Israeli yatangaza rasmi kuingiza majeshi nchini Lebanon upande ya kusini. Nini kitajiri baada ya hatua hii ngumu ya Israeli?

Israeli yatangaza rasmi kuingiza majeshi nchini Lebanon upande ya kusini. Nini kitajiri baada ya hatua hii ngumu ya Israeli?

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Marjayoun- Lebanon.
1727782001785.png

Kifaru cha jeshi la Israeli kilifanya doria kwenye mpaka wa Israeli na Lebanon mapema leo asubuhi. Picha na Aya Margolin wa Flash90

Israeli imetangaza kuingiza majeshi yake upande wa kusini mwa Lebanon na kuliweka eneo hilo chini ya jeshi la IDF yaani "military Zone". Hatua hiyo yafuatia uamuzi ulofanywa na Israeli na kuwaatarifu Marekani kwamba wameamua kuingiza majeshi ya ardhini nchini Lebanon.

Maeneo ya Metula, Misgav Am na Kfar Galadi yaliyoko upande wa kaskazini mwa Israeli yote yamefungwa kwa ajili ya IDF kuyatumia. Naibu kiongozi wa hezbollah Naim Qassim ametoa onyo kwa Israeli kuwa endapo IDF itaingia Lebanon kwa ajili ya vita ya ardhini basi Hezbollah wapo tayari.

Majeshi ya IDF khasa yale maalum au Special Forces tayari yapo ndani ya Lebanon huku vikosi vingine vikiendelea kusogea karibu na mpaka kutokea sehemu ya Kiryat Shmona. Vikosi vya makomandoo wa IDF vitakuwa vikitafuta upenyo wa kuingiza na kupandkiza mabomu ili kuwezesha vifaru kusogea ndani zaidi.

Israeli wamesema watatumia njia zote za ardhini, angani na majini kutimiza azma yao ya kupigana na Hezbollah vita ambayo ni ya pili baada ya vita ilopiganwa mwaka 2006 vita ambayo haikutoa mshindi yoyote. waziri mkuu Benjamin Netanyahu ametoa onyo kwa Iran kuwa hakuna eneo lolote ambalo Israeli itashindwa kulipiga.

Vifaru vya kijeshi vya IDF vimesogea mpakani na Lebanon huku naibu kiongozi wa wa Hezbollah akisema kuwa wapiganaji wa Hezbollah wapo tayari kwa vita ambayo kitaalamu yaitwa Asymmetrical Warfare pale ambapo Hezbollah watatumia mbinu iitwayo "gollila tactics" dhidi ya jeshi la IDF lenye kila aina ya zana ya kijeshi ijulikanayo ulimwenguni.

Lengo kuu ya Israeli ni kubomoa miundombinu ya Hezbollah ambayo yajumuisha njia za chini kwa chini (Tunnels) na njia za panya ambazo Hezbollah huzitumia kupitisha silaha zao na bidhaa zingine kutoka nje. Pia lengo hilo limekusudia kuhakikisha wananchi wa Israeli wanoishi upande wa Kaskazini ambao wamekimbia, warudi katika makazi yao.

Kwanini hali hii imefikia hapa?

Tarehe 17 hadi 18 mwezi huu vifaa vya mawasiliano yaani "pagers" wanotumia Hezbollah vililipuka pamoja na radio za mawasiliano.

Tarehe 23 hadi 24 Israeli ikafanya mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege za kivita dhidi ya maeneo ya Hezbollah.

Tarehe 27 Septemba kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akauawa katika shambulio kubwa la bomu liitwalo "bunker" lilofurumusha majengo na handaki walokuwamo Nasrallah na wenzie.

Tarehe 30 yaani leo jumatatu kiongozi wa Hamas aliekuwepo Lebanon nae ameuawa baada ya Israeli kushambulia tena kwa dege za kivita eneo hilo la kusini mwa Lebanon.

Wachambuzi wengi wa kijeshi na kijajusi wametoa tahadhari kwa Israeli kwamba hata kama safari hii wamejifunza mengi kutokana na vita ya mwaka 2006 lakini pia Hezbollah nao pamoja na kuuliwa kwa viongozi wake wengi kutokana na mashambulizi mengi aloyafanya Israeli, bado wana shaka kuwa Israeli itaweza kupigana vita ya ardhini.

Vita hii ya ardhini ambayo ni rahisi kuingia lakini ngumu kutoka, safari hii imekusanya makundi ya wapiganaji wanojiita "Axis of Resistance" yanojumuisha makundi ya kutoka Lebanon, Hamas, kutoka nchi za Irak na Syria pamoja na kundi la Houdh la Yemen na wote wakiwa na silaha walopewa na Iran.

Wahudhi wamepewa jukumu la kuhakikisha Marekani hapeleki silaha zaidi Israeli huku makundi yaliyoko Syria na Irak wakihakikisha wanatuma makombora upande wa kaskazini mwa Israeli kulipo milinma maarufu ya Golan ambayo Israeli huitumia kufanya doria dhidi ya Syria na Irak.

Milima ya Golan ilipokwa na Israeli baada ya vita ya siku sita ya mwaka 1967 na tangia muda huo milima hiyo imekaliwa na Israeli.

Nini kitajiri katika vita hiyo ambayo itaaqnza kukolezwa muda huu wa usiku wa kuamkia jumanne?

NB:
Tafadhali Mods ninawaomba kuuweka uzi huu Live ili tuendelee kuleta yale yanojiri katika eneo la mashariki ya kati.
 
Ni ngumu sana kuizuia marekani kupeleka silaha Israel hatakama hao houth wapewe silaha gani, marekani ni Israel na Israel ni marekani,
Vyombo vya magharibi vimekuwa vikifurahia hatua ambazo Israeli imechukua hadi sasa ya kubomoa uwezo wa Hezbollah kuweza kurusha makombora zaidi kwenda Tel-Aviv, lakini hatua ya kuingiza vikosi vya ardhini ni risk kubwa kwa sababu niloitaja hapo juu.

Kuhusu Wahudhi na Marekani ni kweli wahudhi hawawezi kuzuia lakini watasababisha ucheleweshaji wa kupelekwa silaha zaidi kwa Israeli yaani "disruption".
 
Vitongoji kadhaa vya mji wa Beirut vimetikiswa na mashambulizi ya makombora yanoendelea kufanywa na Israeli usiku huu.

Maeneo ya haya kama ya Tyre yalipigwa makombora katika vita vya mwaka 2006 na Israeli imedai kuwa maeneo haya yenye makazi ya watu yamekuwa yakitumiwa na wapiganaji wa Hezbollah kuficha silaha zao.
 
Bila unafiki na kuwa biased, haimaanishi covert ops za Israel akisaidiwa na US kuua top leaders wa Hezbollah ndio uhakika kuiondoa Hezbollah hapo....

Israel itazika askari wengi sana hapo, hao Hezbollah huo ukimya kuna tukio la surprise watafanya..

Ukichunguza kwa umakini na matukio yanavyokwenda haraka haraka utagundua Israel wana vipandikizi ndani ya Hezbollah..

Hivyo Israel hawatoi ahueni au muda wa Hezbollah kujipanga kujisahihisha kupanga mikakati na kuondoa hao rats/traitors..

Israel hawataki supu ipoe, ikipoa hailiwi...
Wana intel za siri nyingi CIA wamewaoa ambazo zikitumika vyema wataweza kuidhibiti Hezbollah, ina maana kama wana ramani za silaha zilipo, hawataki kutoa mwanya Hezbollah wazihamishe..

Ndio maana wanaingia Lebanon haraka haraka wamalize kazi... Kabla mapandikizi yao hawajastukiwa ndani ya Hezbollah au intel zao hazijawa useless..

Ngoja tuone...
 
and 100 others

Uko sawa kabisa lakini ni hiyo mission ya kuhakikisha miundombinu yote yaharibiwa na itategemea na taarifa za kijasusi kutoka kwa makomandoo wa IDF.

Ila kiukweli hii operesheni ya sasa IDF na Israeli waliichukulia kuwa ni "Case Study" ya ile vita ya 2006 kwamba wapi walikosea na wapi pahitaji kujiongeza.

Lakini tukio la kuanza kuwavunja nguvu Hezbollah kwa kuauwa wale makamanda wao wakubwa laweza kuwa ni moja ya hatua kubwa katika kutaka kuumaliza mbuyu wa Axis of Resistance.

Ni miaka sita ilopita yaani mwaka 2018 kijana mdogo jasusi wa Israeli alikuja na ripoti ya maendeleo ya Hezbollah na akawajulisha wakubwa wake wa kazi kwamba surveillance kwa Hezbollah imegundua kuwa wameamua kutumia "pagers"na na zile radio ndogo za walkie talkies kwa ajili ya mawasiliano. Hivyo ikawa ni suala la matayarisho kwa kuingilia (intercepting uagizaji wa hizo pagers ambazo yakadiriwa Hezbollah waliagiza kama 3000 hivi).

Kilofuata hapo ni story ndefu lakini kukata kidogo tukasikia kumetokea milipuko, watu waulizana na "consignment" imeingiliwaje hakuna anaefahamu ila ni kazi ya miaka zaidi ya sita ya ujasusi na surveillance ya Israeli na upofu wa Hezbollah katika kugundua (infiltration).
 
1727736623088.png

Leo jumatatu mchana ndege za kivita za Israeli zimeshambulia majengo ya makazi katika eneo liitwalo Kola mjini Beirut. Picha ikionyesha moja ya majengo hayo ambalo limebomolewa hadi kuwa kifusi. Picha na Getty.
 
Marjayoun- Lebanon.

Israeli imetangaza kuingiza majeshi yake upande wa kusini mwa Lebanon na kuliweka eneo hilo chini ya jeshi la IDF yaani "military Zone". Hatua hiyo yafuatia uamuzi ulofanywa na Israeli na kuwaatarifu Marekani kwamba wameamua kuingiza majeshi ya ardhini nchini Lebanon.

Maeneo ya Metula, Misgav Am na Kfar Galadi yaliyoko upande wa kaskazini mwa Israeli yote yamefungwa kwa ajili ya IDF kuyatumia. Naibu kiongozi wa hezbollah Naim Qassim ametoa onyo kwa Israeli kuwa endapo IDF itaingia Lebanon kwa ajili ya vita ya ardhini basi Hezbollah wapo tayari.

Majeshi ya IDF khasa yale maalum au Special Forces tayari yapo ndani ya Lebanon huku vikosi vingine vikiendelea kusogea karibu na mpaka kutokea sehemu ya Kiryat Shmona. Vikosi vya makomandoo wa IDF vitakuwa vikitafuta upenyo wa kuingiza na kupandkiza mabomu ili kuwezesha vifaru kusogea ndani zaidi.

Israeli wamesema watatumia njia zote za ardhini, angani na majini kutimiza azma yao ya kupigana na Hezbollah vita ambayo ni ya pili baada ya vita ilopiganwa mwaka 2006 vita ambayo haikutoa mshindi yoyote. waziri mkuu Benjamin Netanyahu ametoa onyo kwa Iran kuwa hakuna eneo lolote ambalo Israeli itashindwa kulipiga.

Vifaru vya kijeshi vya IDF vimesogea mpakani na Lebanon huku naibu kiongozi wa wa Hezbollah akisema kuwa wapiganaji wa Hezbollah wapo tayari kwa vita ambayo kitaalamu yaiotwa Asymmetrical Warfare pale ambapo Hezbollah watatumia mbinu iitwayo "gollila tactics" dhidi ya jeshi la IDF lenye kila aina ya zana ya kijeshi ijulikanayo ulimwenguni.

Lengo kuu ya Israeli ni kubomoa miundombinu ya Hezbollah ambayo yajumuisha njia za chini kwa chini (Tunnels) na njia za panya ambazo Hezbollah huzitumia kupitisha silaha zao na bidhaa zingine kutoka nje. Pia lengo hilo limekusudia kuhakikisha wananchi wa Israeli wanoishi upande wa Kaskazini ambao wamekimbia, warudi katika makazi yao.

Kwanini hali hii imefikia hapa?

Terehe 17 hadi 18 mwezi huu vifaa vya mawasiliano yaani "pagers" wanotumia Hezbollah vililipuka pamoja na radio za mawasiliano.

Tarehe 23 hadi 24 Israeli ikafanya mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege za kivita dhidi ya maeneo ya Hezbollah.

Tarehe 27 Septemba kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akauawa katika shambulio kubwa la bomu liitwalo "banker" lilofurumusha majengo na handaki walokuwamo Nasrallah na wenzie.

Tarehe 30 yaani leo jumatatu kiongozi wa Hamas aliekuwepo Lebanon nae ameuawa baada ya Israeli kushambulia tena kwa dege za kivita eneo hilo la kusini mwa Lebanon.

Wachambuzi wengi wa kijeshi na kijajusi wametoa tahadhari kwa Israeli kwamba hata kama safari hii wamejifunza mengi kutokana na vita ya mwaka 2006 lakini pia Hezbollah nao pamoja na kuuliwa kwa viongozi wake wengi kutokana na mashambulizi mengi aloyafnya Israeli, bado wana shaka kuwa Israeli itaweza kupigana vita ya ardhini.

Vita hii ya ardhini ambayo ni rahisi kuingia lakini ngumu kutoka, safari hii imekusanya makundi ya wapiganaji wanojiita "Axis of Resistance" yanojumuisha makundi ya kutoka Lebanon, Hamas, kutoka nchi za Irak na Syria pamoja na kundi la Houdh la Yemen na wote wakiwa na silaha walopewa na Iran.

Wahudhi wamepewa jukumu la kuhakikisha Marekani hapeleki silaha zaidi Israeli huku makundi yaliyoko Syria na Irak wakihakikisha wanatuma makombora upande wa kaskazini mwa Israeli kulipo milinma maarufu ya Golan ambayo Israeli huitumia kufanya doria dhidi ya Syria na Irak.

Milima ya Golan ilipokwa na Israeli baada ya vita ya siku sita ya mwaka 1967 na tangia muda huo milima hiyo imekaliwa na Israeli.

Nini kitajiri katika vita hiyo ambayo itaaqnza kukolezwa muda huu wa usiku wa kuamkia jumanne?

NB:
Tafadhali Mods ninawaomba kuuweka uzi huu Live ili tuendelee kuleta yale yanojiri katika eneo la mashariki ya kati.
Breaking: Israel imemuua Hassan Khalil Yassin, aliyechukua nafasi ya Hassan Nasrallah masaa machache yaliyopita.

Hii inavunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa muda mfupi zaidi kama mkuu wa shirika la kigaidi.

Yaaan Hassan baada ya kuuwawa basi wakateua bwana Hassan Yasin kushika nafasi naye hakumaliza masaa

Netanyahu kaiambia dunia kwamba mkono wa israel hakuna sehemu hauwezi fika dunian
 
Back
Top Bottom