Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Marjayoun- Lebanon.
Kifaru cha jeshi la Israeli kilifanya doria kwenye mpaka wa Israeli na Lebanon mapema leo asubuhi. Picha na Aya Margolin wa Flash90
Israeli imetangaza kuingiza majeshi yake upande wa kusini mwa Lebanon na kuliweka eneo hilo chini ya jeshi la IDF yaani "military Zone". Hatua hiyo yafuatia uamuzi ulofanywa na Israeli na kuwaatarifu Marekani kwamba wameamua kuingiza majeshi ya ardhini nchini Lebanon.
Maeneo ya Metula, Misgav Am na Kfar Galadi yaliyoko upande wa kaskazini mwa Israeli yote yamefungwa kwa ajili ya IDF kuyatumia. Naibu kiongozi wa hezbollah Naim Qassim ametoa onyo kwa Israeli kuwa endapo IDF itaingia Lebanon kwa ajili ya vita ya ardhini basi Hezbollah wapo tayari.
Majeshi ya IDF khasa yale maalum au Special Forces tayari yapo ndani ya Lebanon huku vikosi vingine vikiendelea kusogea karibu na mpaka kutokea sehemu ya Kiryat Shmona. Vikosi vya makomandoo wa IDF vitakuwa vikitafuta upenyo wa kuingiza na kupandkiza mabomu ili kuwezesha vifaru kusogea ndani zaidi.
Israeli wamesema watatumia njia zote za ardhini, angani na majini kutimiza azma yao ya kupigana na Hezbollah vita ambayo ni ya pili baada ya vita ilopiganwa mwaka 2006 vita ambayo haikutoa mshindi yoyote. waziri mkuu Benjamin Netanyahu ametoa onyo kwa Iran kuwa hakuna eneo lolote ambalo Israeli itashindwa kulipiga.
Vifaru vya kijeshi vya IDF vimesogea mpakani na Lebanon huku naibu kiongozi wa wa Hezbollah akisema kuwa wapiganaji wa Hezbollah wapo tayari kwa vita ambayo kitaalamu yaitwa Asymmetrical Warfare pale ambapo Hezbollah watatumia mbinu iitwayo "gollila tactics" dhidi ya jeshi la IDF lenye kila aina ya zana ya kijeshi ijulikanayo ulimwenguni.
Lengo kuu ya Israeli ni kubomoa miundombinu ya Hezbollah ambayo yajumuisha njia za chini kwa chini (Tunnels) na njia za panya ambazo Hezbollah huzitumia kupitisha silaha zao na bidhaa zingine kutoka nje. Pia lengo hilo limekusudia kuhakikisha wananchi wa Israeli wanoishi upande wa Kaskazini ambao wamekimbia, warudi katika makazi yao.
Kwanini hali hii imefikia hapa?
Tarehe 17 hadi 18 mwezi huu vifaa vya mawasiliano yaani "pagers" wanotumia Hezbollah vililipuka pamoja na radio za mawasiliano.
Tarehe 23 hadi 24 Israeli ikafanya mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege za kivita dhidi ya maeneo ya Hezbollah.
Tarehe 27 Septemba kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akauawa katika shambulio kubwa la bomu liitwalo "bunker" lilofurumusha majengo na handaki walokuwamo Nasrallah na wenzie.
Tarehe 30 yaani leo jumatatu kiongozi wa Hamas aliekuwepo Lebanon nae ameuawa baada ya Israeli kushambulia tena kwa dege za kivita eneo hilo la kusini mwa Lebanon.
Wachambuzi wengi wa kijeshi na kijajusi wametoa tahadhari kwa Israeli kwamba hata kama safari hii wamejifunza mengi kutokana na vita ya mwaka 2006 lakini pia Hezbollah nao pamoja na kuuliwa kwa viongozi wake wengi kutokana na mashambulizi mengi aloyafanya Israeli, bado wana shaka kuwa Israeli itaweza kupigana vita ya ardhini.
Vita hii ya ardhini ambayo ni rahisi kuingia lakini ngumu kutoka, safari hii imekusanya makundi ya wapiganaji wanojiita "Axis of Resistance" yanojumuisha makundi ya kutoka Lebanon, Hamas, kutoka nchi za Irak na Syria pamoja na kundi la Houdh la Yemen na wote wakiwa na silaha walopewa na Iran.
Wahudhi wamepewa jukumu la kuhakikisha Marekani hapeleki silaha zaidi Israeli huku makundi yaliyoko Syria na Irak wakihakikisha wanatuma makombora upande wa kaskazini mwa Israeli kulipo milinma maarufu ya Golan ambayo Israeli huitumia kufanya doria dhidi ya Syria na Irak.
Milima ya Golan ilipokwa na Israeli baada ya vita ya siku sita ya mwaka 1967 na tangia muda huo milima hiyo imekaliwa na Israeli.
Nini kitajiri katika vita hiyo ambayo itaaqnza kukolezwa muda huu wa usiku wa kuamkia jumanne?
NB:
Tafadhali Mods ninawaomba kuuweka uzi huu Live ili tuendelee kuleta yale yanojiri katika eneo la mashariki ya kati.