Israeli yatangaza rasmi kuingiza majeshi nchini Lebanon upande ya kusini. Nini kitajiri baada ya hatua hii ngumu ya Israeli?

Israeli yatangaza rasmi kuingiza majeshi nchini Lebanon upande ya kusini. Nini kitajiri baada ya hatua hii ngumu ya Israeli?

Israel inaripotiwa kuingiza jeshi ndani ya mipaka ya kusini mwa Lebanon ikiwa na lengo la kupambana na Hizbollah.
Uvamizi huo ulianza jana tarehe 30 September 2024.
Leo ni Oktoba mosi.
Je,ya 2006 yatajirudia ama Lebanon inaenda kuwa Gaza mpya!?
Screenshot_2024-10-01-13-03-04-34_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
Screenshot_2024-10-01-13-03-11-51_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
 
Israel inaripotiwa kuingiza jeshi ndani ya mipaka ya kusini mwa Lebanon ikiwa na lengo la kupambana na Hizbollah.
Uvamizi huo ulianza jana tarehe 30 September 2024.
Leo ni Oktoba mosi.
Je,ya 2006 yatajirudia ama Lebanon inaenda kuwa Gaza mpya!?View attachment 3112023View attachment 3112024
Ulikuwa umelala bado habari hii imetoka tarahe 1 iliposoma tu Israel ilipanga iwe recorded Tarehe moja October 2024

Mod unganisha hii thread
 
Maisraeli yanapenda vita kuliko hata ngono. YAMELAANIWA
Si kwamba Israeli yapenda vita bali ni client state kwa niaba ya Marekani katika kulinda maslahi na kihakikisha usalama wa eneo la Mashariki ya kati wa ajili ya ustawi na ukuaji wake. Ni kama ilivyo kwa Ukraine itumiwavyo na NATO na Marekani dhidi ya Russia.

Lengo kuu la Marekani ni kuliunda upya eneo hilo la mashariki ya kati kikwazo akiwa ni Iran hivyo Iran akijichanganya atakuwa kitoweo.

Ukipata muda msikilize tena Benjamini Netanyahu katika hotuba aloitoa juzi UN akielezea mikakati ya Mashariki ya kati mpya na huku aliilenga Iran kuwa ni kikwazo.

Mara tu baada ya hotuba ile akanyanyua simu na baadae Nasrallah akamalizwa.
 
Updates:Hezbollah yakanusha kwamba majeshi ya Israeli yamevuka mpaka kuingia kusini mwa Lebanon.

Hapa ni vita ya propaganda na kisaikolojia.

Wakti huohuo Uturuki imesema jaribio la Israeli kuingiza majeshi ya ardhini kusini mwa Lebanon ni kinyume cha sheria za kimataifa na yakiuka maslahi na heshima ya mipaka ya Lebanon.

Jeshi la kulinda amani la umoja wa mataifa limesema limetaarifiwa na Israeli juu ya operesheni yake kusini mwa Lebanon.

Operesheni hii ya Israeli yaitwa Operation Arrow.

Russia imesema yafuatilia kwa makini operesheni ya Israeli katika nchi za Lebanon na Syria.
 
Marjayoun- Lebanon.

Israeli imetangaza kuingiza majeshi yake upande wa kusini mwa Lebanon na kuliweka eneo hilo chini ya jeshi la IDF yaani "military Zone". Hatua hiyo yafuatia uamuzi ulofanywa na Israeli na kuwaatarifu Marekani kwamba wameamua kuingiza majeshi ya ardhini nchini Lebanon.

Maeneo ya Metula, Misgav Am na Kfar Galadi yaliyoko upande wa kaskazini mwa Israeli yote yamefungwa kwa ajili ya IDF kuyatumia. Naibu kiongozi wa hezbollah Naim Qassim ametoa onyo kwa Israeli kuwa endapo IDF itaingia Lebanon kwa ajili ya vita ya ardhini basi Hezbollah wapo tayari.

Majeshi ya IDF khasa yale maalum au Special Forces tayari yapo ndani ya Lebanon huku vikosi vingine vikiendelea kusogea karibu na mpaka kutokea sehemu ya Kiryat Shmona. Vikosi vya makomandoo wa IDF vitakuwa vikitafuta upenyo wa kuingiza na kupandkiza mabomu ili kuwezesha vifaru kusogea ndani zaidi.

Israeli wamesema watatumia njia zote za ardhini, angani na majini kutimiza azma yao ya kupigana na Hezbollah vita ambayo ni ya pili baada ya vita ilopiganwa mwaka 2006 vita ambayo haikutoa mshindi yoyote. waziri mkuu Benjamin Netanyahu ametoa onyo kwa Iran kuwa hakuna eneo lolote ambalo Israeli itashindwa kulipiga.

Vifaru vya kijeshi vya IDF vimesogea mpakani na Lebanon huku naibu kiongozi wa wa Hezbollah akisema kuwa wapiganaji wa Hezbollah wapo tayari kwa vita ambayo kitaalamu yaiotwa Asymmetrical Warfare pale ambapo Hezbollah watatumia mbinu iitwayo "gollila tactics" dhidi ya jeshi la IDF lenye kila aina ya zana ya kijeshi ijulikanayo ulimwenguni.

Lengo kuu ya Israeli ni kubomoa miundombinu ya Hezbollah ambayo yajumuisha njia za chini kwa chini (Tunnels) na njia za panya ambazo Hezbollah huzitumia kupitisha silaha zao na bidhaa zingine kutoka nje. Pia lengo hilo limekusudia kuhakikisha wananchi wa Israeli wanoishi upande wa Kaskazini ambao wamekimbia, warudi katika makazi yao.

Kwanini hali hii imefikia hapa?

Terehe 17 hadi 18 mwezi huu vifaa vya mawasiliano yaani "pagers" wanotumia Hezbollah vililipuka pamoja na radio za mawasiliano.

Tarehe 23 hadi 24 Israeli ikafanya mashambulizi ya anga kwa kutumia ndege za kivita dhidi ya maeneo ya Hezbollah.

Tarehe 27 Septemba kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akauawa katika shambulio kubwa la bomu liitwalo "banker" lilofurumusha majengo na handaki walokuwamo Nasrallah na wenzie.

Tarehe 30 yaani leo jumatatu kiongozi wa Hamas aliekuwepo Lebanon nae ameuawa baada ya Israeli kushambulia tena kwa dege za kivita eneo hilo la kusini mwa Lebanon.

Wachambuzi wengi wa kijeshi na kijajusi wametoa tahadhari kwa Israeli kwamba hata kama safari hii wamejifunza mengi kutokana na vita ya mwaka 2006 lakini pia Hezbollah nao pamoja na kuuliwa kwa viongozi wake wengi kutokana na mashambulizi mengi aloyafnya Israeli, bado wana shaka kuwa Israeli itaweza kupigana vita ya ardhini.

Vita hii ya ardhini ambayo ni rahisi kuingia lakini ngumu kutoka, safari hii imekusanya makundi ya wapiganaji wanojiita "Axis of Resistance" yanojumuisha makundi ya kutoka Lebanon, Hamas, kutoka nchi za Irak na Syria pamoja na kundi la Houdh la Yemen na wote wakiwa na silaha walopewa na Iran.

Wahudhi wamepewa jukumu la kuhakikisha Marekani hapeleki silaha zaidi Israeli huku makundi yaliyoko Syria na Irak wakihakikisha wanatuma makombora upande wa kaskazini mwa Israeli kulipo milinma maarufu ya Golan ambayo Israeli huitumia kufanya doria dhidi ya Syria na Irak.

Milima ya Golan ilipokwa na Israeli baada ya vita ya siku sita ya mwaka 1967 na tangia muda huo milima hiyo imekaliwa na Israeli.

Nini kitajiri katika vita hiyo ambayo itaaqnza kukolezwa muda huu wa usiku wa kuamkia jumanne?

NB:
Tafadhali Mods ninawaomba kuuweka uzi huu Live ili tuendelee kuleta yale yanojiri katika eneo la mashariki ya kati.
🇱🇧🇮🇱 | Hezbollah’s Media Relations Officer Mohammad Afif to Reuters: 'No Israeli troops have entered Lebanese territory. The strikes on Tel Aviv earlier were only the beginning'

@MilitaryPOV
 
Israel inaripotiwa kuingiza jeshi ndani ya mipaka ya kusini mwa Lebanon ikiwa na lengo la kupambana na Hizbollah.
Uvamizi huo ulianza jana tarehe 30 September 2024.
Leo ni Oktoba mosi.
Je,ya 2006 yatajirudia ama Lebanon inaenda kuwa Gaza mpya!?View attachment 3112023View attachment 3112024
🇱🇧🇮🇱 | Hezbollah’s Media Relations Officer Mohammad Afif to Reuters: 'No Israeli troops have entered Lebanese territory. The strikes on Tel Aviv earlier were only the beginning'

@MilitaryPOV
 
Tatizo Israel wanatuchanganya sana Wanalebanon

Walituvamia kwa njia ya anga na kuua Viongozi wetu tukajipanga kutafuta namna ya kuziona Drones zao kwa rada ikashindikana....

Kabla ya kumaliza hilo sasa wanatuvamia kwa njia ya Ardhi na vifaru vyao

Sasa sisi tufanyaje jamani?
Ok. Very simple. Wanalebanon; 1. Wakataeni Hezbollah kwani hao sio wenzenu kabisa-ona walipowafikisha sasa.
2. Muwe watiifu na Wepesi wa kuzingatia na utekelezaji kikamilifu maelekezo yatolewayo na IDF.
3. Acheni ushabiki wa Kidini. Hiyo vita asilani sio ya kidini.
4. Beba bendera nyeupe (ishara ya AMANI) esp. mnapokuwa wengi/Kikundi kwa pamoja.
 
Ok. Very simple. Wanalebanon; 1. Wakataeni Hezbollah kwani hao sio wenzenu kabisa-ona walipowafikisha sasa.
2. Muwe watiifu na Wepesi wa kuzingatia na utekelezaji kikamilifu maelekezo yatolewayo na IDF.
3. Acheni ushabiki wa Kidini. Hiyo vita asilani sio ya kidini.
4. Beba bendera nyeupe (ishara ya AMANI) esp. mnapokuwa wengi/Kikundi kwa pamoja.
Lebanon iko hoi, si taifa imara tena.

Itachukua miaka mingi kwa Lebanon kuja kusimama kama taifa huru.
 
Hezbollah kuanzia jana wamevua magwanda yao wanavaa Kiraia wanaogopa kifo.
AaaH! Mambo ya kuweka mpira kwapani waturudishie viingilio vyetu. Eti wanavaa kiraia? yani wao sio wapiganaji tena?? Kwa hiyo wamerejelea uvaaji wa vipedo, kobazi, hijabu na kujificha nyuma ya makalio ya akina mama na watoto?
 
Nchi ama vikundi vingine vya magaidi inatakiwa wajifunze sasa kuwa Iran anawatumia kwenye maslahi yake tuu wakati wa kipigo yeye anakaa pembeni.
Lakini mkuu, Marekani awatumia Israeli na Ukraine kwa kazi zake kujitengenezea himaya zaidi duniani.

Marekani ataka Ukraine, ataka eneo la Pasific akimtumia taiwan na pia ataka eneo la mashariki ya kati akimtumia Israeli.

Kikwazo Mashariki ya kati ni Iran, Ukraine ni Russia na Kusini mwa Asia ni China.
 
Rabin alikuwa na tatizo gani au unakurupuka tuu.
Yitzhak Rabin aliuawa kwa baada ya kusaini mkataba wa Oslo mwaka 1994 na kiongozi wa wapalestina Yaser Arafat maarufu kama Oslo Accord.

Kwa kusaini mkataba huo Rabin akauawa (assassinated) na muisraeli mwenye msimamo mkali Yigar Amir mwaka 1995.

Leo hii waisraeli wenye msimamo mkali wameapa kwamba wataiangusha serikali ya Israeli endapo Benjamin Netanyahu atasaini mkataba wowote wa makubaliano na wapalestina.

Ndo maana suala la "two state solution" bado lachungulia dirishani na hii vita aloianzisha Netanyahu ni katika pia kujitengeneza na kujiimarisha kisiasa baada ya rekodi yake kuvurugwa na shambulizi la Hamas mwaka jana.
 
Back
Top Bottom