Bora useme ukweli , ukifuatilia nyuzi humu unaweza kucheka ...Utaona ushabiki maandazi , kama sisi sote ni watanzania lakini mawazo yetu yapo tofuati sio kosa kuwa upande fulani ila pia tuangalie na ukweli uko wapi .
Hii vita inapigana pale lakini naona wanaokejeliwa waislamu wengine kama ni jambo la ushabiki , kuna vita ya Russia na ukraine hawa wote ni wakristo ila Russia ni wakristo hasaa ...Lakini huoni watu wakiongelea vbaya ukristo kwa sababu Russia anaua watu wa ukraine ambao wote kiimani ni ndgu .
Zipo page za watu wanawakosoa na kuunga mkono pande moja wap na watu hao ni miongoni mwa waislamu, wakristo , hata jewish baadhi wanapiga kitendo cha israel .Tanzania ni ubishani maandazi wala hatujui chochote .
Tufike wakati tusisambaze chuki tubaki ukweli hata kama usem israel ni powerful ila hiyo vita wanagawana madhara na haijaanza leo , wengi humu ni wadogo vita wameikuta .
Mbaya zaidi hatuna uhakika wa kihistoria kamili maana kila mtu anadai pale ni kwake . Pia. swali la kujiuliza Palestine na israel wamefikaje pale mpaka wakawa na miji yao ?