Israel yasema shambulio la Yemen ni onyo kwa maadui zake wote wa mashariki ya kati

Israel yasema shambulio la Yemen ni onyo kwa maadui zake wote wa mashariki ya kati

Yote hayo nayafahamu, swali langu lililenga kupata maoni ya huyo niliemuuliza. Asante kwa kujibu.
Tusichokijua wangapi au kina nani?
Hata mimi nimeongea kauli ya kuuliza kwa kushangazwa,maana habari zilitapakaa kote.
Sijanena kwa ubaya.
 
Kama vichaa wa kiisrael wanafanya kweli basi Hizbollah asingeshambulia kaskazini kwa Israel kiasi wayahudi kuondoka makazi yao.
Kuondoka si kigezo cha kuhitimisha kushindwa.Kuondoka sehemu hakuna tofauti na kukwepa ngumi au kofi la mtu.Kwani mnapopambana,hata na mtu dhaifu,huwa harushi makonde?
 
Kuondoka si kigezo cha kuhitimisha kushindwa.Kuondoka sehemu hakuna tofauti na kukwepa ngumi au kofi la mtu.Kwani mnapopambana,hata na mtu dhaifu,huwa harushi makonde?
Upinzani umezidi zaidi kati ya Hizbollah na Israel.
Kadri Israel inavyoshambulia Lebanon ndivyo kadri Hizbollah inavyozidisha mashambulizi pia.
 
Kwa Misri hawakuwahi kupigana.
Ila kama watapigana vita itakua ngumu maana tabu kuu ilipo ni kuwa IRAN iko nyuma ya Houthi.
We hujiulizi nguvu ya makombora ya masafa marefu,vifaru na APC vehicles na bunduki zenye nguvu Houthi wanatoa wapi!?
Yani ili Houthi wafeli basi Iran isiingilie kati.
Najua wanapata full support toka iran. Alietoa hayo mawazo amesema houthi imesema itawapiga hao Waarabu wote, Soudia, Misri, Jordan,

Una maoni gani kuhusu hao Waarabu, je hawana watu nyuma yao ambao ni tishio kwa washirika wa houthi pia?
 
Upinzani umezidi zaidi kati ya Hizbollah na Israel.
Kadri Israel inavyoshambulia Lebanon ndivyo kadri Hizbollah inavyozidisha mashambulizi pia.
Kwani wewe ulitegemea watulie tu?Lazima waoneshe ukinzani wao.Ni wachezaji wawili uwanjani.Mmoja anajihami,na mwingine anataka ushindi.
 
Ndugu yangu unachukuliwa vita kama maigizo, hizo nchi za kiarabu na Afrika wakapigane na Israel kwa sababu ipi? kama drone za Yemen zinafika Israel wao IDF wanashindwaje kufika Yemen? Mbona akili zako ndogo , kama una akili kweli unaweza kuvamia nuclear states? Wewe dini inakusumbua, njoo tuwatetee wasidhani, wakongo wanaopigana, achana na mambo ya waarabu na wayahudi, kweli kama una akili Yemen ndo wakupiga Israel na kuishinda?
Madrasa
 
Najua wanapata full support toka iran. Alietoa hayo mawazo amesema houthi imesema itawapiga hao Waarabu wote, Soudia, Misri, Jordan,

Una maoni gani kuhusu hao Waarabu, je hawana watu nyuma yao ambao ni tishio kwa washirika wa houthi pia?
Mtu aliye nyuma yao ni huyo waliyemsaidia Israel na USA,UK.
Ila hiyo ni mikwara Houthi hawezi akipiga nchi zote hizo.
Labda ni mikwara tu ya kutishana.
Uvamie nchi tatu kwa mara moja sio kitu chepesi.
Ingekuwa Iran kama Iran ningesema inawezekana,ila Houthi ambaye anabebwa na Iran ni kitu kigumu haiwezekani.
 
Isreal ni bla bla nyingi kwanza hizo F35 mpaa zifike Yemen wanazo two option wapunguze uzito, wa maboom ndio zitafika Yemen, kama wakitumia njia ya Red Se.

Hao mimi na kwenda na wale walio sema hizo ndege zilizo piga ni za US, UK, Egypt na Saud Arabia. Israel bila kupewa green light watumie Air space ya Egypt na Saud Arabia ni vigumu kufika huko ndege zao bila kuwa refuel, na hizo ndege tulizo onyeshwa zina refuel sio za Israel eti zipo Red Sea, ni video zipo kwenye archive zao.

Option ya pili walitumia UAE kwenda ku attacked Yemen.

Huku na huku warabu wameshiriki kama kawaida zao wameruhusu ndege za Israel kutumia anga ya Jordani, Saud Arabia na Egypt Warabu na wafrica si watu wakuwamini,wakiona ngozi ya pink.

R.I.P commander wangu Robert Mgabe huyu ni katika wale wakristo 10% naheshimu misimamo yao, sio hivi vikristo njaa vinavyo amini bibilia ya Paulo na taifa teule lake

Hi video nzuri kwa waimba kwaya watazame vipi Mungu wa bibilia zaio.ni Racist 😄


View: https://youtu.be/kQI7WWCi-eQ?si=RG6Ku8g3825pzy2U

Hizi vita kuna kundi wanafaidika nalo, haiwezekani kila siku watu wanauawa na UN wapo kimya
 
Kwani wewe ulitegemea watulie tu?Lazima waoneshe ukinzani wao.Ni wachezaji wawili uwanjani.Mmoja anajihami,na mwingine anataka ushindi.
Nani anajihami na nani anataka ushindi!?
Japo nilitegemea kwa jinsi Israel inavyosifika basi Hizbollah ingeogopa na kutuliza vurugu.
 
Yemen kama kweli anauwezo kuliko Israel mpaka leo hii angeshajibu mapigo: Iran nae baada ya kupelekewa Moto angeshajibu mpaka sasa hivi... Usije ukajifariji UKWELI LAZIMA USEMWE Israel kutokana na rabsha za kila siku toka kwa Warabu wamekuwa na Uhodari na mbinu pamoja na Silaha za kutosha kujikinda
Iran ajibu kwani kafanywa nini mzee mbona unachanganya madawa
Kuhusiana na Yemen suala la kujibiwa nilazima watajibu
Kuhusiana na rabsha israhell hana rabsha zozote toka kwa waarabu nandio maana katulia
Ana rabsha wakati UAE SAUDIA nk wanamuuzia mafuta nk yanayomfanya aendelee kuitwanga ghaza
Zamani kweli alikumbana na rabsha za hapa na pale ila kwa sasa karelax sana anapewa upinzani na vikundi zamani alikua anapewa na nchi ama waarabu wengi kama sii wote
 
Mtu aliye nyuma yao ni huyo waliyemsaidia Israel na USA,UK.
Ila hiyo ni mikwara Houthi hawezi akipiga nchi zote hizo.
Labda ni mikwara tu ya kutishana.
Uvamie nchi tatu kwa mara moja sio kitu chepesi.
Ingekuwa Iran kama Iran ningesema inawezekana,ila Houthi ambaye anabebwa na Iran ni kitu kigumu haiwezekani.
Hiyo ni fact.
Kwa nini unahisi Iran ana uwezo wa kuwapiga misri, Jordan na saudia kwa pamoja?
 
Israel ilifanya shambulio lake la mwanzo kwa Yemen na kuiharibu vibaya bandari ya Hodeida nchini humo kwenye eneo linalodhitiwa na Houth.

Waziri wa ulinzi wa Israel,Yoav Gallant amesema shambulio hilo si kwa Houth pekee bali ni onyo kwa wote wenye uadui na Israel.Akaongeza kusema kuwa moto unaowaka Hodeada unashuhudiwa na watu wote wa mashariki ya kati.

Kinachoshangaza ni jinsi mataifa hayo ya mashariki ya kati wanavyochukulia kuwa shambulio hilo ni kwa Houth pekee wakati mayahudi wanakusudia kuwatisha wote.

Israel imeanza Gaza na ukingo wa magharibi,imeingia Yemen na itafanya kwengine kwa ubabe bila hao watawala wa mashariki ya kati kuzinduka.

Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuleta mabadiliko kwenye akili za watawala hao na kutamkwa kwake ni kipimo cha kibri cha Israel ikikaribia kuangamia kama ilivyotokea kwa firauni wakati alipozidi uadui na Mungu muda mfupi kabla ya kushikwa na kuangamizwa.

Baadhi ya wachambuzi wenye kufuatilia mizozo ya mashariki ya kati wamesema maamuzi ya Israel kuishambulia Yemen yanaweza kuwa sababu ya kuyapa nguvu makundi yanayopingana nayo na si kinyume chake.

Yemen's Houthi rebels vow open battle with Israel and the U.S., as fears rise of Mideast war

firauni sialitea kibri wana wa israili au hamkusomaga hivyo?
 
Kwamba ww una technical knowledge kuliko israel airforce ? Dude pls
kwanza F-35 wanazotumia F-35 ni modified kwa matumizi yao tu, wamechuku airframes waka install mifumo yao according to their needs. And hawana tu F-35 wana fleet kubwa ya ndege nyingine, so kwenye flight sortie hawa fly ndege aina moja.

Sisem israel is the best, but dont under estimate them na experience waliyo gain of all years
Kijana sikiliza kwanza nilicho ongea kiko wazi hakuna technology yoyote ile Israel anayo yaweza kupeleka F35 Al Houdaida, Yemen bila kurefuel.

Short distance akitumia njia ya Red Sea 2,350 KM karibu, wakati Iran ni 1750 KM, hata hio Iran anaweza kwenda na kurudi kwa shaka, na lazima awe kabeba silaha hazina impact kubwa.

Punguza mapenzi kijana ya kuisifu Israel, mimi kwenye mambo ya ndege za kivita hunizidi hata siku moja, nawala usidanganywe na mtu hakuna technology ambayo Israel anayo ya kumfikisha Al Hudauda bila ku Refuel.

Mwenye technology hawezi kuwazidi wale orignal maker, hawezi yeye kutengeneza F16 au kutengeneze F35 afu unamsifia kuliko USA. Israel akibahatika kumodify kwenye fuel consumption itakuwa ni 1/10 sio zaidi ya hapo, na akitaka izidi stage ya 3>-4/10 ya fuel consumption, nilazima afanye off-loading capacity ya orignal loading capacity ya F35 na hapo harudi ila kwa kibahati bahati ataishia kwenye bahari la Red Sea 😄
 
Hiyo ni fact.
Kwa nini unahisi Iran ana uwezo wa kuwapiga misri, Jordan na saudia kwa pamoja?
Kwanza kulingana na historia yake ya vita, pili kulingana na uwezo wake wa kijeshi.
Ndio maana hata mataifa ya kiarabu yalipoombwa bandari zake zitumike dhidi ya Iran zilikataa.
Iran pale middle east ana missile power kuliko taifa lolote.
Na missile power zote ziko active,tena makombora mengine yana uwezo wa kukwepa ADS na kuifikia target.
Pia ana stock ya kutosha.
Sio vya kuagiza kama Houthi.
 
Mfanano upo lakini indirectly kwa sababu Makundi tajwa yapo kwenye nchi na nchi hizo zinayakumbatia na kwa jinsi hiyo nchi yote inajumuishwa kama ndo inashambulia. e.g. HAMAS Wapo Palestina(Gaza) lakini Palestina haiwakatai, Houthi wapo Yemen na Yemen haiwakatai; kwa mantiki hiyo Yemen inajumuishwa kwamba ni Adui na inapigwa.
Iran ni mjanja anawasakizia Waarabu wenzake yeye katulia zake anaangalia ngoma inavyochezwa. Kutoa silaha au materials nyingine za kivita sio hoja sana kwani silaha na vitu bila Watu-Wapambanaji ni kazi bure. Iran anatoa mafunzo/anawafundisha mbinu lakini wanaofundishwa watafundishwa zaidi na IDF kwenye uwanja wa vita halisi.
Hakuna mfanano wa makundi na nchi na hautakuja uwepo
Mnataka mfananishe kufidia kushindwa kwa mzayuni
Nchi itaendelea kua nchi na makundi yataendelea kua makundi
Hamas wapo ila wao hawaelewani na fatah wapo nchi moja unawafananishaje na nchi?
Houthi wapo ila nchi imegawanyika kuna serikali zaidi ya moja hawa unafananishaje na nchi?
Walau hizbullah wao ni sehemu ya sirikali
Ila hakuwezi kukawa sawa baina ya nchi na kundi
 
Kwanza kulingana na historia yake ya vita, pili kulingana na uwezo wake wa kijeshi.
Ndio maana hata mataifa ya kiarabu yalipoombwa bandari zake zitumike dhidi ya Iran zilikataa.
Iran pale middle east ana missile power kuliko taifa lolote.
Na missile power zote ziko active,tena makombora mengine yana uwezo wa kukwepa ADS na kuifikia target.
Pia ana stock ya kutosha.
Sio vya kuagiza kama Houthi.
Nakubali wana siraha nyingi na uzoefu.
Linapokuja swala la kupigana na nchi 3 kwa wakati mmoja ni changamoto sana. Itamlazimu kuligawa jeshi lake kukabirina na majeshi ya nchi 3 kitu ambacho kitapunguza uwezo wake.

Ila kwa nchi moja moja nakubali hana mpinzani dhidi ya hizo nchi tatu.
 
Back
Top Bottom