Israel yasema shambulio la Yemen ni onyo kwa maadui zake wote wa mashariki ya kati

Israel yasema shambulio la Yemen ni onyo kwa maadui zake wote wa mashariki ya kati

Hakuna kitu kama hicho hakuna sehemu yoyote ndani ya Israel limetua kombora lolote la houthi tangu Israel Ishambulie
Wamepiga,raia walisema walisikia milipuko,jeshi likasema walidundua makombora ya houthi nje ya anga la Israel,hapa unajua kabisa IDF inadanganya,houthi kesho yake tu walianza kwa kubutua meli ya marekani kwa mvua ya drones na makombora,wakapiga na Israel
 
Hivi kuna ISRAEL ya kwenye media na ISRAEL halisi?
Ndio MKUU yakwenye media inaenda kupigana na mataifa saba kwa siku sita ila inashindwa na kagroup kwa mwaka mzima
Yakwenye media inaenda entebbe kuokoa mateka wake kwa masaa 24 ila inashindwa kuokoa mateka wake hapo mlangoni kwao kwa mwaka kasoro sasa
Nadhani umeiona israhell halisi naile ya kwenye media
 
Israel ilifanya shambulio lake la mwanzo kwa Yemen na kuiharibu vibaya bandari ya Hodeida nchini humo kwenye eneo linalodhitiwa na Houth.

Waziri wa ulinzi wa Israel,Yoav Gallant amesema shambulio hilo si kwa Houth pekee bali ni onyo kwa wote wenye uadui na Israel.Akaongeza kusema kuwa moto unaowaka Hodeada unashuhudiwa na watu wote wa mashariki ya kati.

Kinachoshangaza ni jinsi mataifa hayo ya mashariki ya kati wanavyochukulia kuwa shambulio hilo ni kwa Houth pekee wakati mayahudi wanakusudia kuwatisha wote.

Israel imeanza Gaza na ukingo wa magharibi,imeingia Yemen na itafanya kwengine kwa ubabe bila hao watawala wa mashariki ya kati kuzinduka.

Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuleta mabadiliko kwenye akili za watawala hao na kutamkwa kwake ni kipimo cha kibri cha Israel ikikaribia kuangamia kama ilivyotokea kwa firauni wakati alipozidi uadui na Mungu muda mfupi kabla ya kushikwa na kuangamizwa.

Baadhi ya wachambuzi wenye kufuatilia mizozo ya mashariki ya kati wamesema maamuzi ya Israel kuishambulia Yemen yanaweza kuwa sababu ya kuyapa nguvu makundi yanayopingana nayo na si kinyume chake.

Yemen's Houthi rebels vow open battle with Israel and the U.S., as fears rise of Mideast war

Hao Youth mpaka wanaichokonoa Islael ilikuwa imewafanya nini?
 
Israel huwa hawamtishi mtu awaye yote.Huwa wanatuma taarifa tu.Kwamba,nitakupiga huku tayari kakukung'unta unalialia.
Watu wameshajifunza zaidi na tangu zamani walikuwa wanajuwa kwani Allah aliyewaumba ameshatoa taarifa.
Hao waarabu wanebaki na ujinga na kiburi chao tu.Iko siku watachanganywa wote pamoja.
 
Inaua watu wasiokua na hatia pale ghaza na kuwaacha hamas
"Kwasababu ina nguvu kuliko hamas" (Russia v/s Ukrain?)
- Houth kwanini hawakuchaguwa kuisaidia Palestine waakimarishana huko huko ndani ya palestine ambako tayari moto ilikuwa ukiwaka, au walitaka kupanua eneo la mapigano?
 
Nakubali wana siraha nyingi na uzoefu.
Linapokuja swala la kupigana na nchi 3 kwa wakati mmoja ni changamoto sana. Itamlazimu kuligawa jeshi lake kukabirina na majeshi ya nchi 3 kitu ambacho kitapunguza uwezo wake.

Ila kwa nchi moja moja nakubali hana mpinzani dhidi ya hizo nchi tatu.
Point yako iko sawa kwenye vita ya kuvunja majumba, barabara, kuwauwa raia kweli Israel atawashinda lakini kwa vita haswa hanshindi hata mmoja.
 
Acha kuropoka narudia acha kuropoka.
Israel kabla ya kuvamiwa hiyo October 7 na Hamas August walikua wakipora mashamba ya Zaituni.
Pia ilikua ikivunja makazi ya watu huko Jenin ili ipanue makazi ya Wazayuni.
Na sasa hivi wameamua kuikata Jenin yote iwe sehemu ya Israel,ilhali hiko ni kinyume na makubaliano ya mipaka.
Au unatuchukulia sisi ni mazwazwa hatufuatilii kitu!?
Ndio ujiulize kwanini safari hii mataifa makubwa kama Spain,Brazil,Colombia,Belgium,Norway yameenda kinyume na Israel.
Wanajua fika vurugu hazikuanzia Oktoba 7.
Kipindi Israel kupitia IDF mnamo August inavunja nyumba za Jenin na kuwaacha Palestina hawana makazi dunia ilikaa kimya na katika habari ilikua inatangazwa.
Ila Hamas kulipiza kizazi Oktoba naona dunia imehamaki.
Wapuuzi wakubwa.
Mwanamke anapoandanana kudai haki sawa, ni kuwaonea tu wanaume, maana wanaume hawajawanyima haki yoyote

Wanawake wanapaswa kufahamu kwamba, wanayetakiwa kumdai hizo haki ni MUNGU, maana huyo ndiye aliyesema mwanaume ndiye kichwa cha familia basi..!

Mungu ndiye aliyesema, Mwanaume atamtawala mwanamke, wamdai yeye na siyo kuandamana wakitudai sisi wanaume

ukimkuta kiongozi kasimama kuungana na kelele hizo za wanawake wakidai haki hizo, ujue anataka kusimama kwenye nafasi ya MUNGU

Nataka kusema hivi..! MUNGU ndiye aliyewapa hiyo aridhi Waisrael

Hao Parestina wanapaswa kuandamana wamuulize huyo Mungu ni kwa nini aliwapa aridhi waisrael? JE wao waende wapi? Atawajibu

Sasa wewe, aidha unitukane mimi,, na au umtukane huyo Mungu aliyesema hivyo

Sasa kazi ni kwako
 
Nakubali wana siraha nyingi na uzoefu.
Linapokuja swala la kupigana na nchi 3 kwa wakati mmoja ni changamoto sana. Itamlazimu kuligawa jeshi lake kukabirina na majeshi ya nchi 3 kitu ambacho kitapunguza uwezo wake.

Ila kwa nchi moja moja nakubali hana mpinzani dhidi ya hizo nchi tatu.
Hatuwezi kujua huwenda vyote vikawezekana.
Maana ukitizama Iran haijapakana na taifa lolote kati ya hayo.
Kwahiyo vita itayopiganwa ni ya makombora,roketi na ndege.
Maana si Iran wala hao waarabu atakayekubali kuvuka zaidi ya kilometa 1000 kumfuata mwenzake.
Ila makombora ndio yatahusika.
Na hakuna taifa la kiarabu lenye uwezo wa kupimiana nguvu za makombora na Iran,Iran pia inao uwezo wa kurusha makombora kwa nchi hizo tatu kwa wakati mmoja maana mifumo yake iko activated siku zote.
Labda useme uvamizi wa miguu ndio ungehitaji kugawanya jeshi,ila hapo haitofanyika uvamizi wa miguu maana hawachangii mipaka ya nchi.
Hata hizo nchi zikijaribu kuivamia kwa miguu Iran zitashindwa,maana Iran wako vizuri kwenye ku repell ground attacks.
Turejelee vita ya Iraq-Iran war ya 1980-1988.
Iraq aliivamia Iran akisapotiwa na USA na France in all millitary wise.
Ila walishindwa kumpiga Iran.

Kiufupi mkuu hapo itapiganwa vita ya masafa marefu ikihusisha makombora na ndege na drones .
Na kwenye hiyo sekta hakuna mtu yeyote middle east anamfikia Iran.
 
Point yako iko sawa kwenye vita ya kuvunja majumba, barabara, kuwauwa raia kweli Israel atawashinda lakini kwa vita haswa hanshindi hata mmoja.
Soma kuelewa kaka sio kujibu.
Tunaongelea Iran dhidi ya Misri, Jordan na Saudia sio Israel. Kosugi
 
Hatuwezi kujua huwenda vyote vikawezekana.
Maana ukitizama Iran haijapakana na taifa lolote kati ya hayo.
Kwahiyo vita itayopiganwa ni ya makombora,roketi na ndege.
Maana si Iran wala hao waarabu atakayekubali kuvuka zaidi ya kilometa 1000 kumfuata mwenzake.
Ila makombora ndio yatahusika.
Na hakuna taifa la kiarabu lenye uwezo wa kupimiana nguvu za makombora na Iran,Iran pia inao uwezo wa kurusha makombora kwa nchi hizo tatu kwa wakati mmoja maana mifumo yake iko activated siku zote.
Labda useme uvamizi wa miguu ndio ungehitaji kugawanya jeshi,ila hapo haitofanyika uvamizi wa miguu maana hawachangii mipaka ya nchi.
Hata hizo nchi zikijaribu kuivamia kwa miguu Iran zitashindwa,maana Iran wako vizuri kwenye ku repell ground attacks.
Turejelee vita ya Iraq-Iran war ya 1980-1988.
Iraq aliivamia Iran akisapotiwa na USA na France in all millitary wise.
Ila walishindwa kumpiga Iran.

Kiufupi mkuu hapo itapiganwa vita ya masafa marefu ikihusisha makombora na ndege na drones .
Na kwenye hiyo sekta hakuna mtu yeyote middle east anamfikia Iran.
Nakubaliana na wazo lako.
Lakini umeangalia upande wa kushambulia tu. Vipi na wao wakishambuliwa kwa wakati mmoja, uwezo na ubora wao katika kujilinda utabaki ule ule?
 
Mwanamke anapoandanana kudai haki sawa, ni kuwaonea tu wanaume, maana wanaume hawajawanyima haki yoyote

Wanawake wanapaswa kufahamu kwamba, wanayetakiwa kumdai hizo haki ni MUNGU, maana huyo ndiye aliyesema mwanaume ndiye kichwa cha familia basi..!

Mungu ndiye aliyesema, Mwanaume atamtawala mwanamke, wamdai yeye na siyo kuandamana wakitudai sisi wanaume

ukimkuta kiongozi kasimama kuungana na kelele hizo za wanawake wakidai haki hizo, ujue anataka kusimama kwenye nafasi ya MUNGU

Nataka kusema hivi..! MUNGU ndiye aliyewapa hiyo aridhi Waisrael

Hao Parestina wanapaswa kuandamana wamuulize huyo Mungu ni kwa nini aliwapa aridhi waisrael? JE wao waende wapi? Atawajibu

Sasa wewe, aidha unitukane mimi,, na au umtukane huyo Mungu aliyesema hivyo

Sasa kazi ni kwako
Unaonesha una akili mgando sana.
Je Mungu ameruhusu mwanaume amnyanyase mwanamke kwa kumpiga na kumdhalilisha kimaneno!?
Je Mungu aliruhusu sisi wanaume tuwatumikishe hovyo hovyo wanawake katika majumba!?
Je Mungu aliruhusu sisi wanaume tuwaonee wanawake hata kama sisi ndio tumekosea!?
Hizo hapo juu ndio sababu ya wanawake kupata mwanya wa kudai haki zao za uhuru.
Kama sisi wanaume tungeliwatendea haki basi tusingelifikia huko kuandamwa na wanawake wakidai haki zao za uhuru na usawa.

Wanaisrael walishafikishwa nchi ya ahadi!?
Unaweza kututajia nchi ya ahadi ambayo wanaisrael walifikishwa na Mungu!?

Sawa twende taratibu,Israel walipewa ardhi kubwa inayowatosheleza ikiwemo Jerusalem wanayoitaka wao.
Ila hawakuishia hapo kuanzia 1948 walivamia;
-Central Syria.
-Gollan heights.
-Lebanon.
-Sinai-Egypt.
-Suez canal-Egypt.
Aya tuambie Mungu alimpa ardhi zote hizi Israel!?
Pia unasahau kuwa hao Palestina ndio wafilisti.

Una safari ndefu sana kifikra.
Mungu wa sisi sote na anatutendea sote pasi na upendeleo na ardhi ni ya sisi sote.
Ingekuwa hivyo basi hata GREEK/UGIRIKI ingeanzisha vita na UTURUKI kudai ISTANBUL(CONSTANTINOPLE),BURSA,ANATOLIA/ANTALYA.
Maana takriban asilimia 45 ya ardhi ya Uturuki ni ardhi ya UGIRIKI.
Je haki ya kudai ardhi anayo Israel tu!?

Pole sana.
 
Nakubaliana na wazo lako.
Lakini umeangalia upande wa kushambulia tu. Vipi na wao wakishambuliwa kwa wakati mmoja, uwezo na ubora wao katika kujilinda utabaki ule ule?
Unaweza usibaki ule ule kaka,ila itatarajiwa hao watashambulia wakati gani maana mifumo yao haipo active kama ya Iran.
Pia Iran ina historia ya kuchangiwa na zaidi ya taifa moja na ikahimili mashambulizi.
Hivyo katika medani ya vita wako vizuri,japo hatuwezi kujua kitatokea nini moja kwa moja.
 
"Kwasababu ina nguvu kuliko hamas" (Russia v/s Ukrain?)
- Houth kwanini hawakuchaguwa kuisaidia Palestine waakimarishana huko huko ndani ya palestine ambako tayari moto ilikuwa ukiwaka, au walitaka kupanua eneo la mapigano?
Umeongea nini hapa mbona hueleweki!?
Tulia uandike vizuri.
 
Ndio MKUU yakwenye media inaenda kupigana na mataifa saba kwa siku sita ila inashindwa na kagroup kwa mwaka mzima
Yakwenye media inaenda entebbe kuokoa mateka wake kwa masaa 24 ila inashindwa kuokoa mateka wake hapo mlangoni kwao kwa mwaka kasoro sasa
Nadhani umeiona israhell halisi naile ya kwenye media
Mkuu nimekuelewa sasa. Hizi media hasa za western ni majanga. Tnalishwa matango pori kila siku.
US nayo itakuwa hivyo mikwara kibao ila hakuna kitu😕😕😕😕😕
 
Hakuna mfanano wa makundi na nchi na hautakuja uwepo
Mnataka mfananishe kufidia kushindwa kwa mzayuni
Nchi itaendelea kua nchi na makundi yataendelea kua makundi
Hamas wapo ila wao hawaelewani na fatah wapo nchi moja unawafananishaje na nchi?
Houthi wapo ila nchi imegawanyika kuna serikali zaidi ya moja hawa unafananishaje na nchi?
Walau hizbullah wao ni sehemu ya sirikali
Ila hakuwezi kukawa sawa baina ya nchi na kundi
Sawa. Sasa inakuwaje nchi husika haziwakatai ili kujiepusha na kipigo/Uharibifu? e.g. Unapomhifadhi kibaka aliyeingia nyumbani kwako (haumtoi); raia wenye hasira kali waliokuwa wanamfukuza wanaweza kuichoma nyumba hiyo ambayo ni mali yako na ww ndo unapata hasara. e.g. Bandari iliyochomwa ni mali ya Yemen na sio mali ya Houthi. Ila Yemen ndo amepata hasara.
 
Houthi ni chama cha kisiasa kihistoria unasemaje wanahifadhiwa hapo Yemeni!?
Ni sawa useme ACT wazalendo wanahifadhiwa hapa Tanzania mkuu utakua uko serious kweli!?
Houthi wote ni asili ya Yemeni na wana historia katika kila siasa za Yemeni toka 1990s.
Unasema mtu anahifadhiwa nchini kwake!?
Ni Chama cha siasa kweli, lakini kimeenda mbali zaidi na kujiwekea mkondo wa kijeshi ndani ya chama. Hauwezi kuwa na majeshi mawili katika nchi moja. Ndo mana nimesema wanahifadhiwa kwa mana kwamba Yemen ana-intertain uwepo wa jeshi lisilo rasmi nchini mwake hata kama wahusika ni wenyeji.
Yan ACT wazalendo wawe na vikosi vya kiJeshi hapa Tz? Hawatakubaliwa japo ni Watanzania halisi- Hizo ni vurugu. Kama Tz wataridhika bila kuchukua hatua ina maana wamekubaliana na jambo hilo. Kama wakichukua hatua, hata nchi marafiki watasaidia kuvifurusha vikosi hivyo haramu(Sio vikosi rasmi na havitakiwi).
 
Sawa. Sasa inakuwaje nchi husika haziwakatai ili kujiepusha na kipigo/Uharibifu? e.g. Unapomhifadhi kibaka aliyeingia nyumbani kwako (haumtoi); raia wenye hasira kali waliokuwa wanamfukuza wanaweza kuichoma nyumba hiyo ambayo ni mali yako na ww ndo unapata hasara. e.g. Bandari iliyochomwa ni mali ya Yemen na sio mali ya Houthi. Ila Yemen ndo amepata hasara.
Houthi ndio inaunda serikali ya Yemeni sasa hivi,japo muunganiko bado haujawa sawa.
Raia wote wanaunga mkono anachofanya Houthi.
90% ya raia wa Yemeni wanaungana na anachofanya Houthi.
 
Back
Top Bottom