Israeli kusitisha mapigano na Hezbollah, je ni hatua ya Israeli kujiimarisha zaidi au ni mbinu na mkakati wa kumfifisha Iran?

Ushaambiwa "over a decade" ww unasema mwaka Jana au lugha ni tatizo?
Unahisi huko Litan river wamefikaje kama sio baada ya kuwapelekea moto wa kutosha hao Hizbullah?
Hizo ni mbwembwe tu kwani sisi hatufahamu kuwa mwezi wa 11 Mwaka jana IDF waliingia hapo!?
Au sisi tuna amnesia !?
 
Hivi huwa hata unapitia unachorusha ama unarusha tu!?
Mbona unayoyaleta ni OP na unayozungumza!?
Sababu za Iran kukaa kimya ndio hii article uliyoleta!?
😂😂😂😂😂😂😂Aiseeee.
 
kuna watu wanajitekenya wenyewe huku wanacheka eti Israel imeshindwa vita na hezibola , Israel imeshindwa vita kivipi na wakati hezibola wamesogezwa kutoka eneo la kusini mwa Lebanon na jeshi la Lebanon ndio litachukua uzibiti wa eneo la kusini kama makubaliano ya kuthitisha vita na kama waki compromise within 60 days kiminyo pale kipo pale. Walebanon na waisrael wamefurahia sana hii truce lengo ni watu waishi kwa amani na waendelee na maisha yao ya kila siku otherwise vita sio nzuri kwa pande zote .
 
Hivi huwa hata unapitia unachorusha ama unarusha tu!?
Mbona unayoyaleta ni OP na unayozungumza!?
Sababu za Iran kukaa kimya ndio hii article uliyoleta!?
😂😂😂😂😂😂😂Aiseeee.
Naona unataka mabishano😀Sina muda huo mambo yapo hadharani subiri utaona😄😄
 
Ngoma kurudi uwanjani inawezekana maana Israel itakua ishajipanga.
Japo Hizbollah kuondoka Kusini mwa Lebanon ni uongo.
Serikali ya Lebanon imegawanyika na upande ambao anatawala Hizbollah ndio huo .
Upande uliokuwa unatawaliwa na Hezbollah ndiko walikofurushwa i.e. Hezbollah walikimbilia kaskazini na kuvuka mto Litani. Kwa mujibu wa makubaliano -Ceasefire; Hezbollah anatakiwa abakie hukohuko kaskazini ng'ambo ya mto Litani i.e. Upande aliokuwa anatawala Hezbollah ndo basi tena sasa umekuwa ndo buffer zone. IDF na Hezbollah hawaruhusiwi kuonekana hapo.
Hezbollah kwa kukubali kwake na kusaini mpango-dili wa ceasefire manake anakubali kuondoka kuisini mwa Lebanon bila shuruti. Nadhani hilo ndio jambo gumu sana kwa Hezbollah kwani linaleta hisia ya kupelekwa Uhamishoni ng'ambo ya mto Litan. Halafu ukizingatia muda Hezbollah aliokuwa ametawala eneo hilo ni wazi kwamba bado yapo maslahi yake huko kusini mwa Lebanon.
Mafadhili mkuu wa makundi hayo ya Hezbollah na HAMAS hajasema neno na Utekelezaji wa cease fire ulianza siku Jumatano 27/11/2024.
 
Sawa sina muda wa kubishana mambo yapo wazi Irani kanywea hata humsikii kizungumzia mambo Lebanoni,Hezbolah katulizwa
Acha ujinga. Israeli amepoteza sana kwenya hayo makubaliano maana kuna maeneo mawali ya Lebanon amabayo Israeli alijimilikisha inabidi hayaachie
 
Mkuu hakuna eneo ambalo Hizbollah amefukuzwa embu kasome taarifa vizuri.
Maana huko Kusini mwa Lebanon hakuna eneo ambalo IDF walifanikiwa kulishikilia hata kwa sekunde.
Hizbollah inatawala Kusini yote ya Lebanon.
Ni sawa useme Kwa Tanzania iwe inatawala kuanzia Mkuranga hadi mpakani na Msumbiji.
Ingekua Hizbollah wamefurushwa huko basi kipengele moja wapo cha makubaliano kisingesema "Hizbollah isihusike na kujipanga kisilaha na utawala wa maeneo ya Kusini,badala yake vikosi vya jeshi kuu la Lebanon ndio vihusike".
Hii inamaana bado Hizbollah wana supremacy na hilo eneo.
Swali linakuja je Hizbollah watakubali kuondoka hilo eneo!?
 

Kusimama kwa mapigano ni faida kwa wote wawili Israel na Hizbolah maana wote walikuwa wanahitaj hili ili wajipange..

Ila ni faida zaid kwa Israel kwasababy nao wanarudisha nguvu kwa Hamas, hata netanyau kasema kuwa kusimamishwa kwa mapigano kutasaidia wao kujipanga na kukusanya nguvu. Na kutawapa nafasi ya kufocus kwa adui wao namba noja iran.

Ukiangalia naona kusimama kwa mapigano kutaivunja nguvu Hamas kwasababu sapoti waliokuwa wanaipata kwa Iran, Hizbolah na houthi kulifanya israel ijigawe na kuelemewa.. maana hata uwe mwamba vipi ikiwa unashambuliwa kila kona lazima utafite namna ya kuretreat..

hizbola hawakupaswa kukubali hii ceasefire kama nia ililuwa kuwasaidia hamas. Imewachukua miaka 16 Hizbolah kujiimarisha walitakiwa. Wahakikishe kuwa hamas anafanikiwa lengo lake.. kitendo cha kukubali kusitisha mapigano ni kumpa nafasi israel kuhakikisha hakutwi offguard tena
 
Umeongea kwa mapenzi na hisia badala ya uhalisia na hoja.
 
Hizbullah wamefurushwa kusini mwa Lebanon?
Ebu soma tena ulicho kiandika.
 
sasa iran atafifia vipi wakati hizbollah mtoto wa Iran wameomba poo, Iran ni giant kwa izrael peke yake hatoboi ww angalia Iraq alipigwa ni karibu nchi zote za ulaya na US na japan kipindi hiko, sasa Iran amejivuta sana na kujipanga sana kuliko Iraq ya Sadam Hussen
 
Hizbullah wamefurushwa kusini mwa Lebanon?
Ebu soma tena ulicho kiandika.
Ndiyo. Hezbollah walifurushwa kutoka kusini mwa Leabanon(Eneo walilokuwa wamelishikilia kwa siku nyingi na kulitawala).
Labda kama ww unaelewa zaidi, basi mjadala uendelee.
 

What the ceasefire deal looks like​

US President Joe Biden has said the deal that took effect November 27 “is designed to be a permanent cessation of hostilities.” Here’s what it entails.​




Sources: A US senior administration official, Lebanon's Prime Minister Najib Mikati
Graphic: Henrik Pettersson, CNN
 
Wajanja sana hawa jamaa USA, Westerners + Israel.
Walichofanikiwa Wayahudi:
1. Ardhi ya nyongeza bure
2. Wamewadhihirishia Majirani wao Mahasimu (nchi za Kiarabu)kwamba usijaribu kutunishiana misuli na Myahudi hata siku moja. Wamefanikiwa kutoa ONYO.
3. Wamefanikisha azma yao ya kuilazimisha Hezbollah iondoke eneo la mpakani ikae mbali huko kaskazini ng'ambo ya mto Litani.
 
Acha ujinga. Israeli amepoteza sana kwenya hayo makubaliano maana kuna maeneo mawali ya Lebanon amabayo Israeli alijimilikisha inabidi hayaachie
Usiwe mvivu kufikiri kwa kulevya na propaganda,jiulize lengo Hezbollah kuingilia ugomvi wa Hamasi na Israeli lilikuwa ni Nini?

Hamas walisema wanaingia kupigana na Israeli na hawataacha mpaka Israeli waondoke Gaza,je wamefanikiwa?

Israeli iache kuingilia ugomvi wake na Hammas ikiwa ni pamoja na kiondoka kusini mwa Lebanoni na waache kurusha Makombora Je Hezbolah hawajatii?? Kama hapa basi uelewi bass madras hamna kitu
 
Ndiyo. Hezbollah walifurushwa kutoka kusini mwa Leabanon(Eneo walilokuwa wamelishikilia kwa siku nyingi na kulitawala).
Labda kama ww unaelewa zaidi, basi mjadala uendelee.
Sasa kama walikuwa wamesha furushwa maana yake ni Israel ilikuwa imesha shinda vita sasa hayo makubaliano ni ya nini?
Mpaka makubaliano yanasainiwa Israel ilikuwa haija dhibiti hata Kijiji kimoja sasa hao Hizbullah imewafurusha muda gani?
Hizbullah haitaondoka kusini mwa Lebanon bali wataondoka kwenye eneo lijulikanalo kama msitari wa buluu ambao uliwekwa na UN mwaka 2006 , msitari wa buluu ni mpaka usio rasmi kati ya Lebanon na Israel ulio wekwa na UN mwaka 2006 baada ya vita kati ya Hizbullah na Israel.
Hata Israel hata ruhusiwa kufanya harakati zozote za kijeshi eneo hilo.
 
Mkuu samahani ningeomba ufafanue hii ramani inalenga nini!??
Hapa hakuna nilichoelewa.
 
Embu usiongee Kwa kupotosha.
Basi tuanze mwanzo wa vita na malengo ya Kila mmoja.
*Lengo la Hizbollah kushambulia Israel tangu Oktoba 8 2023 ilikua ni kuwapunguza nguvu Israel kushambulia Gaza dhidi ya Hamas ikiwezekana kuishinikiza Israel kuendesha vita Hamas.Lengo la kupunguza nguvu walifanikiwa kwasababu iliwalazimu Israel kuhamisha baadhi ya nguvu kaskazini mwa Israel dhidi ya Hizbollah.
*Lengo la Israel kuanzisha operation ya kijeshi Kusini mwa Lebanon ni kuleta amani kaskakazini mwa Lebanon ili raia warudi kwenye makazi yao ikiwemo Galilee pia kuwa disarm/dismantle ama kuwavunja nguvu Hizbollah na kuwarudisha nyuma ya mto Latan/Letan.
Nakuuliza wewe maswahili mazeeh,
-Je raia wa kaskazini mwa Israel wamefanikiwa kurudi hadi sasa!?
-Je Hizbollah wamevunjwa nguvu kama ilivyotakiwa na hawawezi kushambulia tena!?

*Hizbollah kukubali itakua ni kwasababu ya shinikizo la serikali yake sio kwasababu anamtii ISRAEL.
Embu elewa how diplomacy works kijana.
Japo Hizbollah bado hajatoa tamko juu ya hili ila hata akikubali ni sawa na ni kheri kwake kwasababu akikataa itakua ni mbaya kwake Kwa ushawishi wa serikali yake hususan Kusini mwa Lebanon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…