Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Swali langu tena nalirudia pasipo kujali hali inayo endelea mashariki ya kati kwa sasa.

Kwa nini mfumo wa siasa wa Iran ina ruhusu mpasuko mkali wa ndani tena wenye athari kubwa kati reformists[ Western lover & sympathiser] na conservatives ?
 
View attachment 3550324

Iran wamepiga na kituo cha kusafishia maji Mitaa kadhaa Tel Aviv kuna mafuriko.
Safari hii lazima waipate..
Mimi kifo cha Ayatollah nilitegemea kabisa na hata sijashangaa.. wala kushtuka. KWa wasio elewa wanadhani ni ushindi kwa Israel, huku wakiandaa videos za propaganda mitaani kwamba wananchi wanashangilia kifo cha Ayatollah..

Hii mipango yote inapangwa kimkakati sana na Israel pamoja na US... imeandaa na vikundi mtaani kufanya hizi cheap propaganda..
 
Swali langu tena nalirudia pasipo kujali hali inayo endelea mashariki ya kati kwa sasa.

Kwa nini mfumo wa siasa wa Iran ina ruhusu mpasuko mkali wa ndani tena wenye athari kubwa kati reformists[ Western lover & sympathiser] na conservatives ?
Hakuna western lovers Bali kuna wairan ambao wanampenda Ayatollah na wengine ambao wanajiendesha kisecular, ila wote kwa pamoja Wairan ni watu ambao wapo proud Sana na identity Yao. Na bila kuweka mfumo inclusive kwa ajili ya Wairan wote ni ngumu nchi kuendelea.

Bunge Lao, viongozi wao wengi wapo ambao sio pro Ayatollah ila ukifanya inclusion inasaidia sana kwenye nchi.
 
Swali langu tena nalirudia pasipo kujali hali inayo endelea mashariki ya kati kwa sasa.

Kwa nini mfumo wa siasa wa Iran ina ruhusu mpasuko mkali wa ndani tena wenye athari kubwa kati reformists[ Western lover & sympathiser] na conservatives ?

Usaliti.

Iran inafanyiwa fitina na njama kijeshi ,kisiasa na kiuchumi ili ianguke na US/Israel aweke pandikizi lake.

Iran kuna hadi wanasayansi walikamatwa wakiwa wanavujisha taarifa za siri kuhusu projects zao za nuclear..
 
Hili sio tukio la kwanza wala la pili. Kwa muda mrefu Israel anaingia anaua wanasayansi anavyotaka. Bado mtu anakwambia wapo mzani sawa

Iran inatakiwa kuinvest kwenye intelligency
 
Hawa ndio wanao muamini marekani mara nyingi na danganya toto zake mwisho wa siku anawapa za uso O.K nimekuelewa
 
Usaliti.

Iran inafanyiwa fitina na njama kijeshi ,kisiasa na kiuchumi ili ianguke na US/Israel aweke pandikizi lake.

Iran kuna hadi wanasayansi walikamatwa wakiwa wanavujisha taarifa za siri kuhusu projects zao za nuclear..
Hilo tayari ni tatizo la kuonesha adui yako kakuzidi kete upande huo mpaka kuweza kukuingilia kirahisi hivyo
 
mosad mashariki ya kati kote wamejaa mpaka chooni
 
Iran inayahitaji mabomu yote machafu ikiwemo nyuklia kwa usalama wake kuliko hayo mabomu yanavyo muhitaji Iran fatwa za kidini haziwezi wafikisha popote nilisema kabla, nasema sasa na nitaendelea kusema kama watasalimika round hii tena kama walivyo salimika awali.
 
Eneo Iran alilopo na siasa zake na madui zake alionao sina hakika kama huo mpasuko una afya yoyote ile zaidi utakuwa una wakaribishia matatizo tu yasiyokwisha.
 
Vipi huko Iran nasikia nyoka kakatwa kichwa ni kweli au western propaganda?
 
Unacho sema ni kweli, niliwai kuona Rais wao Mstafu yuko mtaani anachunga mbuzi
 
Hawa ndio wanao muamini marekani mara nyingi na danganya toto zake mwisho wa siku anawapa za uso O.K nimekuelewa
Usiangalie nchi Kwa upande wa vita Tu. As I said comments kibao humu, miaka ya 70 sector nyingi kuanzia kielimu Hadi Afya tulikua tumewapita Iran, pamoja na vikwazo walivyowekewa ila Leo sio wenzetu.

Iran ni nchi ambayo ipo top 20 Duniani kisayansi, ina rank kama Nchi ya 3 Duniani kuproduce Ma Engineer, toka Karne ya 21 hakuna Nchi yoyote Duniani ambayo imekua kisayansi kwa haraka Sana kushinda wao, sekta nyingi za Kielimu, Afya etc zinakua kwa Kasi,

hio Elimu na ukuaji kisayansi havitokani na kubagua raia wako, Bali inabidi utoe Elimu kwa wote, upate ma Genius wa kuwaendeleza ili waje kuwa wanasayansi wakubwa kuipeleka nchi mbele, Iran pengine ndio nchi pekee ambayo inatoa Elimu ya kisasa ya bure kwa wakimbizi.

So inakuja na disadvantage kama hizo ni rahisi Ku infiltrate ila usi ignore faida nyengine, wangetemea Tu Jeshi la kiisilamu pengine wangekua Leo wanatumia makombora Urusi na China.
 
Iran naikubali kwa mengi sana tu lakini kuna mambo baadhi sifurahishwi toka kwao hivyo ndivyo jinsi nilivyo kwangu Iran sio kila kitu sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…