Israeli kusitisha mapigano na Hezbollah, je ni hatua ya Israeli kujiimarisha zaidi au ni mbinu na mkakati wa kumfifisha Iran?

Israeli kusitisha mapigano na Hezbollah, je ni hatua ya Israeli kujiimarisha zaidi au ni mbinu na mkakati wa kumfifisha Iran?

Ushaambiwa "over a decade" ww unasema mwaka Jana au lugha ni tatizo?
Unahisi huko Litan river wamefikaje kama sio baada ya kuwapelekea moto wa kutosha hao Hizbullah?
Hizo ni mbwembwe tu kwani sisi hatufahamu kuwa mwezi wa 11 Mwaka jana IDF waliingia hapo!?
Au sisi tuna amnesia !?
 
Sawa endelea kuamini hilo sisi tunasubiri Ahadi ya Ayatollah asifirikiri tume sahau,na asipotimiza ameisha atakuwa kama Syria tu

BBC News, Swahili
Ruka hadi maelezo
Yaliyomo

Kwanini Iran inakabiliwa na maamuzi magumu katika mzozo wake na Israel?​

xx

Chanzo cha picha,Reuters
27 Oktoba 2024
Imeboreshwa 28 Oktoba 2024
Shambulio la Israel dhidi ya Iran linazidisha vita katika Mashariki ya Kati. Kuepuka, au hatari kuongezeka ambayo itafanya hali kuwa mbaya zaidi katika mzozo kati ya Israel na Iran ikiwa miongoni mwa yaliyomo kwenye maamuzi yanayochukuliwa na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei na washauri wake wakuu.
Lazima waamue chaguo ambalo halitakuwa na athari kidogo kati ya chaguzi ngumu zilizopo.
Kati ya chaguzi walizonazo ni kushambulia kwa wimbi jingine la makombora ya balestiki. Israel tayari imetishia kulipiza kisasi tena iwapo hilo litatokea.
Upande mwingine ni kuamua kuwa na mpaka chini ya mashambulizi mbaya ya moja kwa moja ya pande zote mbili kwenye maeneo yao.
Hatari kwa Iran ikiwa itajizuia kujibu shambulizi la Israel ni kuonekana kuwa dhaifu, kutishwa na kuzuiwa na nguvu za jeshi la Israel inayoungwa mkono na Marekani.
Mwishowe, kiongozi mkuu na washauri wake wana uwezekano wa kuchukua uamuzi ambao, kwa maoni yao, utakuwa na madhara kidogo kwa utawala wa Kiislamu wa Iran.
Soma zaidi:

Vitisho vitupu?​

.

Chanzo cha picha,EPA
Vyombo vya habari rasmi vya Iran saa chache kabla na baada ya mashambulizi ya Israel zilizungumzia taarifa za dharau ambazo, bila kuzifikiria kwa undani, zinaonyesha uamuzi wa kujibu tayari umechukuliwa.
Lugha yake inafanana na ya Israel, ikitaja haki yake ya kujilinda dhidi ya mashambulizi. Lakini hatari kwa uamuzi huo iko juu sana kiasi kwamba Iran inaweza kuamua kutotimiza vitisho vyake.
Hayo ni matumaini ya Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer, ambaye naye pia aliunga mkono msisitizo wa Marekani kwamba Israel imechukua hatua ya kujilinda.
"Nazungumza kwa uwazo kabisa kwamba Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Iran," alisema. "Niko wazi vile vile kwamba tunahitaji kuepuka kuzidisha mzozo wa kikanda na kuzitaka pande zote kujizuia. Iran haipaswi kujibu."
Matamshi ya Iran yenyewe yamekuwa thabiti tangu kombora lake la balistiki dhidi ya Israel tarehe 1 Oktoba. Wiki moja iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, aliambia mtandao wa NTV wa Uturuki kwamba "shambulio lolote dhidi ya Iran litazingatiwa kuvuka mstari mwekundu kwa ajili yetu. Shambulio kama hilo halitakosa kujibiwa."
Saa chache kabla ya mashambulizi ya Israel, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmail Baqai alisema: "Uchokozi wowote wa utawala wa Israel dhidi ya Iran utakabiliwa kwa nguvu zote." Alisema, ilikuwa, "kupotosha sana na isiyo na msingi" kupendekeza kwamba Iran haitajibu mashambulizi kidogo ya Israel.
Wakati ndege za Israel zilipokuwa zikirejea kwenye kambi, wizara ya mambo ya nje ya Iran ilizungumzia haki yake ya kujilinda "kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 51 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa". Taarifa ilisema Iran inaamini kuwa ilikuwa na haki na wajibu wa kujibu vitendo vya uchokozi kutoka nje ya nchi.

Mabadilishano mabaya​

Israel imeonyesha kuwa tayari kuzidisha mzozo tangu mwanzoni. Inaiona Iran kama muungaji mkono muhimu wa mashambulizi ya Hamas yaliyoua takriban watu 1,200 - Waisrael na zaidi ya raia 70 wa kigeni - tarehe 7 Oktoba mwaka jana.
Kwa kuhofia kuwa Israel ilikuwa inatafuta nafasi ya kushambulia, Iran ilionyesha mara kwa mara kwamba haitaki vita kamili na Israel.
Hiyo haikumaanisha kwamba ilikuwa tayari kukomesha shinikizo lake la mara kwa mara, ambalo mara nyingi linakuwa baya, badala yake ilikuwa inapunguza shinikizo kwa Israel na washirika wake.
Watehran walidhani walikuwa na wazo bora kuliko vita vya pande zote. Iran ilitumia washirika wake katika kile kinachoitwa "mhimili wa upinzani" kushambulia Israel.
Wahouthi nchini Yemen walizuia na kuharibu meli katika Bahari ya Shamu. Milio ya roketi ya Hezbollah kutoka Lebanon iliwalazimu Waisrael 60,000 kutoka makwao.
Miezi sita baada ya vita, kulipiza kisasi kwa Israel kuliwalazimu mara mbili ya Walebanon kutoroka makazi yao ya kusini, na si hayo tu, kwasababu Israel ilikuwa tayari kufanya mengi zaidi.
Ilionya kwamba ikiwa Hezbollah haitasitisha mashambulizi yake dhidi ya Israel na kurudi nyuma kutoka kwenye mpaka itachukua hatua.
Iran ikiwa kwenye vita vyake vya kimkakati.
Iliishia kuwa mfululizo wa mapigo makali ambayo yaliuvuruga utawala wa Kiislamu mjini Tehran na kuuacha mkakati wake katika hali tete. Ndio maana, baada ya shambulio la hivi punde la Israel, viongozi wa Iran wana maamuzi magumu tu.
Israel ilitafsiri kusita kwa Iran kupigana vita vya kila upande kama udhaifu, na ikaongeza shinikizo kwa Iran na washirika wake. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na makamanda wa Israel wanaweza kumudu kuchukua hatua ambayo inaweza kuhatarisha hali.
Walikuwa na uungwaji mkono usioyumba wa Rais Joe Biden, ambao sio tu unaandamana na uwasilishaji mkubwa wa silaha, lakini pia kwa uamuzi wake wa kutuma vikosi muhimu vya majini na kwenye anga vya Marekani katika Mashariki ya Kati ili kuunga mkono dhamira ya Marekani ya kuilinda Israel.
Tarehe 1 Aprili shambulizi la anga la Israel liliharibu sehemu ya jumba la kidiplomasia la Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria. Ilimuua kamanda mkuu wa Iran, Brig Jenerali Mohammed Reza Zahedi, pamoja na maafisa wengine wakuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).
,

Chanzo cha picha,Reuters
Lakini tangu majira ya kiangazi, Israel imezidisha mara kwa mara vita na Iran na washirika wake. Pigo kubwa zaidi ilikuwa katika mashambulizi makubwa dhidi ya mshirika muhimu wa Iran, Hezbollah nchini Lebanon. Iran imetumia miaka mingi kujenga safu ya silaha za Hezbollah kama sehemu muhimu ya ulinzi.
Wazo lilikuwa shambulio la Israel dhidi ya Iran lingezuiwa na maarifa kwamba Hezbollah ingeishambulia Israel kutoka juu ya mpaka wa Lebanon.
Lakini Israel ilichukua hatua ya kwanza, kutekeleza mipango iliyokuwa imeweka tangu Hezbollah ilipopigana nayo katika vita vya mwaka 2006.
Ililipua vifaa vya mawasiliano na mazungumzo ambayo ilikuwa imewalaghai Hezbollah kununua, ikavamia kusini mwa Lebanon na kumuua kiongozi wa Hezbollah Sheikh Hasan Nasrallah, mtu ambaye alikuwa ishara ya upinzani mkali kwa Israel kwa miongo kadhaa.
Mamlaka mjini Beirut inasema kuwa mashambulizi ya Israel nchini Lebanon hadi sasa yameua zaidi ya watu 2,500, na kuwafanya wengine zaidi ya milioni 1.2 kuyahama makazi yao na kusababisha uharibifu mkubwa kwa nchi ambayo tayari imesambaratika baada ya uchumi wake kuporomoka kwa kiasi kikubwa.
Hezbollah bado inapigana na kuwaua wanajeshi wa Israel ndani ya Lebanon na kurusha idadi kubwa ya makombora. Lakini inayumba baada ya kumpoteza kiongozi wake na idadi kubwa ya silaha zake.
Ikikabiliwa na kuporomoka kwa mkakati wake, Iran ilihitimisha kuwa lazima ilipize kisasi. Kuruhusu washirika wake kupigana na kufa bila kujibu kunaweza kuharibu nafasi yake kama kiongozi wa vikosi vya kupambana na Israel na Magharibi katika eneo hilo.
Jibu lake lilikuwa shambulio kubwa zaidi la kombora la balestiki dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 1.
Mashambulio ya anga ya Ijumaa tarehe 25 Oktoba yalikuwa jibu la Israel. Walichukua muda mrefu kujibu kuliko wengi walivyotarajia. Kuvuja kwa mipango ya Israel kunaweza kuwa sababu.
Israel pia inafanya mashambulizi makubwa kaskazini mwa Gaza. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk ameutaja wakati mbaya zaidi wa vita vya Gaza, huku jeshi la Israel likiwaweka watu wote kwa mashambulizi ya mabomu, kuzingirwa na hatari ya njaa.
Ni vigumu kwa mtu wa nje kujua kama muda wa mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran ulikusudiwa kuvutia nadhari kimataifa kutoka kaskazini mwa Gaza. Lakini inaweza kuwa sehemu ya mipango yake.
Soma zaidi:
Imetafsiriwa na Asha Juma

Mada zinazohusiana​

Habari kuu​

Gumzo mitandaoni​

Iliyosomwa zaidi​

  1. 1
    Kwanini usitishaji mapigano wa Lebanon ni ahueni na sio suluhu kwa mzozo wa Mashariki ya Kati?
  2. 2
    Tetesi za soka Ulaya: Liverpool na Real Madrid wafanya mazungumzo kuhusu mustakbal wa Alexander Arnold
  3. 3
    Kwanini paka weusi wanahusishwa na uchawi na bahati mbaya?
    Imeboreshwa mwisho: 22 Agosti 2023
  4. 4
    Kwanini nyota wa Westham huvalia jezi yenye muundo tofauti?
  5. 5
    Maana zilizofichika katika mchoro wa utupu wa karne ya 16
BBC News, Swahili
© 2024 BBC. BBC haihusiki na taarifa za kutoka mitandao ya nje. Soma kuhusu mtazamo wetu wa viambatanishi vya nje.
Hivi huwa hata unapitia unachorusha ama unarusha tu!?
Mbona unayoyaleta ni OP na unayozungumza!?
Sababu za Iran kukaa kimya ndio hii article uliyoleta!?
😂😂😂😂😂😂😂Aiseeee.
 
kuna watu wanajitekenya wenyewe huku wanacheka eti Israel imeshindwa vita na hezibola , Israel imeshindwa vita kivipi na wakati hezibola wamesogezwa kutoka eneo la kusini mwa Lebanon na jeshi la Lebanon ndio litachukua uzibiti wa eneo la kusini kama makubaliano ya kuthitisha vita na kama waki compromise within 60 days kiminyo pale kipo pale. Walebanon na waisrael wamefurahia sana hii truce lengo ni watu waishi kwa amani na waendelee na maisha yao ya kila siku otherwise vita sio nzuri kwa pande zote .
 
Hivi huwa hata unapitia unachorusha ama unarusha tu!?
Mbona unayoyaleta ni OP na unayozungumza!?
Sababu za Iran kukaa kimya ndio hii article uliyoleta!?
😂😂😂😂😂😂😂Aiseeee.
Naona unataka mabishano😀Sina muda huo mambo yapo hadharani subiri utaona😄😄
 
Ngoma kurudi uwanjani inawezekana maana Israel itakua ishajipanga.
Japo Hizbollah kuondoka Kusini mwa Lebanon ni uongo.
Serikali ya Lebanon imegawanyika na upande ambao anatawala Hizbollah ndio huo .
Upande uliokuwa unatawaliwa na Hezbollah ndiko walikofurushwa i.e. Hezbollah walikimbilia kaskazini na kuvuka mto Litani. Kwa mujibu wa makubaliano -Ceasefire; Hezbollah anatakiwa abakie hukohuko kaskazini ng'ambo ya mto Litani i.e. Upande aliokuwa anatawala Hezbollah ndo basi tena sasa umekuwa ndo buffer zone. IDF na Hezbollah hawaruhusiwi kuonekana hapo.
Hezbollah kwa kukubali kwake na kusaini mpango-dili wa ceasefire manake anakubali kuondoka kuisini mwa Lebanon bila shuruti. Nadhani hilo ndio jambo gumu sana kwa Hezbollah kwani linaleta hisia ya kupelekwa Uhamishoni ng'ambo ya mto Litan. Halafu ukizingatia muda Hezbollah aliokuwa ametawala eneo hilo ni wazi kwamba bado yapo maslahi yake huko kusini mwa Lebanon.
Mafadhili mkuu wa makundi hayo ya Hezbollah na HAMAS hajasema neno na Utekelezaji wa cease fire ulianza siku Jumatano 27/11/2024.
 
Sawa sina muda wa kubishana mambo yapo wazi Irani kanywea hata humsikii kizungumzia mambo Lebanoni,Hezbolah katulizwa
Acha ujinga. Israeli amepoteza sana kwenya hayo makubaliano maana kuna maeneo mawali ya Lebanon amabayo Israeli alijimilikisha inabidi hayaachie
 
Upande uliokuwa unatawaliwa na Hezbollah ndiko walikofurushwa i.e. Hezbollah walikimbilia kaskazini na kuvuka mto Litani. Kwa mujibu wa makubaliano -Ceasefire; Hezbollah anatakiwa abakie hukohuko kaskazini ng'ambo ya mto Litani i.e. Upande aliokuwa anatawala Hezbollah ndo basi tena sasa umekuwa ndo buffer zone. IDF na Hezbollah hawaruhusiwi kuonekana hapo.
Hezbollah kwa kukubali kwake na kusaini mpango-dili wa ceasefire manake anakubali kuondoka kuisini mwa Lebanon bila shuruti. Nadhani hilo ndio jambo gumu sana kwa Hezbollah kwani linaleta hisia ya kupelekwa Uhamishoni ng'ambo ya mto Litan. Halafu ukizingatia muda Hezbollah aliokuwa ametawala eneo hilo ni wazi kwamba bado yapo maslahi yake huko kusini mwa Lebanon.
Mafadhili mkuu wa makundi hayo ya Hezbollah na HAMAS hajasema neno na Utekelezaji wa cease fire ulianza siku Jumatano 27/11/2024.
Mkuu hakuna eneo ambalo Hizbollah amefukuzwa embu kasome taarifa vizuri.
Maana huko Kusini mwa Lebanon hakuna eneo ambalo IDF walifanikiwa kulishikilia hata kwa sekunde.
Hizbollah inatawala Kusini yote ya Lebanon.
Ni sawa useme Kwa Tanzania iwe inatawala kuanzia Mkuranga hadi mpakani na Msumbiji.
Ingekua Hizbollah wamefurushwa huko basi kipengele moja wapo cha makubaliano kisingesema "Hizbollah isihusike na kujipanga kisilaha na utawala wa maeneo ya Kusini,badala yake vikosi vya jeshi kuu la Lebanon ndio vihusike".
Hii inamaana bado Hizbollah wana supremacy na hilo eneo.
Swali linakuja je Hizbollah watakubali kuondoka hilo eneo!?
 
Israel kupitia Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu imetangaza kukubali kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, hatua inayodhaniwa kumaliza vita hivyo vilivyodumu ndani ya mwaka mmoja na kuua takriban watu 3,800.

Rais Joe Biden ametangaza kuwa Marekani imesaidia kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Lebanon, ambayo yatamaliza vita kati ya Israeli na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

Kusimama kwa mapigano ni faida kwa wote wawili Israel na Hizbolah maana wote walikuwa wanahitaj hili ili wajipange..

Ila ni faida zaid kwa Israel kwasababy nao wanarudisha nguvu kwa Hamas, hata netanyau kasema kuwa kusimamishwa kwa mapigano kutasaidia wao kujipanga na kukusanya nguvu. Na kutawapa nafasi ya kufocus kwa adui wao namba noja iran.

Ukiangalia naona kusimama kwa mapigano kutaivunja nguvu Hamas kwasababu sapoti waliokuwa wanaipata kwa Iran, Hizbolah na houthi kulifanya israel ijigawe na kuelemewa.. maana hata uwe mwamba vipi ikiwa unashambuliwa kila kona lazima utafite namna ya kuretreat..

hizbola hawakupaswa kukubali hii ceasefire kama nia ililuwa kuwasaidia hamas. Imewachukua miaka 16 Hizbolah kujiimarisha walitakiwa. Wahakikishe kuwa hamas anafanikiwa lengo lake.. kitendo cha kukubali kusitisha mapigano ni kumpa nafasi israel kuhakikisha hakutwi offguard tena
 
ITR , toa balanced views, unaposema Iran ina uwezo wa kuipiga Israel moja kwa moja, kwa nini isiipige, toka mapinduzi ya Iran yafanyike 1978, kauli mbiu yake yote imekua ni "Death to America" Kwa sababu ndio yuko nyuma ya Israel, na wanajua hivyo....Je Leo America imekuwa n kikubwa ni Marekani! Kama wana uwezo wa kuipiga Israel, ina maana wanauwezo wa kuifuta Marekani! Ni akili ya mwendawazimu tu inaweza fikiri hivyo!

Na unaposema uhitaji wa Makundi yaliyopo karibu na Israel unapungua, Mkuu hata kama una mapenzi makubwa Hamas au Hezbollah, Ukweli ni kwamba vikundi hivyo vimeshindwa kabisa kutimiza malengo ya Iran! Ni kweli havijateketezwa 100% lakini vimeshindwa, ile support kubwa toka Iran haijaletea matunda! Na Kwa upande wa Hezbollah, vita vikiendelea hata nguvu yake ndani ya Lebanon inapungua na iatazidi kupungua. Hezbollah wanajua hilo na Iran pia!

Iran imeridhia, si kwa kutaka, wala uwezo wao wa Kijeshi, ni muda wa kujipanga upya! Hezbollah imemwangusha Iran, na ujio wa Trump haujulikani utaleta nini! Hezbolah imeangalia yote hayo! Na Israel nayo imekubali kumridhisha Biden, maana azimio lolote likipishwa UN bado wahahitaji Veto ya US, na ukumbuke pia Biden anaondoka Middle East hana legacy yoyote ile! Hivyo angalau aache hata kumbukumbu alisimamisha mapigano Lebanon.

ITR....Pitia source zote BBC/Ajazeera/CNN uone kila upande nikiwa na maana, Hezbollah/Israel /Biden kuna kitu anakipata katika mapatano haya.
Umeongea kwa mapenzi na hisia badala ya uhalisia na hoja.
 
Upande uliokuwa unatawaliwa na Hezbollah ndiko walikofurushwa i.e. Hezbollah walikimbilia kaskazini na kuvuka mto Litani. Kwa mujibu wa makubaliano -Ceasefire; Hezbollah anatakiwa abakie hukohuko kaskazini ng'ambo ya mto Litani i.e. Upande aliokuwa anatawala Hezbollah ndo basi tena sasa umekuwa ndo buffer zone. IDF na Hezbollah hawaruhusiwi kuonekana hapo.
Hezbollah kwa kukubali kwake na kusaini mpango-dili wa ceasefire manake anakubali kuondoka kuisini mwa Lebanon bila shuruti. Nadhani hilo ndio jambo gumu sana kwa Hezbollah kwani linaleta hisia ya kupelekwa Uhamishoni ng'ambo ya mto Litan. Halafu ukizingatia muda Hezbollah aliokuwa ametawala eneo hilo ni wazi kwamba bado yapo maslahi yake huko kusini mwa Lebanon.
Mafadhili mkuu wa makundi hayo ya Hezbollah na HAMAS hajasema neno na Utekelezaji wa cease fire ulianza siku Jumatano 27/11/2024.
Hizbullah wamefurushwa kusini mwa Lebanon?
Ebu soma tena ulicho kiandika.
 
Israel kupitia Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu imetangaza kukubali kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah la Lebanon, hatua inayodhaniwa kumaliza vita hivyo vilivyodumu ndani ya mwaka mmoja na kuua takriban watu 3,800.

Rais Joe Biden ametangaza kuwa Marekani imesaidia kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Lebanon, ambayo yatamaliza vita kati ya Israeli na kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.
sasa iran atafifia vipi wakati hizbollah mtoto wa Iran wameomba poo, Iran ni giant kwa izrael peke yake hatoboi ww angalia Iraq alipigwa ni karibu nchi zote za ulaya na US na japan kipindi hiko, sasa Iran amejivuta sana na kujipanga sana kuliko Iraq ya Sadam Hussen
 
Hizbullah wamefurushwa kusini mwa Lebanon?
Ebu soma tena ulicho kiandika.
Ndiyo. Hezbollah walifurushwa kutoka kusini mwa Leabanon(Eneo walilokuwa wamelishikilia kwa siku nyingi na kulitawala).
Labda kama ww unaelewa zaidi, basi mjadala uendelee.
 
Mkuu hakuna eneo ambalo Hizbollah amefukuzwa embu kasome taarifa vizuri.
Maana huko Kusini mwa Lebanon hakuna eneo ambalo IDF walifanikiwa kulishikilia hata kwa sekunde.
Hizbollah inatawala Kusini yote ya Lebanon.
Ni sawa useme Kwa Tanzania iwe inatawala kuanzia Mkuranga hadi mpakani na Msumbiji.
Ingekua Hizbollah wamefurushwa huko basi kipengele moja wapo cha makubaliano kisingesema "Hizbollah isihusike na kujipanga kisilaha na utawala wa maeneo ya Kusini,badala yake vikosi vya jeshi kuu la Lebanon ndio vihusike".
Hii inamaana bado Hizbollah wana supremacy na hilo eneo.
Swali linakuja je Hizbollah watakubali kuondoka hilo eneo!?

What the ceasefire deal looks like​

US President Joe Biden has said the deal that took effect November 27 “is designed to be a permanent cessation of hostilities.” Here’s what it entails.​

ai2html-graphic-mobile375.18c8013a.png

Sources: A US senior administration official, Lebanon's Prime Minister Najib Mikati
Graphic: Henrik Pettersson, CNN
 
Sababu kubwa ni kuwa, uongozi mpya wa USA, Trump, unataka Vita iieshe, haupo taysri kuendelea kutoa pesa, pili, jeshi la Israel, limechoka kwa sasa, kupigana Vita kwa miaka miwili, sio mchezo, TZ ilipigana Vita ya kagera, 40yrs +, Ila mpaka Leo, madhara ya ile Vita kiuchumi bado yapo,
Mafanikio kwa wayahudi wenzangu ni kuwa wamejipatia ardhi ya bure, Lebanon, Ila wao walitaka zaidi Gaza, wajenge settlements zao
Wajanja sana hawa jamaa USA, Westerners + Israel.
Walichofanikiwa Wayahudi:
1. Ardhi ya nyongeza bure
2. Wamewadhihirishia Majirani wao Mahasimu (nchi za Kiarabu)kwamba usijaribu kutunishiana misuli na Myahudi hata siku moja. Wamefanikiwa kutoa ONYO.
3. Wamefanikisha azma yao ya kuilazimisha Hezbollah iondoke eneo la mpakani ikae mbali huko kaskazini ng'ambo ya mto Litani.
 
Acha ujinga. Israeli amepoteza sana kwenya hayo makubaliano maana kuna maeneo mawali ya Lebanon amabayo Israeli alijimilikisha inabidi hayaachie
Usiwe mvivu kufikiri kwa kulevya na propaganda,jiulize lengo Hezbollah kuingilia ugomvi wa Hamasi na Israeli lilikuwa ni Nini?

Hamas walisema wanaingia kupigana na Israeli na hawataacha mpaka Israeli waondoke Gaza,je wamefanikiwa?

Israeli iache kuingilia ugomvi wake na Hammas ikiwa ni pamoja na kiondoka kusini mwa Lebanoni na waache kurusha Makombora Je Hezbolah hawajatii?? Kama hapa basi uelewi bass madras hamna kitu
 
Ndiyo. Hezbollah walifurushwa kutoka kusini mwa Leabanon(Eneo walilokuwa wamelishikilia kwa siku nyingi na kulitawala).
Labda kama ww unaelewa zaidi, basi mjadala uendelee.
Sasa kama walikuwa wamesha furushwa maana yake ni Israel ilikuwa imesha shinda vita sasa hayo makubaliano ni ya nini?
Mpaka makubaliano yanasainiwa Israel ilikuwa haija dhibiti hata Kijiji kimoja sasa hao Hizbullah imewafurusha muda gani?
Hizbullah haitaondoka kusini mwa Lebanon bali wataondoka kwenye eneo lijulikanalo kama msitari wa buluu ambao uliwekwa na UN mwaka 2006 , msitari wa buluu ni mpaka usio rasmi kati ya Lebanon na Israel ulio wekwa na UN mwaka 2006 baada ya vita kati ya Hizbullah na Israel.
Hata Israel hata ruhusiwa kufanya harakati zozote za kijeshi eneo hilo.
 
What the ceasefire deal looks like​

US President Joe Biden has said the deal that took effect November 27 “is designed to be a permanent cessation of hostilities.” Here’s what it entails.​

ai2html-graphic-mobile375.18c8013a.png

Sources: A US senior administration official, Lebanon's Prime Minister Najib Mikati
Graphic: Henrik Pettersson, CNN
Mkuu samahani ningeomba ufafanue hii ramani inalenga nini!??
Hapa hakuna nilichoelewa.
 
Usiwe mvivu kufikiri kwa kulevya na propaganda,jiulize lengo Hezbollah kuingilia ugomvi wa Hamasi na Israeli lilikuwa ni Nini?

Hamas walisema wanaingia kupigana na Israeli na hawataacha mpaka Israeli waondoke Gaza,je wamefanikiwa?

Israeli iache kuingilia ugomvi wake na Hammas ikiwa ni pamoja na kiondoka kusini mwa Lebanoni na waache kurusha Makombora Je Hezbolah hawajatii?? Kama hapa basi uelewi bass madras hamna kitu
Embu usiongee Kwa kupotosha.
Basi tuanze mwanzo wa vita na malengo ya Kila mmoja.
*Lengo la Hizbollah kushambulia Israel tangu Oktoba 8 2023 ilikua ni kuwapunguza nguvu Israel kushambulia Gaza dhidi ya Hamas ikiwezekana kuishinikiza Israel kuendesha vita Hamas.Lengo la kupunguza nguvu walifanikiwa kwasababu iliwalazimu Israel kuhamisha baadhi ya nguvu kaskazini mwa Israel dhidi ya Hizbollah.
*Lengo la Israel kuanzisha operation ya kijeshi Kusini mwa Lebanon ni kuleta amani kaskakazini mwa Lebanon ili raia warudi kwenye makazi yao ikiwemo Galilee pia kuwa disarm/dismantle ama kuwavunja nguvu Hizbollah na kuwarudisha nyuma ya mto Latan/Letan.
Nakuuliza wewe maswahili mazeeh,
-Je raia wa kaskazini mwa Israel wamefanikiwa kurudi hadi sasa!?
-Je Hizbollah wamevunjwa nguvu kama ilivyotakiwa na hawawezi kushambulia tena!?

*Hizbollah kukubali itakua ni kwasababu ya shinikizo la serikali yake sio kwasababu anamtii ISRAEL.
Embu elewa how diplomacy works kijana.
Japo Hizbollah bado hajatoa tamko juu ya hili ila hata akikubali ni sawa na ni kheri kwake kwasababu akikataa itakua ni mbaya kwake Kwa ushawishi wa serikali yake hususan Kusini mwa Lebanon.
 
Back
Top Bottom