila kitu kuanzia mafuta, Hadi Ardhi.

Kuna kipindi miaka ya 50-60 Iran walitoka kwenye utawala wa Shah na kumchagua waziri Mkuu Mosadegh ambaye alipendwa na wananchi na kuanza kurudisha mafuta ya Iran kwa wananchi, kupitia CIA walimpindua na kurudisha utawala wa kidikteta wa Shah tena.

So Toka Mapinduzi ya 79 ya kiisilamu Marekani inawauma Sana, wamekosa mafuta na source kubwa ya Rasilimali watu, wanasayansi wengi wa USA kipindi hicho walitoka Iran.

So chochote kinachoifanya Iran iwe strong ina maana dream ya USA kumiliki tena Iran inapotea. Ndio maana Muda wote wanaiwekea vikwazo na kudhoofisha kwa namna yoyote Ile.
 
Iran imekuwa threat sana kwa wauzaji wa silaha US, viwanda vya silaha US wanaiona Iran ni threat, kwanini? Jamaa wanatengeneza billions/trillions of money kutengeneza na kuuza silaha, interceptor kama SM-3 inafika dola milioni 30.

Yaani missile ya kuirusha ikalipuke inauzwa dola milioni 30, tomahawk inafika dola milioni 2 hadi dola milioni 2.5, kiufupi jamaa biashara ya silaha inawapa ukwasi wa ajabu.

Iran sasa anakuja na njia mbadala ambapo ana silaha zake kama hizo drones na baadhi ya missiles ambazo gharama yake ipo chini ukilinganisha na uwezo yaliyonayo.

Kwa hii vita iliyotokea inapelekea wateja wa US wa silaha waanze kujitafakari, mfano mzuri gulf states ambao walikuwa wateja wazuri wa US made air defende systems ambazo zinauzwa mamilioni ya dola na badala yake haijasaidia zaidi ya kuzidiwa na mashambulizi na kuishiwa interceptors tokana na uchache halafu ni gharama.

Imebidi hadi Zelensky apeleke specialists wakawasaidie waarabu jinsi ya kupambana na drones za Iran, maana njia wanayoitumia Ukraine ni nafuu zaidi.

Hata kwenye mashambulizi nchi nyingi sasa wataanza na wao kuwekeza zaidi kwenye makombora zaidi maana ni gharama nafuu na ni silaha hatari. Pia tutegemee nchi nyingi zaidi kuanza kutengeneza bases chini ya milima. Kiufupi hata China watafanya hivyo kama bado ukiachana na Pakistan, India, Afghanistan n.k

Iran imekuwa threat na kufanya silaha za US kuonekana kituko... Iran imegeuza muelekeo wa vita duniani..
Zelensky mwenyewe tapeli Tu vitu alivyopewa alinde vyote vimepigwa, wataalam wake wakafkuzwa Dubai.
 
Iran lilikua koloni la USA kwa Muda mrefu mno, Shah walikua ma puppet waligawa kila kitu kuanzia mafuta, Hadi Ardhi.

Kuna kipindi miaka ya 50-60 Iran walitoka kwenye utawala wa Shah na kumchagua waziri Mkuu Mosadegh ambaye alipendwa na wananchi na kuanza kurudisha mafuta ya Iran kwa wananchi, kupitia CIA walimpindua na kurudisha utawala wa kidikteta wa Shah tena.

So Toka Mapinduzi ya 79 ya kiisilamu Marekani inawauma Sana, wamekosa mafuta na source kubwa ya Rasilimali watu, wanasayansi wengi wa USA kipindi hicho walitoka Iran.

So chochote kinachoifanya Iran iwe strong ina maana dream ya USA kumiliki tena Iran inapotea. Ndio maana Muda wote wanaiwekea vikwazo na kudhoofisha kwa namna yoyote Ile.
Shukrani sana kwa maelezo yako ya kina mkuu
 
Mbona naona kama mpigaji alimiss target!
Ukiangalia mwanzo yes, then wanarudia mara ya pili huku wamezoom na kuzungushia lilipotua ndio kuna concetration ya watu na unaona watu kama wanaelea hawaendi tena walipokua wanaenda mwanzo

Wataalam watatusaidia model ya Hilo shell bomb, ila la kawaida kabisa unakuta kill radius ni Mita 50 na sharpnell zinaenda mbali zaidi, so hao wa karibu probably wote ni marehemu na wa mbali majeruhi wa kutosha.
 
Kuna mtu anaweza kunambia sababu ya msingi ni kwanini Marekani hataki Iran asimiliki silaha za nyuklia?
Mkuu hii elimu ipo unaweza kujisomea mtandaoni...baada ya marekani kulitumia bomu hilo la nuclear kwenye vita ya pili ya dunia dhidi ya japan..

Kutokana na athari ya silaha hyo,mwaka 1970 umoja wa mataifa ulipitisha azimio la kutoendelezwa kwa silaha hyo hatari duniani..kwa maana ya kutoruhusu nchi nyingine duniani kuimiliki..maana yake zile nchi ambazo tayari zinamiliki zibaki vile vile na nchi ambazo hazimili zisiweze kumiliki silaha hyo hatari ya nuclear.

Hivyo basi Irani ilikuwa ni moja wapo ya nchi iliyo tia saini mkataba huo wa kukubali kutomiliki hyo silaha ya nuclear pamoja na nchi nyingine ambazo mwa wakati huo.

Nadhani umenielewa japo kwa ufupi,,zaidi unaweza kwenda kujisomea
 
Nimekuelewa vizuri sana mkuu. Ingawa hii sheria ina ukakasi chake maana ninaamini baada ya hii convention mataifa yaliyokuwa na hii silaha yaliendelea kulimbikiza stock zao au kuna baadhi ambayo hayakuwa nazo yaliweza kuzipata namna tofauti kwa sababu za kiusalama pia.

Ilitakiwa waliokuwa nazo waziangamize ili dunia isiwe na nyuklia kabisa.
 
Ni kweli mkuu,mfano israel na pakistani hawakusaini ila waliweza kulimiliki hilo bomu baadae.
 
Kimenuka
Hakuna kulala

1776535883024.png
 
Netanyahu ni tatizo kwa dunia, huyu jamaa auawe ili dunia itulie, huyu shetani ndiye tatizo maana Trump anamsikiliza huyo shetani.

Hilo jamaa lina roho mbaya, hajali chochote kuhusu maisha ya watu nauchumi wa dunia.

Kwenye mkutano wa Islamabad wa upatanishi, JD Vance kila muda alikuwa akiongea na Netanyahu kwa simu.
 
Iran will prioritise vessels that pay in the Strait of Hormuz
“Given the limitation on the number of vessels that will be allowed to pass, Iran has decided to give priority to those vessels that respond more quickly to the new Strait of Hormuz protocols and pay the costs of security and safety services,” a senior Iranian official told CNN today.
The vessels that don’t pay, the official said, will be “postponed”. Aljazeera

Hi Kauli Imenifurahisha sana aisee, Hakuna unyonge
Back to square one
Baada ya Trump kuropoka hovyo posture ya Iran imebadilika tofauti na ilivyotarajiwa
Kila mtu amejiandaa vilivyo everything is replenished for the next round.
 
Back
Top Bottom