Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel sio Iran haiitaji Makombora 500 wala baliistic missiles 150.

Israel kila silaha yake inathamani
Hizo silaha zenye thamani hazijafanya maangamizi yeyote hakuna majeruhi wala kilichoharibika.
Na hata vinu vya nuclear walivyolenga kulipua wamevikosa na vipo hapo hapo Isfahan.
 
Kuna kila dalili WWW3 inakwenda kuanza rasmi........na mwisho wa Israel unakaribia........kumbuka Amerika ameshasema yeye anakaa kando......
America yupi wa kukaa kando? Hujui mambo mengi wewe...! Subili uone.America huyu ambaye hataki hata Palestine ipate kiti UN? Democrats wanacheza na akili za voters tuu( Arab Americans). Marekani imemtafuta mda mrefu sana Iran...hapo wanakoleza moto chini chini tu. Kama huelew hata Saudi Arabia anachekelea sana anaomba ipiganwe vita rasmi kati ya Iran na Israel
 
taarifa zisizoegamia upande wowote zinasema miji saba ya Iran imepokea kichapo cha makombora ya chap chap na miundo mbinu kuteketea.
Hizo taarifa zisizoegemea upande wowote hazina hata vipicha picha mkongwe!? Au hata video?
Kama zipo, fanya kutuma hata link. Nikiwa kijiweni napiga ngenga kuhusu hizi mambo inabidi niwe na ushahidi kidogo, maana kuna vijana wengine wanapendaga stori zangu ziambatane na ushahidi kidogo.
 
Kuna kiongozi mkubwa Iran juzi kati hapa alisema marekani waliwatumia barua wakiomba Israel ijibu kwa kufanya shambulizi lisilo na madhara ndani ya Iran ili kuiondolea Israel aibu.

Naona ndicho kilichofanyika
Win to win situation... Ndo kitu kilichotokea hapo ila Israel akizidi zaidi ya hapo Marekani atakua kando kusoma mchezo
 
Bado upo chini kwenye kuelewa propaganda za kivita ndugu yangu......kwa watu wenye uelewa na mambo ya kivita hapo Iran kichwa kinamuuma na kuna maswali kibao anajiuliza.........
Siwezi kukupinga ama kukubaliana na wewe.
Ila kwa mimi Israel kichwa kinamuuma zaidi,maana Israel ni nchi ambayo bado inapitia vita kila leo.
Jumatano Hizbollah wameshambulia Galilee na kujeruhi watu saba.
Point yangu ni kwamba Israel amekaa vibaya sana katika huu mgogoro kiasi wananchi wao na baadhi ya viongozi wameshachoka na vurugu za kila leo.
Israel haina tofauti sana na Ukraine kila baada ya muda unasikia air siren mkuu.
Hii raia wameichoka.
Screenshot_2024-04-18-14-09-16-53_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
 
America yupo wa kukaa kando? Hujui mambo mengi wewe...! Subili uone.America huyu ambaye hataki hata Palestine ipata kiti UN? Democrats wanacheza na akiliza voters tuu( Arab Americans). Marekani imemtafuta mda mrefu sana Iran...hapo wanakoleza moto chini chini tu. Kama huelew hata Saudi Arabia anachekelea sana anaomba ipiganwe vita rasmi kati ya Iran na Israel
Saudi Arabia amekataa uwanja wake wa ndege vita kutumika dhidi ya Iran.
Saudi Arabia na Iran wana mahusiano ya kidiplomasia kama haujui.
Saudi Arabia hawezi kutaka jambo hilo hata mara moja labda utuletee ushahidi wa usemayo.
US iko nyakati mbaya sana red sea kazi haijakamilika na Ukraine bado kubichi hawezi jihusisha na vita inhine kiwepesi.
 
inaonekana ilikuwa very limited strike, haifikii hata kiwango kile iran ilifanya kwa israel, naona walikuwa kama wanatoa msg kuonyesha kuwa wanao uwezo wa kuingia hadi ndani ya nchi. nafikiri cha kuangalia ni kama watapiga tena au la, ila hadi sasa iran bado ni boss. alichofanya israel ni kama kupiga alimradi tu ili na yeye aonekane hakukubali kupigwa, na inaonekana baada ya hii, hawatarushiana tena, kila mtu atamheshimu mwenzake. ugomvi utaishia hapo na iran itaendelea kuogopwa kwamba sio ya kitoto. let truth be told.
 
Kila mmoja anaihofia vita mkuu.
Iran kwa jinsi ilivyo sio salama kuingia vitani ukweli usemwe,itaumiza sana raia wake.
 
Siwezi kukupinga ama kukubaliana na wewe.
Ila kwa mimi Israel kichwa kinamuuma zaidi,maana Israel ni nchi ambayo bado inapitia vita kila leo.
Jumatano Hizbollah wameshambulia Galilee na kujeruhi watu saba.
Point yangu ni kwamba Israel amekaa vibaya sana katika huu mgogoro kiasi wananchi wao na baadhi ya viongozi wameshachoka na vurugu za kila leo.
Israel haina tofauti sana na Ukraine kila baada ya muda unasikia air siren mkuu.
Hii raia wameichoka.View attachment 2967951
Labda Tu nikuambie.......vita ndio vinamuweka Israel huko tangu alipotangaza taifa lake.......kumekuwepo na majaribio kadhaa ya kuiondoa Israel upande huo lakini imeshindikana.......kwa lugha nyepesi Israel anakaa hapo kwa ngu u za kijeshi na msaada wa mataifa they nguvu duniani.......

Hivyo vita anapigania kila leo na bado anaendelea kuishi....... threat pekee Kwa Israel kwenye ukanda huo ni Iran pekee
 
Saudi Arabia amekataa uwanja wake wa ndege vita kutumika dhidi ya Iran.
Saudi Arabia na Iran wana mahusiano ya kidiplomasia kama haujui.
Saudi Arabia hawezi kutaka jambo hilo hata mara moja labda utuletee ushahidi wa usemayo.
US iko nyakati mbaya sana red sea kazi haijakamilika na Ukraine bado kubichi hawezi jihusisha na vita inhine kiwepesi.
Ngoja tusubili. Saudia analindwa na Marekani na ana base pale.
 
Back
Top Bottom